KAMA HAWAFAHAMU UMUHIMU WAKO USILAZIMISHE.
wakati mwingine tunajikuta tunasahaulika katika mamba fulani. Hii haimanishi kuwa kutokushirikiswa katika jambo hilo wewe si wa muhimu La! Hasa. Umuhimu wako upo pale pale ila pengine anayetakiwa kukushirikisha Yeye ndo hatambui umuhimu wako. Kwa hiyo "usiilazimishe maiti kusimama wakati unajua kabisa ni mfu-Marehemu"
USIOMBE KUSHIRIKISWA
Watu wengi huwa wanatamani kushirikishwa hasa katika maswala ambayo yanaonesha kuwa kuna ulaji.
Kushirikishwa katika mambo mazuri na vyema sana lakini watu wengi huwa hawapendi kushirikisha wenzao kwenye fursa mpaka waone kuwa fursa hiyo haina faida, Na ndipo huamua kuwashirikisha wenzao ili tu kama ni hasara wapate wote. Kiufupi WANAKUSHIRIKISHA KWENYE HASARA.
Sikia kisa hiki......
" Kulikuwa na Mfalme mmoja ambaye aliota ndoto ya ajabu sana, Baada ya kuamka asubuhi akawa amesahau ile ndoto aliyoiota hivyo alifadhaika sana kwa kutoikumbuka hiyo ndoto. Mfalme akawaita wasaidizi wake na kuwaambia kilichotokea, Wasaidizi wake wakamshauri Mfalme aite wakuu wa Waganga, wachawi, Wasomi, wataalamu wa nyota na wataalamu wengine ili kwa kutumia hekima zao waweze kumwambia mfalme kile alichoota na tafsri yake. Mialiko ikaenda kwa watu hao ili watu hao wakakusanyike ikulu wamwambie Mfalme ndoto aliyoota na Tafsiri yake. Wale wakuu wakafika wakajaribu kila mtu kutumia ujuzi wake kulingana na kitengo chake wakiamini kuwa mapema tu wangefanikiwa na kupata zawadi kubwa sana kutoka kwa Mfalme. Lakini badala yake mambo hayakuenda kama walivyotarajia, Piga hivi na vile kwa nguvu na akili zao zote lakini wapi! Mwisho wakamwendea mfalme wakamwambia kuwa "Jambo ulilosema haliwezekani!" Mfalme akakasirika sana akawaambia "Kwa vile mmekubariana kunidanganya jambo moja tu linawapasa KUUAWA". Unajua mfalme alikuwa anatumia pesa nyingi sana kuwalipa na kuwatunza hawa watu, Lakini badala ya kufanya kazi waliyopewa wakaanza siasa, Ndiyo maana mfalme alikasirika sana.
Baada ya watu hawa kuona kitumbua kimeingia mchanga wakaanza kuwakimbuka Wenzao ambao huwa wanafanya nao kazi lakini walivyopata mwaliko hawakuwaalika kwa sababu ya Roho mbaya, na wivu kwa kuhofia kuwa ikiwa wamgewaalika na wao posho ambayo wangetakiwa kupata baada ya kumaliza kazi ambayo mfalme angewapa ingepungua Hivyo wakaaMua kwenda peke yao.
Sasa mambo yalipo kuwa magumu wakaanza kutaja "Unajua Mfalme kuna kijana pia huwa tunafanya naye hizi kazi lakini hajaja (kumbuka mwanzoni walikuwa hawamkumbuki) Hivyo Mfalme tunaomba na yeye Aitwe ili na yeye kama Akishindwa tufe wote".
"USIOMBE WATU WAKUSHIRIKISHE KWENYE FURSA BALI SUBIRI MAMBO YAKIWASHINDA WATAKUTAFUTA".
Kijana akaitwa Mbeleza Mfalme, wote waliamini kuwa hata huyu naye atashindwa, Kijana akafika mbele ya Mfalme Kwa sababu Yeye alikuwa akimtegemea sana Mungu wa mbinguni, Mara moja akamwomba Mungu wake akamfunulia ndoto ile na tafsiri Yake.
Mfalme akampa zawadi zote ambazo alipanga kuwapa Waganga , wachawi na wasomi kama wangeweza kumwambia ndoto na tafsiri yake. Waganga wachawi na wasomi ambao walijiweka Mbelembele kwa Mfalme wakaaibika na hawakupata kitu kwa Mfalme.
> Hivyo ndivyo mambo yalivyo, Wapo watu ambao wanakukwepa kwa kuamini kuwa huna cha kuwasaidia, Usihangaike nao, maana kuna uwezekano kile wanachokimbilia muda ukifika wao wenyewe watakuita uende ukachukue maana Mungu amekiweka kwa ajili yako.
"USILAZIMISHE WATU WENGINE KUFAHAMU UMUHIMU WAKO SUBIRI MUDA UKIFIKA WATAKUTAFUTA".