JE UNAIFAHAMU NJIA YA MAFANIKIO YAKO?
Mimi Ni mwalimu kwa Taaluma, Nimekuwa nikishughulika na watoto kwa miaka kadhaa Sasa, Jambo ambalo nimekuja kugundua Ni kwamba wengi wa watoto hawajui Njia ya mafanikio yao. Na hii imetokana na malezi kutoka kwa wazazi na watu wa karibu pamoja na mfumo wa Elimu ambao haumfunyi mtoto kutambua njia itakayompatia mafanikio.
Malezi pamoja na mfumo wa Elimu unatufundisha kuona vitu katika mtazamo ambao kila mtu anaviona na pale unapofikiri na kufanya tofauti na wengine wanavyoona Hilo linahesabika kuwa Ni kosa.
Nimejifunza pia kuwa kila mtu anazaliwa na uwezo wa kipekee ambao mtu mwingine yoyote hana. Unakuta mwanafunzi ana uwezo mkubwa wa kucheza mpira, au kuchora, au kutunga hadithi na kadhaliko kuliko wanafunzi wengine wote darasani. Kinachoumiza Zaidi Ni kwamba unapojaribu kumsaidia kutambua kitu ambacho kinaonekana kitampa mafanikio Zaidi atakwambia "Baba yangu ameniambia niwe mtu Fulani" kitu ambacho unaona kabisa Hana uwezo nacho au atatumia nguvu nyingi sana na muda mwingi kufanikiwa.
Ndiyo maana unaweza kuta mtu amesomea kitu Fulani, lakini hafurahii kufanya Kile alichokisomea. Mwisho wa siku anaamua kuacha alichokisomea, anaamua kwenda kufanya kitu kingine ambacho hajakisomea Ila anachokipenda, au anaamua kwenda kusomea kitu kingine nachokipenda ili afanye kazi anayoipenda itakayompatia mafanikio makubwa kwa haraka Zaidi.
Hivyo Basi ili ufanikiwe kwa haraka na kufurahia mafanikio yako unatakiwa kugundua mapema kitu Cha pekee kilichopo ndani yako, La sivyo itakulazimu kufanya kitu usichokipenda maisha yako yote ili mradi tu upate kipato au kurudi nyuma kutafuta Kile kitakachokupa furaha na mafanikio Zaidi.
Kama haujui unakoenda maana yake hauende popote, maana unaweza ukuta unazunguka tu na kurudi ulipokuwa.
Mwanahabari, mwandishi na Lecturer maarufu nchini marekani Samwel L. Clemens ambaye pia alijulikana Kama mark Twain aliwahi kusema
"The two most important days in your life are the day you are born and the day you find out why." – Mark Twain
Akimaanisha "Siku mbili muhimu Zaidi katika maisha yako Ni siku uliyozaliwa na siku uliyogundua kwa Nini ulizaliwa"
Bila shaka Kuna wakati Fulani katika maisha ulikuwa na ndoto za kuwa na mafanikio makubwa Sana ndani ya muda mfupi. Ulianza kupiga hatua kuelekea mafanikio lakini Cha ajabu mpaka Sasa Bado upo palepale, huna chochote Cha maana ambacho umefanya. Huwa unajilaumu Bila kujua Kile ambacho kinatafuna mafanikio yako Ni kipi. Pengine ulifuanikiwa lakini haufurahii kile unachokifanya.
SASA UNAPASWA KUFANYA NINI?
Mafanikio makubwa pamoja na furaha ya maisha kutoka ndani ya moyo Ni muunganiko wa vitu vitatu: Kile unachokipenda, Jumlisha Kile unachokiweza na Kile unacholipwa vizuri kwacho.
Tofauti na hapo hautaweza kufurahia mafanikio katika maisha yako yote.
Watu wengi duniani tumejikuta tukiteseka Sana kufikia Mafanikio kwa sababu hatujui njia itakayotufikisha kwenye mafanikio. Ukiifahamu njia itakuwa Ni Rahisi Sana kufika uendako.
P.S Njia haimtafuti mtu Bali mtu ndiye hutafuta njia. Kaa chini tafakari kujua kile anachokipenda na uwezo ulionao katika kufikia hayo Malengo yako. Wewe ndiyo unajijua Zaidi ya mtu yoyote.
Kuna maeneo ambayo utapambana Sana lakini hautafanikiwa na wakati mwingine utaonekana wewe hujui lolote, na Wala si lolote, Lakini tatizo Ni kwamba haujajua tu Ugenius wako upo sehemu gani. Wengi imefikia hatua wakaaminishwa na wakaamini kuwa wao na hata familia yao siyo watu wa kufanikiwa, wamekatishwa tamaa na kuamuamini hawawezi kabisa.
Mwanasayansi maarufu duniani Albert Einstein aliwahi kusema kuwa “Kila mtu ni Genius Lakini kama utamhukumu samaki kwa kushindwa kupanda juu ya mti, basi samaki ataishi Maisha yake yote akiamini kwamba hana akili”
(Everyone is a genius but if you judge a fish by its ability to climb a tree, it will live its whole life believing that it is stupid).
Chagua uwanja wako wa mapambano kwa busara.
Joybell C alisema "Chagua mapambano yako kwa Busara, Hata Hivyo maisha hayapimwi kwa kuangalia Mara ngapi ulisimama ili kupambana, Siyo kushinda mapambano kunakokufanya ufurahi, Bali Ni Mara ngapi uligeuka kutazama uelekeo Bora Zaidi. Maisha Ni mafupi Sana kuyatumia kupigana Vita. Pambana mapambano mbayo Ni ya muhimu Sasa, na mengine acha yaende".
Choose your battles wisely. After all, life isn't measured by how many times you stood up to fight. It's not winning battles that makes you happy, but it's how many times you turned away and chose to look into a better direction. Life is too short to spend it on warring. Fight only the most, most, most important ones, let the rest go. ― C. JoyBell C.
Kuchagua uwanja wako wa Vita, Aina ya Vita na Namna ya kupigana kwa Busara kutakufanya uwe mpambanaji Bora na Hivyo kufikia Mafanikio yako kwa haraka Sana.
Sikia! Simba na mamba wakipambana nchi kavu, Bila shaka Simba atashinda. Lakini mamba yuleyule na Simba yule yule wakipambana majini Bila shaka mamba atashinda. Hii inaonesha kwamba kila mmoja Ni Bora katika uwanja wake.
Usimsikilize kila mtu anayekuambia kuwa huwezi kufanya kitu Fulani kwa sababu uwanja wake na wako Ni tofauti. Namna anavyoona yeye siyo sawa na wewe uonavyo. Jipime wewe mwenyewe Kwanza na Kisha uamue.
Usipoteze muda kufanya kila kitu, Bali tumia muda wako kuchagua na kufanya vitu ambavyo Ni vya muhimu tu katika safari yako. "Hauwezi kufika uendako haraka kama utasimama kila Mara na kuanza kumrushia mawe kila mbwa anayekubwekea njiani"
Watu wengi huwa wakiniomba ushauri kwamba "Nifanye biashara gani au Nifanye Nini ili niweze kufanikiwa? Huwa nawauliza maswali manne muhimu
Swali la Kwanza: Unafikiri Unapenda ufanya Nini? Au kitu gani ukifanya unakuwa huru Zaidi? Au unafikiri una kitu gani Cha kipekee ndani yako?
Swala la pili: Je unao uwezo wa kufanya kwa ufanisi kiasi gani kile ambacho unakipenda?
Swali la tatu: Je unayo maarifa au ujuzi wa kufanya kile ambacho unatamani kukifanya?
Swali la nne: Mazingira yanayokuzunguka yanasupport kufanya hicho kitu? Au utatafuta mazingira yanayoendana na hicho kitu.
Akifanikiwa kuyajibu maswali hayo kwa usahihi pasipo kujipendelea atakuwa ametambua Ni kitu gani atakachofanya kitaweza kumpatia mafanikio makubwa na ya haraka.
Hata wewe Kama unahitaji kufikia Mafanikio makubwa kwa haraka, jiulize maswali hayo kwa uaminifu na majibu yatoke ndani ya moyo wako. Majibu yako ndiyo yatakuonesha njia ya mafanikio yako.
_____________________________________________________________________
Kwa maoni na ushauli piga simu/WhatsApp number +255786216172
Ni Mimi mdau wa mafanikio yako
Lucas Robert

