MPENZI WAKO ANASUBIRI
Biblia Takatifu katika kitabu cha wimbo Ulio bora 3:1-4
"1 Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate.
2 Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate.
3 Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
4 Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa.
Yesu ni Rafiki yetu mpendwa ambaye anatupenda upeo, Alitupenda upendo wa AGAPE hata tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Warumi 5:8
8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Mtunzi wa wimbo no 130 (YESU KWETU NI RAFIKI - what A friend we have in Jesus) Bw. Joseph Medlicott scriven Andaandika shairi kwenda kwa mama yake Mpenzi ambaye alikuwa ni mgonjwa sana huku yeye akishindwa kwenda kumuona kutokana na ukata wa kifedha, Anaandika ili kumfariji akisema
1. Yesu kwetu ni rafiki Hwambiwa haja pia,
Tukiomba kwa babaye, Maombi asikia
Lakini twajikosesha Twajitweka vibaya,
Kwamba tulimwomba Mungu Dua angesikia.
2. Una dhiki na maojo, Huwezi kwendelea,
Haifai kufa moyo, Dua atasikia,
Hakuna mwingine Mwema Wakutuhurumia,
Atujua tu dhaifu, Maombi asikia
3. Je hunayo hata nguvu Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa, Ujaparushwa pia,
Watu Wangekudharau, Wapendao Dunia hukwambata mikononi Dua Atasikia.
Ikumbukwe Kuwa ndugu Joseph aliwahi kupoteza mpenzi mara mbili karibia kabisa na siku ya Harusi yake.
Rafiki tuliye naye Anatuhurumia maana na yupo tayari kujibu Dua zetu muda wote na kutupatia kile ambacho ni hitaji la mioyo yetu kama tutamuomba maana hakuna mwingine anayeweza kufanya hivyo.
Tatizo tunajiweka katika nafasi au upande ambao unakuwa ni Ngumu kwetu kupata msaada wake.
Kama ilivyo kwa mashua zile zinazosukumwa na upepo zinaweza kuelekea kule upepo unakoenda kama tu itaamua kung'oa nanga.
Leo tunaweza kukubali kuongozwa naye, Tung'oe nanga na tufuate uelekeo anaotupeleka nasi tutapata Raha nafsini.
Mathayo 11:28
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Rafiki yetu kipenzi (Yesu) akiwa anasafiri na wanafunzi wake katikati ya Bahari Dhoruba kali ilitokea na yeye akiwa amelala usingizi juu ya mto.
Marko 4:35-39
35 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo.
36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.
37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.
38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
Rafiki yetu anaweza kutuliaza mahari na ataweza kutuliza kila kitu pia katika maisha yako.
Unaweza kudhani amelala lakini bado anasikia sema hetaji lako kwako naye atatenda.
Yeye anasubiri, Rafiki anasubiri uiwasilishe haja inayokusumbua kwake naye itaifanya kuwa yake na wewe utaondoka ukiwa huru na Amani kuu itatawala moyo wako.
Katika Mianzo ya mwako huu Piga hatua moja mbele uwasilishe Haja yako kwake uone maajabu atakayokutendea.
Anasikitika anapoona unahangaika huku msaada wako ukiwa karibu yako.
MPENZI WA NAFSI YAKO AMEAHIDI KUKUPUMZUSHA..🙏
Nakutakia *HERI NA BARAKA NA MAFANIKIO MAKUBWA MWAKA 2024*
Unaweza kushare kwa ndugu jamaa na marafiki baraka hizi za mwaka 2024
*Sharing is caring*
Unaweza ku- SUBSCRIBE you tube chanel yangu inayoitwa kwa kutafuta jina *Fanikiwa na afya yako*
Ahsante kwa kujali 🙏
Imeandaliwa na mwl Robert
