NJIA YA MAFANIKIO ILIYONYOOKA...
Kutoka Misri kwenda kaanani ambayo kwa sasa inapatikana katika nchi za Palestina, Israeli na Lebanini ni takribani kilomita 613.
Mungu alikusudia wana wa Israeli wasafiri kwa muda wa siku arobaini(40) tu kutoka Misri kwenda kaanani lakini kwa sababu ya kutokuamini kwao na maovu yao ili walazimu kuzunguka jangwani muda wa miaka 40
Biblia katika kitabu cha hesabu 32:13 imeandikwa
13 "Na hasira za Bwana ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huku jangwani muda wa miaka arobaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa Bwana kikaisha angamia".
Wakati mwingine katika maisha yako utachelewa kufika kule unakoenda siyo kwa sababu ni mbali bali kwa sababu unajifanya mjuaji hautaki kukubali kuelekezwa na Yule anayeijua kesho yako yaani MUNGU.
Mara zote kabla hujaanza safari katika kufanikisha jambo fulani, kama unataka lifanikiwe kwa haraka kaa chini umuulize kwanza yeye mwenye uwezo wa kuiona kesho kabla haijaitwa Leo.
Yeye anaweza kukuelekeza shortcut ambayo kama ungeenda peke yako ingeweza kukugharimu maisha yako yote pasipo kufika unakoenda.
Ezra katika safari yake ya kwenda kuujenga upya mji wa Yerusalemu baada ya kukaa utumwani kwa muda mrefu alikaa chini ili kumuuliza Yeye anayeijua njia (MUNGU) kile wanachopaswa kukifanya.
Ezra 8:21-23 imeandikwa
21 Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.
22 Maana naliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao.
23 Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali.
Baada ya hapa Ezra anapata hekima ipitayo hekima zote kutoka kwa Mungu na baada ya hapo kazi yako inakuwa rahisi sana.
Chini ya usimamizi wa Nehemia kazi ambayo ingeweza kufanyika kwa muda wa miaka kadhaa sasa inakamilika ndani ya siku hamsini na mbili (52) tu kwa sababu walikubali kujinyenyekeza ili waongozwe hivyo wakapokea Nguvu isiyo ya kawaida kutoka kwa Mungu mwenye nguvu zote.
(Nehemia 6:15)
Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili.
Itoshe tu kusema kwamba kama unataka kufikia mafanikio uliyokuwa unayatamani kwa haraka, Acha kuwa mjuaji, Jinyenyekeze kubali kuongozwa. Nakuhakikishia ndani ya muda mfupi utarudi hapa na ushuhuda.
Je Mwaka huu umepanga njia yako ya mafanikio iwe imenyooka au iliyopinda pinda?
*Niandikie kwenye sehemu ya comment, Usisahau kushare na kulike*
*"Live an inspired Life"*
Mwl Robert
