Ticker

6/recent/ticker-posts

NAMNA YA KUONGEZA THAMANI YA KILE UNACHOKITHAMINI

 HAKUNA ATAKAYETHAMINI KILE UNACHOKITHAMINI MPAKA UONESHE THAMANI YAKE.



Kipindi nasoma sekondari Kuna jamaa mmoja alishona mfuko wa daftari kwa kutumia kitambaa Fulani Cha kutengenezea Sofa . Kitambaa Kile kilikuwa na mwonekano mbaya, kila mtu aliyekuwa akiutazama ule mfuko alikuwa anacheka sanaa. Tulikuwa tukimuuliza mbona umeamua kushona mkoba wa kubebea daftari wa kutumia kitambaa kibaya hivyo?. Jamaa kwa Ujasiri alijibu mfuko Huu umeshonwa kwa kutumia mojawapo ya vitambaa vya gharama Sana vinavyotumika kutengeneza sofa. Yeye pekee ndiye aliyekuwa anajua thamani ya kitambaa kile.

Ukweli ndio huo kwamba "Siyo kila unachokiona wewe Ni Cha thamani Basi kila mtu atakithamini". Usikatishwe tamaa na wale ambao hawaoni thamani yako, thamani ya Kile unachokifanya, thamani ya huduma au bidhaa unayoiuza. Unachotakiwa Ni kuendelea kufanya thamani ya Kile unachoamini Ni Cha thamani ijulikane.

Kuna watu wanalipwa kidogo katika Kile wanachofanya kwa sababu Bado thamani ya Kile wanachokifanya haijajulikana. Thamani ya Kile unachokifanya unaijua wewe unachotakiwa Ni kuboresha na kupaza sauti Zaidi kuonesha uthamani wa Kile unachokithamini. 

Wapo watu ambao wanabidhaa au huduma Bora Sana na wanajua thamani yake lakini kutokana na kukatishwa tamaa na watu wasio jua thamani yake wameishia kushusha thamani ya Kile walichokuwa wanakisamini.

Dunia tunayoishi inataka tuishi kwa kuamini Namna ambavyo wengine wanaamini, ukiamini tofauti na wengine wanavyoamini watakwambia haiwezekani. Dunia inatulazimisha tufanane na watu wengine kimtazamo na Namna ya kufikiri. Inatulazimisha kuona vitu Fulani tu ndiyo vina thamani kuliko vingine.

Hiki Ni mojawapo ya kizuizi kikubwa Sana Cha mafanikio.

"While children are struggling to be unique, the world around them is trying all means to make them look like everybody else."

- Dr. APJ Abdul Kalam

Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema "Wakati watoto wanapambana kuwa wa pekee, Dunia inayowazunguka inatumia Namna yoyote kuwafanya wawe Kama watu wengine". 


Sikia, uthamani wa kitu unategemea na uelewa wako. Ukichukua mfuko wa pesa na mfuko wa ndizi na kuweka mbele ya nyani nyani atachagua mfuko wa ndizi na kuacha mfuko wa pesa kwa sababu yeye anaona ndizi ina thamani kwako kuliko pesa, Wala hajui kwamba mifuko Zaidi ya elfu moja ya ndizi inaweza kununuliwa na pesa alizoziacha.

Hautafanikiwa mpaka uwe na uwezo wa kuona thamani katika Kile amacho wengine hawaoni thamani yake.

Dunia inataka wewe uwe sawa na wengine ili ikupe kile ambacho kila mtu anapata. Kama unataka kufanikiwa zaidi, lazima uende kinyume na dunia inavyotaka uwe, lazima uwe wewe na lazima utoe kile kilichopo ndani yako.


Namna ya Kuongeza thamani yako au Kile unachokifanya.


1.Jithamini wewe mwenyewe kwanza.



Ni ukweli kabisa, jinsi unavyojiona ndivyo ulivyo. Kama utajiona wewe Ni wa thamani kiasi gani pia hata wanaokuzunguka watakuona wewe Ni wa thamani. Kutambua thamani iliyo ndani yako itakusukuma kufanya Zaidi hata vile ambavyo inaonekana haiwezekani. Yai likipasuka kwa nguvu itokayo nje, uhai wa yai Hilo unakoma ila, Kama likipasuka kutokana na Nguvu kutoka ndani kifaranga hutoka na maisha yanaendelea. Mfano Huu unaonesha Namna ambavyo nguvu kutoka ndani maisha mapya yanaanza. Usijidharau maana hakuna ambaye atakuthamini Bila wewe Kwanza kuanza kukithamini. 


2.Tumia uwezo binafsi uliyoko ndani mwako.

Kila mtu amezaliwa na uwezo Fulani maalumu ambao mwingine Hana na Kama akiutumia huo uwezo Bila shaka utafanikiwa Sana na thamani yako itaongezeka. Kushindwa kufanya Jambo Fulani haina maana kwamba huwezi kufanya kila kitu, Kuna kitu Fulani ambacho wewe binafsi una uwezo wa kukifanya kwa ufanisi Zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Kwani hujawahi kuona mtu hata chuo hajafika lakini unasikia watu wanasema "kama ukitaka kitu chako kifanyike vizuri mtafute Fulani". Na watu wanatambua thamani yake kiasi kwamba akikosekana tu kila mtu anatambua kutokuwepo kwako.

 Mimi binafsi ilifika wakati nikaona kabisa Hakuna Cha maana ambacho naweza kufanya kwa ufanisi, lakini nilianza kutambua uwezo wangu wa kipekee baada ya kusoma kitabu Cha mwandishi maalufu Joel Arthur Nanauka kiitwacho CORE GENIUS, Napendekeza ukitafute ukisome.


3. Chagua watu wanaoendana na thamani yako.



Haijalishi wingi au uchache lakini watu wako wa karibu wana pima thamani yako.

“Show Me Your Friends and I’ll Show You Your Future” -  Dan Pena

Kwa tafsiri anamaanisha "Nioneshe marafiki zako nikuambie kesho yako"

Utafiti umeonesha kwamba kipato chako Ni wastani wa marafiki zako 10 wa karibu Sana ambao mnatumia muda mwingi pamoja. Hivyo Basi Ni muhimu kuchagua marafiki ambao watafanya thamani yako iongezeke. Epuka marafiki ambao wao wenyewe hawajithamini na ambao hawathamini wengine.

4.Epuka Tabia zinazoshusha thamani.

Tabia ndiyo humtambulisha mtu, Tabia yako ndilo jina lako. Kuna tabia ambazo ukiwa nazo tu kila mtu anakudharau, anakushusha thamani. Tabia yako inaathiri thamani yako na kila kitu unachokifanya. Hata katika Biashara Kuna baadhi ya tabia ulizonazo ambazo zinshusha thamani ya Biashara zako, kiasi kwamba ukimwambia mtu Bei ya bidhaa au huduma yako watakwambia una Bei kubwa, Na wakati huo huo wananunua bidhaa au huduma kibwa kwa gharama kubwa Zaidi hata ya kwako. Ukiona Hivyo tambua kuwa kuna tabia Fulani ulizonazo ambazo zinashusha thamani ya Biashara yako.

"Tembea katika tabia Zinazoendana na ndoto zako"

Ukitaka kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa Ni muhimu kuhakikisha unaongeza thamani yako kila siku. Kula kulingana na thamani yako, vaa kulingana na thamani yako, tembea na tembelea maeneo kulingana na thamani yako, zungumza kulingana na thamani yako. 

Wekeza juu yako mwenyewe (Invest in yourself). Nakuhakikishia baada ya muda mfupi tu utakuwa mtu wa thamani ya juu Sana. Hutakubali kulipwa kidogo Kama ilivyo Sasa, hutauza bidhaa zako au huduma kwa Bei ya kugalaliza Kama unavyofanya Sasa.

Wekeza katika afya bila kusahau kuongeza maarifa yako kila siku.

Kama unahitaji ujuzi wa ziada usisite kuwasiliana nami nitakuunganisha na watu waliobobea katika maswala mbalimbali ya yatakayokuletea mafanikio.

Pia kwa wale wanaohitaji kuboresha afya zao, mwonekano na kuwa na uhuru na Kujiamini katika maisha Usisite uwasiliana namili ili kupata ushauri BURE kuhusu changamoto mbalimbali za kiafya.

Unaweza kuwasiliana nami kwa kupiga simu /WhatsApp number +255764075392/786216172

Lucas Robert

"Live an inspired Life"