Ticker

6/recent/ticker-posts

HATUA SABA (7) ZA MAFANIKIO.
Mwandishi na muelimishaji maarufu katika maswala ya Maisha na mafanikio ya kiuchumi Anayejulikana kwa jina la Brian Tracy Alisema, "Personal success needs self discipline". Akimaanisha kuwa mafanikio binafsi yanahitaji nidhamu binafsi. Kuwa na nidhamu wewe mwenyewe kufanya kile ambacho unjua unatakiwa kukifanya ili kuweza kuwa bora zaidi katika uwanja wako.

Nidhamu binafsi ni nini?
Nidhamu binafsi ni ule uwezo wa kujiamrisha wewe mwenyewe kufanya kile unachotakiwa kukifanya, ukifanye kwa wakati gani, ukiwa unajisikia kukifanya au hujisikii kukifanya.
Je kuna maamuzi gani ambayo unahitajika kuyafanya Leo ili kuanza safari yako ya kuelekea juu ya njozi yako?,  Fanya maamuzi hayo leo.
Tendo hili peke yake linaweza kubadilisha mwelekeo Mzima wa maisha yako.


Zipo hatua kuu Saba ambazo kila Mtu mwenye mafanikio huzitumia au zikiwa na marekebisho kidogo Sana ili kuweza kufikia malengo yao. Wewe pia unaweza kuzitumia.
Hatua hizo ni Kama ifuatavyo :-

Hatua ya Kwanza: Amua au chagua kile unachokihitaji. Katika kila sehemu ni lazima uchague kile unachokihitaji, uwe na vitu mahususi kabisa unavyovihitaji na kuvifanya.

Hatua ya pili: Andika vizuri vitu unavyotaka kuvifanya na kwa ndani. (Think on paper).  "Malengo ambayo hayapo katika maandishi siyo malengo". Hayo yatakuwa ni matakwa au matamanio tu na hayana nguvu yoyote ya kuyasukuma.

Hatua ya tatu: Weka tarehe au siku ya mwisho ya kufanyia kazi malengo yako (set deadline for your 4th goals). Siku ya Mwisho kwa ajili ya kutimiza malengo yako ni Kama mfumo wa nguvu ya msukumo katika akili yako. Hii hukuchochea kufanya vitu ambavyo ni vya muhimu ili kufanya malengo yako yawe halisi.

Hatua ya nne: Weka orodha.  Orodhesha kila kitu unachofikiri unahitajika kukifanya ili kufikia malengo yako. Kipindi unapofikiria kazi mpya ama majukumu mapya ya kufanya yaandika Katina orodha yako na endelea kuandika mpaka orodha yako ikamilike.


Hatua ya tano: Pangilia Orodha yako.
Ipange orodha yako ili kupata mpango kazi. Amua ni kipi utafanya kwanza kabla ya kingine na Kipi ni cha muhimu zaidi kuliko kingine.

Hatua ya sita:
Chukua hatua,  Ufanyie kazi mpango kazi wako,  Fanya kitu Tafadhali, fanya kitu chochote ili mradi uwe bize, Endelea kwenda mbele, usibaki hapo ulipo.

Hatua ya Saba:
Kila siku fanya kitu. Fanya kitu kinachokusukuma kukuelekeza kwenye uelekeo wa malengo yako muhimu kwa sasa kila siku.

Unawezaje kuzifanyia kazi hatua hizi?
Kuna vitu vya muhimu viwili unavyoweza kufanya ili mawazo hayo yaweze kufanya kazi.
(a). Amua kabisa kile unachokihitaji, kiandike ukiambatanisha na siku za mwisho wa kukifanyia Kazi (Deadlines), tengeneza mpango kazi na uchukue hatua, fanya angalau lengo moja. Unaweza kufanya Leo??

(b). Hesabu gharama utakazotakiwa kuzilipa ili kufikia malengo yako na uwe bize kulipa gharama hizo. Vyovyote vile jitahidi kulipa gharama.

Brian Tracy alisema msemo wa kiingereza "How To get everything you want faster want than you ever thought possible".

Natumaini tukizingatia hatua hizo tutashangaa namna ambayo tutafanikiwa haraka kutimiza malengo yetu.

Be positive, work hard, make it happen.

Imeandaliwa na Mwl. Robert Lucas
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com.