Ticker

6/recent/ticker-posts

NAMNA YA KUPUNGUZA UZITO NA KUZUIA KITAMBI AU UNENE KUPITA KIASI

CHANZO KITAMBI NA UNENE KUPITA KIASI NA NAMNA YA KUEPUKA.

Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyo hitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini. Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI).

Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako.
Kujua BMI yako chukua uzito katika kilograms (kg) gawanya kwa urefu Mara urefu katika mita (m2)
Utajuaje kama zito ulionao unafaa kulingana na urefu wako?
Kama BMI Ni chini ya 18 inamaanisha unauzito mdogo Sana, rekebisha mfumo wa ulaji wako ili uongeze uzito kidogo.
BMI kati ya 18.5 hadi 25.5 uzito uko sawa
BMI 26 hado 29.5 unaelekea Kuwa na uzito mkubwa chukua tahadhari.
BMI Zaidi ya 30 Uzito umezidi Sana, pambana Sana kuhakikisha unapunguza Uzito.



CHANZO CHA KITAMBI NA UNENE KUPITA KIASI (Obesity).
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na :

1. Vyakula vya mafuta - Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.

2. Kutofanya mazoezi - Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.

3. Kurithi viashiria vya asili (genes) - Viashiria hivi vinaweza kuwa moja ya vichocheo vya kuongeza uzito kwani ndivyo huamua namna mafuta yanavyotumika na kuhifadhiwa mwilini na kwa kiwango gani. Lakini haimanishi kuwa mtu akiwa navyo basi ndio atakumbwa na tatizo hili.

4. Umri - Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass).

5. Matatizo ya kisaikolojia - Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.

6. Dawa - Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.

7. Matatizo ya afya - Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa kama cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika

MADHARA YA UNENE KUPITILIZA
Unene kupita kiasi una madhara mengi Sana kiafya na Ni chanzo Cha magonjwa mengi sana



Miongoni mwa Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza Ni Kama fuatavyo:-
1. Kisukari

2. Shinikizo la damu (hypertension)

3. Kiharusi (Stroke)

4. Magonjwa ya moyo

5. Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)

6. Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)

7. Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu (cholesterol ikiwemo triglycerides)

8. Ugonjwa wa mifupa kama baridi yabisi (osteoarthritis).

9. Saratani ya matiti

10. Saratani ya tezi dume (prostate cancer)

11. Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer).

12.Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni (varicose veins).

13.Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza ( obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo;

✓Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) - kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
✓Shinikizo la damu (hypertension)
✓Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
✓ Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
✓ Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress)


Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi
✓Siri ya kupunguza Uzito na kuzuia Uzito wa mwili Kuongezeka ipo katika mambo mawili tu:

1.Kuzuia mafuta na sukari kuingia na kurundikana mwilini.

2.Kutumia kiasi Cha mafuta na sukari mwilini kwa ufanisi.
Mafuta na sukari ndivyo vyanzo na visababishi vikuu vya Uzito wa mwili kuongezeka.
P.S: Wengi wanasumbuka Sana kupunguza Uzito hii Ni kutokana na kukosa uelewa kuhusu chanzo Cha Uzito kupitiliza. Leo nataka nikwambie, Kitu hatari Zaidi na kinachoongeza Uzito na unene kupita kiasi kwa haraka Zaidi Ni Sukari na siyo mafuta. Hii itakuchanganaya lakini ndiyo ukweli wenyewe.

Elewa mambo haya mawili kuhusu sukari.
 ∆Sukari inafyonzwa kirahisi Sana kuingia mwilini kuliko Aina zingine za vyakula. 
∆Sukari inaweza kubadilishwa kuwa mafuta kwa urahisi kuliko chakula chochote.
Unapokuwa umekula wanga tambua kabisa hapa umekula chanzo Cha mafuta.
Mfano: Asubuhi umeamka ukala chapati (wanga) ambao usipotumika hubadilishwa kuwa mafuta na kutunzwa mwilini, chapati ambazo zimekaangwa kwa mafuta, nayo yasipotumika yanatunzwa mwilini, Umekunywa na chai Kama Ni ya maziwa ndani yake Kuna mafuta ndani yake, Kama Ni ya rangi ndani yake Kuna sukari ambayo pia isipotumika itatinzwa mwilini Kama mafuta. Kwa ufupi umekula mafuta+ mafuta+ mafuta = Uzito kupita kiasi. 

KUMBUKA: Kama wanga (sukari) na mafuta ndivyo vinavyounda miro yako ya kila siku Basi unapaswa kuushughulisha mwili ili uhakikishe kiasi hicho kinatumika chote mwilini na kwa wakati.

Hivyo Basi Kama utazingatia uwiano sahihi wa chakula unachokula kulingana na mahitaji ya mwili wako, swala la kupungua Uzito wa mwili au kuzuia Uzito wa mwili kuongezeka litakuwa Ni Jambo linalowezekana.

 ✓Mabadiliko ya tabia ya mhusika pia Ni njia nyingine muhimu sana itakayosaudia kuthibiti Uzito wa mwili. Mabadiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku. Mabadiliko haya yanahusisha mazoezi, chakula na madiliko ya tabia ya mtu.

✓Unaweza pia kupunguza uzito wako kwa kutumia chakula lishe kilichoandaliwa Kitaalamu na kisicho na madhara yoyote kiafya. 
Tiba lishe hiyo inakuwezesha kupungua kwa kuendana na matakwa yako na ni nzuri sana kwa wale ambao hawana muda wa kutumia njia ngumu kwa ajili ya kuupunguza mwili au wale waliokwisha kufanya hivyo ila kutokana na uvivu wakashindwa.
Kwa sababu chakula lishe hiki kinahitaji utaalamu na teknolojia ya Hali ya juu katika kukiandaa Mara nyingi inakuwa siyo rahisi kukipata. Hata Hivyo kuna kampuni kadhaa ambazo mpaka Sasa zinazalisha na kusambaza bidhaa hii katika ubora unaohitajika. 

Mimi Ni miongoni mwa wale ambao walikuwa na Uzito mkubwa Sana lakini baada ya kutumia chakula lishe hiki matokeo yake yalinishangaza na mpaka Sasa nafurahia maisha. 
Ninaweza kukusaidia kupata mojawapo ya bidhaa hii ambayo itakusaidia kupunguza Uzito au kuthibiti Uzito wako kuongezeka kwa haraka ndani ya siku 30 tu pasipo kupata madhara yoyote kiafya.
Cha kufanya wasiliana nami kwa simu/WhatsApp number +255786216172.

Unaweza kuendelea kupata Elimu kuhusu maswala mbalimbali kwa ku-follow ukurasa wetu wa Facebook : Fanikiwa_na_Afayako  Na Instagram: fanikiwa_na_afyayako 

"Live an inspired life"