Ticker

6/recent/ticker-posts


MKAO WA MWILI ULETAO AFYA (Healthy Body posture).
Mkao mzuri wa mwili unahusisha namna unavyoufundisha mwili wako kusimama, kutembea, kukaa na kulala kwa namna ambayo mgandamizo mdogo unakuwa umewekwa kwenye misuli na ligamenti unapokuwa unatembea au unapokuwa umebeba mzigo.
Mkao mzuri wa mwili utakufanya uendelee kuwa na mwonekano wa ujana kwa Muda mrefu zaidi na hata utakapo kuwa Mzee bado muonekano wako utakuwa na mvuto ambao hautakuwa na maumivu ya mifupa na mgongo.
 Mkao mzuri ni wa muhimu zaidi kuliko hata mwonekano mzuri wa uso, kwa sababu mkao mbaya huweza kuathiri mfumo Mzima wa ufanyaji kazi wa mifumo mbalimbali muhimu ya mwili Kama vile Mfumo WA fahamu, mfumo wa mzunguko WA damu,  Mfumo wa hewa pamoja na  mfumo wa Mifupa.

NAMNA YA KUBORESHA MKAO WA MWILI.
Kitu cha kwanza kabisa cha kufanya ili kuboresha mkao wa mwili wako ni kufahamu pale unapokosea pindi unapokuwa umesimama, umekaa au unapokuwa unatembea. Njia nzuri zaidi ya kuweza kufahamu Kama mkao wako ni sahihi au wa kiafya ni kujiangalia wewe mwenyewe wakati ukiwa unatembea. Angalia mwenendo wako kuanzia kichwani mpaka kwenye unyayo.

Weka kumbukumbu za mkao na support ya mgongo. Hii itakusaidia kujua ni wakati gani na sehemu gani zinazopelekea kuwa na mkao mbaya.
Mkao mzuri unaweza kutambulika kwa utembeaji rahisi na mzuri, wakati mkao mbaya husababisha utembeaji kuwa wa kuchosha na usio na Muunganiko mzuri.

Pia baadhi ya watu, hutumia njia ya kuwaomba wengine wawaangalie pindi wanapokuwa wanatembea au wanapokuwa wamekaa.

Njia nyingine ni ile ya kusimama mbele ya kioo. Hii husaidia kufunua na kufahamu mengi Sana kuhusu mkao wako.

VYAKUFANYA NA VISIVYO VYA KUFANYA ILI KUDUMISHA MKAO MZURI.
1. WAKATI UNAPOKUWA UMEKAA.
.Kwa wale ambao hukaa kwenye kompyuta Masaa mengi ni muhimu Kutengeneza tabia ya kukaa katika mkao uletao Afya. Uti wa mgongo haujatengenezwa kubeba uzito Mkubwa kwa muda mrefu katika sehemu moja. Hii inaweza kusababisha maumivu ya pingiri za uti wa mgongo katika siku za mbeleni.
.Wakati unapokuwa umekaa kwenye kiti, sehemu ya chini ya uti wa mgongo (lumber region) lazima ipate msaada wa kutosha. Hii husaidia kuwa na mkao mzuri na kuzuia maumivu ya mgongo katika sehemu ya chini.

Weka compyuta yako usawa wa macho huku ukihakikisha kwamba mikono na kiuna vinapata Msaada wa kiti na meza, wakati kichwa kikiwa kimetulia kwenye Kiti.


2. WAKATI UNAPOKUWA UMESIMAMA.
Watu wengi huwa wana tabia ya kuweka mikono mfukoni pindi wanapokuwa wamesimama. Hii hufanya mabega kujikunja, kwa sababu wakati ukiwa umesimama njia sahihi ya kudumisha mkao mzuri wa mwili ni mikono kuning'inia pembeni ya mwili. Acha nafasi kidogo Kati ya miguu ili iwe sawa na mabega.

Ili uelewe zaidi kuhusu hili jaribu kusimama kwenye ukuta. Kwa watu walio wengi kila kitu vitakuwa vimegusa ukuta isipokuwa kichwa tu. Hii inaashiria kuwa una maendelea mazuri katika zoezi la kuwa na mkao bora. Jaribu kuendeleza tabia  ya kusimama huku mabega yakiwa yamenyoka. Hii husaidia kichwa kunyooka na kuwa kwenye msitari mnyoofu na uti wa  mgongo.

3. WAKATI UNAPOKUWA UNATEMBEA.
Unapokuwa unatembea hakikisha mwili wako umenyooka vizuri.
Usibinue matako, usiinamie mbele wala usikunje mabega pindi unapokuwa unatembea. Unapokuwa unatembea tanguliza kifua mbele, mgongo ukiwa umenyooka, matako msawazo. Kiukweli hili ni zoezi gumu kwa wengi, kuna njia ambayo inashauriwa na wataalamu, njia yenyewe inaitwa (overhead card method)  yaani ni njia ya kutembea ukiwa umeweka kadi juu ya kichwa, baada ya hapo jaribu kufanya hivyo hata kipindi ambapo kadi haipo kichwani. Mwanzoni itakuwa ni ngumu Sana lakini kadri utakavyoendelea mwisho wa siku utazoea na utaona ni kawaida.

4. WAKATI UKIWA UMELALA.
Lalia godoro gumu kwa sababu hulinda mwili wote na kufanya mgongo ubaki umenyoka.
Lala kwa mgongo (chali) badala ya kulala kwa ubavu hii husaidia kuboresha mkao wa mwili. Uti wa mgongo hupata support ya kutosha kutoka kwenye kitanda na mabega huwa katika msawazo mzuri na mwili Mzima.
.kwa wale wanaopenda kutumia mito ya kulalia ni bora zaidi kutumia mito ambayo ni miembamba Kama mara nyingi unalala kwa mgongo.
Unaweza kuweka mto mmoja au zaidi chini ya magoti wakati unapokuwa umelela kwa mgongo ili kupunguza mgandamizo katika sehemu ya chini  ya uti wa mgongo.

5. FANYA MAZOEZI.
Simona  Mara kwa mara kwenye kiti na kujinyoosha kwa vipindi vya muda vinavyofanana, hii itasaidia kuzuia misuli kukaza sababu ya kutopata oxygen ya kutosha.
Watu wanaofanya mazoezi huwa wana mkao bora zaidi ya watu wanaopenda kukaa Sehemu moja muda mrefu.
Jaribu kufanya mazoezi hayo ya kujinyoosha kwa Vipindi Kati ya dakika  15 - 30 katika ratiba yako ya siku na matokeo mazuri utayaona.


Maumivu mengi ya mgongo, misuli na mifupa huweza kusababishwa na mikao mibaya ambayo tunakuwa tunakaa pindi tutembeapo, tukaapo, tusimamapo na wakati tunapokuwa tumelala.
Pia maumivi ya kichwa huweza husababishwa na mkao mbaya wa kichwa, kwa sababu kuchwa kimeungani moja kwa moja na uti wa mgongo.

Robert Lucas
+255764075392
lucastrngwakwa@gmail.com

Motto : Internal power can change the world.