Ticker

6/recent/ticker-posts

BUSINESS PLAN

BUSINESS PLAN ( MPANGO BIASHARA)
Business plan au mpango biashara ni ramani ambayo inaenesha namna unavyotegemea kuendesha biashara na malengo mahususi ya biashara yako.
Mpango biashara (business plan) inapanuka kulingana na biashara yako inavyotanuka, ikiwa umeandika mpango biashara ukitegemea mtaji wa milioni moja biashara yako ikipanuka na kuwa na mtaji wa milioni kumi utahitaji kuandika busness plan mpya au kuipnua zaidi ile ya kwanza ili iendane na mtaji wako.




*UMUHIMU WA BUSINESS PLAN.* 

i)  Mpango huo unaelezea njia ambayo mfanya biashara au mjasiriamali anayopaswa kupitia kipindi chote cha uendeshaji wa biashara yake. Katika biashara lazima kuwepo na kanuni na taratibu, hivyo basi ili biashara yako ikue lazima kuwe na njia unazopaswa kupitia, na kupitia business plan kila kitu kitakuwa kimejipambanua humo. 

ii) Husaidia wawekezaji, watu wa mabenki na wafadhili wengine kuelewa na kumkubali mfanya biashara kwa ajili ya uwekezaji wao katika biashara yake.  Lazima utambue kuwa popote utakapo hitaji kwenda kupata msaada wa kuongeza mtaji (mkopo) kwa ajili ya kukuza biashara yako lazima uwe na mpango kazi huu ili kumuwezesha huyo anayetaka kuwekeza kwako au kukupatia mkopo kuona ni kwa kiasi gani unaweza kunufaika na huo mkopo. 

iii)  Mpango kazi mzuri utakusaidia kukuza biashara yako kirahisi maana inasaidia kuwaonyesha wafadhili wako kuwa soko la bidhaa zako lipo, na usimamizi wa biashara yako upo imara kwa ajili ya kutoa huduma nzuri. 

iv) Business Plan nzuri humsaidia mfanya biashara kupunguza gharama zisizo za lazima  na kuepusha uwezekano wa biashara yake kushindwa kuendelea. 

v) Humsaidia mfanyabiashara kujiendeleza kiutawala na kiujuzi. 

vi) Hutumika kama kiunganishi kati ya mfanya biashara na wadau mbali mbali.  Mpango biashara huchukua nafasi kubwa katika kujipambanua kwa watu mbali mbali maana hutoa ufafanuzi wa kina juu ya biashara yako. 

SEHEMU KUU ZA BUSINESS PLAN.
Mpango biashara unakuwa na sehemu kuu sita, nazo ni kama ifuatavyo:

1.MUHTASARI WA BIASHARA
2.UTAMBULISHO WA BIASHARA AU KAMPUNI.
3.UTAFITI KUHUSU SOKO
4. BIDHAA AU HUDUMA UTAKAZOTOA.
5. MAUZO NA MANUNUZI.
6. MPANGO WA KIFEDHA.

1.MUHTASARI WA BIASHARA  ( Executive summary)
Katika sehemu hii vitu vifuatavyo vinatakiwa kuonekana:
   .Tambulisha biashara yako, biashara yako itakuwa inajihusisha na nini hasa, mfano: Biashara ya nafaka na mazao ya chakula.
    .Ainisha wateja ambao umelenga kuwauzia bidhaa au utakuwa unawapatia huduma.
     .Iandike kwa ufupi na iwe na nguvu yaani ibebe ujumbe wote kuhusu biashara yako
      . Elezea namna biashara yako itakavyokuwa na kufanikiwa zaidi.

2. UTAMBULISHO AU UFAFANUZI WA BIASHARA (Business description).
   .Toa maelezo ya hali ya juu sana kuhusu biashara unayotaka kuianzisha.
    . Ni namna gani utaendesha biashara yako na namna gani utatengeneza pesa kupitia biashara yako .
   . Husisha njozi yabiashara yako na mahali utakapoifanyia hiyo biashara.
    . Ainisha waajiriwa utakaowatumia kuboresha biashara yako, Hawa ndio wataifanya biashara yako kuwa bora na ya kipekee. Husisha watu kama, wahasibu, wanasheria, n.k

3.UTAFITI KUHUSU SOKO (market research).
    . Onyesha kwa undani ni kwa jinsi gani umetumia muda wako kutafiti soko la bidhaa zako.
    . Elewa kwa undani upatikanaji wa bidhaa (industry) na soko ulilolenga.
     . Pima ushindani katika biashara yako, waelewe kwa undani washindani wako na namna utakavyotumia mapungufu yao ili kufanta biashara yako kuwa bora zaidi ya washindani wako.
     . Elezea namna utakavyoshughulikia uhalali au namna uatakavyofanya biashara yako kuwa halali, Namba utakavyosajili biashara yako, Na namna ya kupata nyaraka halali za bishara yako kama lessen n.k.


4. BIDHAA NA HUDUMA UTAKAZOTOA (Products or Services)
    .Ni bidhaa gani utauza?
    .Ni kwa namna gani bidhaa zako zitakidhi mahitaji ya wateja wako?
     .Namna gani bidhaa zako na huduma zako zitashinda ushindani katika soko.
     . Elezea kwa ufupi maendeleo ya biashara yako kwa muda huu.

5.MAUZO NA MANUNUZI (Marketing and sales).
     .Elezea namna unavyowafahamu wateja wako, ni kipindi gani na kwa njia gani utawafikia.
     . Elezea njia utakazotumia kuendesha biashara au njia za kuuza. Mfano, kuuza kwa njia ya mtandao (online selling), Uuzaji wa moja kwa moja (direct selling), kumfuata mteja mahali alipo, n.k.

6.MPANGO WA KIFEDHA (Finencial projection).
    . Gusia kuhusu wawekezaji na wakopeshaji utakaowatumia kupata mtaji.
     . Elezea namna ambavyo biashara yako itatimiza vigezo vya kifedha, na namna gani utadumisha uwiano wa kifedha, mfano, kiasi gani biashara yako itaingiza kwa mwezi, mwaka, miaka mitano n.k.
     . Ikiwa unatarajia kuchukua mkopo hakikisha unaweka mipango madhubuti ya namna itakavyoweza kurudisha pesa utakazokopa.
     . Ni muhimu kuainisha kiwango cha pesa unachotaka kukopeshwa na namna utakavyozitumia.

Hizo ndizo sehemu kuu za mpango biashara (business plan). Namna mpango biashara utakavyokuwa umeandaliwa vizuri ndivyo biashara itakavyokua zaidi.
Weka picha ya biashara yako kupitia business plan ili upate nguvu ya kuifikia hiyo picha.


Makala hii imeandaliwa na
Mwalimu Robert Lucas, unaweza kuwasiliana naye kwa +255764075392 / +255713056903.
Email: lucastrngwakwa@gmai.com.

Kwa taarifa zaidi kuhusu business plani tembelea,   www.satnavcoaching.com

Mwenyezi Mungu awe nawe unapoelekea mafanikio yako.