NJIA 10 ZA KUENDELEA KUBAKI KIJANA.
.Je unahitaji kuendelea kuwa kijana? Nani ambaye hapendi kuendelelea kubaki kijana? Hapa chini ni vidokezo vya namna ya kuendelea kuwa kijana angalau miaka 10 nyuma ya umri wako halisi.
Tahadhali: Usitarajie miujiza au Matokeo ya kulala na kuamka, uvumilivu na nidhamu vinahitajika katika kufuata Sheria hizi ili uweze kufikia malengo.
1. Kunywa kikombe Kisija cha juisi ya mboga mboga kila siku. Judi ya Mboga za majani imejaa viondoa sumu (antioxidants) ambavyo huondoa sumu mwilini (free radicals).
2. Kula angalau vipande vitano vya matunda na kisosi cha mboga za majani kila siku. Uzuri wa mboga za majani na matunda hautakiwi kudharuliwa hata siku moja.
3. Punguza matumizi ya mafuta. Utumiaji wa mafuta mengi huongeza ufanyaji kazi wa free radicals mwilini. Free radical hizi ni ziada ya vile ambavyo mwili wenyewe hauhitaji kuvitumia na badala yake kusababisha uzee. Kutumia mafuta yaliyokwisha tumika ni mazoea hatari sana ambayo watu wengi sana hupenda kuyafanya.
4. Epuka matumizi ya sukari na matumizi ya unga wa nafaka zilizokobolewa.
5. Acha uvutaji wa sigara. Kuvuta sigara kunamfanya Mtu awe mzee miaka Kumi zaidi ya umri wake wa kawaida. Uvutaji wa sigara unazeesha ngozi, na kusababisha mikunjo mikunjo sehemu za midomo na macho.
6. Kula robo tatu (3/4) ya uwezo wako. Usijaze tumbo kupita kiasi, hii inasaidia mfumo wa chakula kufanya kazi vizuri. Katika mlo wako husisha angalau vyakula viwili vyenye madini ya calcium ndani yake kila siku.
7. Fanya mazoezi, Tembea kwa kasi angalau dakika 30- 40 mara kwa mara angalau mara 6 kwa wiki. Inashauriwa kutembea mita 10,000 kwa siku.
8. Jihusishe na marafiki pamoja na wanafamilia wenzako. Kupendwa na kuthaminiwa hufanya kazi kama kifyonza mshituko (shock absorbers) hivyo kuinua kinga ya mwaka.
9. Kuwa na mtazamo chanya kwa nje (positive Outlook). Kuwa na furaha na uchangamfu pia husaidia kuongeza kinga ya mwili na kuzuia uzalishaji wa sumu mwilini.
10. Fanya kile ambacho unakipenda na kukifurahia. Zaidi ya yote fanya kazi zenye maana kwa uaminifu na kuishi maisha binafsi kwa kujitambua na kwa uwajibikaji, hivi vyote huchangia kuwa na amani ya moyo.
Hizo ni dokezo ambazo ukizingatia itakuchukua muda mrefu sana sura yako kuonekana ya kizee.
Motto: Healthily life, live longer.
Makala imeandaliwa na Mwalimu, Robert Lucas
Mawasiliano: +255764075392
lucastrngwakwa@gmail.com
