Ticker

6/recent/ticker-posts

FAIDA ZA MAJI MWILINI

 FAIDA ZA KUNYWA MAJI KWA UTARATIBU MZURI..




Unywaji wa maji una faida nyingi sana katika mwili wa binadamu. Maji yana kazi nyingi sana za muhimu kwa ajili ya ufanisi wa ufanyaji kazi wa mwili ili kuboresha afya ya mwili.

Walio wengi hunywa maji pale tu wanaposikia kiu ya maji, wengine wasiposikia kiu ya maji ana uwezo wa kukaa hata siku kadhaa pasipo kunywa maji hasa katika majira ya baridi. 

Kwa watu walio wengi unywaji wa maji kwao siyo kipaumbele kabisa. Jambo ambalo linahatarisha sana afya ya mwili. Hata hivyo hakuna kiwango maalumu cha matumizi ya maji kinachokubalika kila mahali. 

 Lakini ni muhimu kuzingatia kunywa maji mengi kwa wakati unaofaa kulingana na mahitaji ya mwili wako.

KUMBUKA: Zaidi ya asilimia 60 ya mwili wa binadamu ni maji. 


UMUHIMU WA MAJI MWILINI.

Zifuatazo ni sababu muhimu kwa nini unatakiwa kutumia maji kwa kiwango kinachotakiwa na kwa usahihi kila siku:

1. Kulainisha viungo (Lubricating the joints)

Katika viungo kuba mifupa laini inayozui msuguano ijulikanayo kama cartilage ambayo ina hadi 80% maji. Hivyo kukosekama kwa maji mwilini huweza kupelekea kuongeza kwa msuguano kwenye viungo na kusababisha maumivu ya viungo.


2. Hulinda Ubongo, uti wa mgongo na na sehemu zingine muhimu mwilini.

Viungo muhimu kama ubongo na uti wa mgongo vinazungukwa na vimiminika (maji) ili kulinda kuwezesha kufanya kazi yake pasipo bughudha kutoka nje. Upungufu wa maji wa muda mrefu kwenye ubongo huweza kupelekea kupungua kwa kumbukumbu na hatimaye kuharibu ubongo kabisa.

3. Kurekebisha Joto la mwili (Regulates body temperature)

Joto la mwili wakati mwingine huongezeka kulingana na shughuli zinazoendelea mwilini (matabolism) au kutokana na hali ya hewa. Jambo ambalo hupelekea maji yaliyondani ya mwili kutumika kupoza mwili na kisha kuondoka kwa mfumo wa jasho (mvuke). Kukosekana kwa maji mwilini hufanya mwili kuumia wakati wa joto.


4. Kusaidia chakula kumeng'enywa

Tumbo linahitaji maji ili kukichanganya chakula na vimeng'enya vizuri ili kimeng'enywe kifae kwa ajili ya kifyonzwa mwilini. Kukosekana kwa maji huweza kupelekea choo kigumu (constipation), na kuongezeka kwa acid mwilini. Hii huongeza uwezekano wa kiungulia na ugonjwa wa vidonda vya Tumbo (Ulcers)


5. Kusafisha mwili au Kuondoa taka mwili (waste products).

Maji ni muhimu sana katika michakato ya utoaji taka mwili kama vile Kutokwa jasho na Kukojoa. Maji yanapokuwepo kwa wingi hufagia taka mwili zote hivyo kupunguza mrundikano wa sumu mwilini ambao huweza kusababisha kichwa kuuma mara kwa mara, uchovu kupita kiasi na magonjwa mengine mengi.

6. Huzuia shinikizo la damu (Blood pressure).

Ukosefu wa maji mwilini husababisha mishipa ya damu kunenepa hivyo kupunguza kipenyo kinachotakiwa kwa ajili ya kusafirisha damu hivyo kupelekea shinikizo la damu.


7. Huboresha Afya ya Ngozi na kuongeza Urembo.

Kunywa maji ya kutosha hufanya ngozi iwe laini inayong'aa na yenye mvuto zaidi. Kwani husaidia katika kurekebisha sehemu zilizojeruhika na utengenezaji wa seli mpya.

Mwili unapokosa maji ya kutosha hufanya ngozi kuwa hatarini kupata magonjwa na kufanya uwe na muonekano wa uzee kabla ya wakati wake.


8. Hulinda Figo.

Figo ni mojawapo ya viungo muhimu sana katika mwili. Figo hurekebisha kiwango cha maji na vimiminika vingine ndani ya mwili pamoja na kuondoa taka mwili. Kukosekana kwa maji ya kutosha ndani ya mwili hupunguza ufanisi wa figo na mwisho kushindwa kabisa kufanya kazi kabisa (kidney failure) jambo ambalo linaweza kupelekea kifo.


9. Huongeza ufanisi wa tendo la ndoa.

Ufanisi katika tendo la ndoa hasa kwa wanaume huhusisha mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu inahitaji kuwa na kiwango sahihi cha maji ili iweze kuzunguka vyema mwilini ili kuchukua oxygen na sukari (glucose)  kwa ajili ya kuzalisha nishati au nguvu inayohitajika katika tendo la ndoa. Hivyo kushindwa kutumia maji katika kiwango sahihi hupunguza ufanisi katika tendo la ndoa na hivyo mwanaume husemekana kupungukiwa nguvu za kiume.


10. Husaidia kupunguza uzito.

Maji husaidia kupunguza uzito au unene kupitiliza kama yatatumika badala ya vinywaji vyenye sukari nyingi kama sukari za viwandani na soda. Kunywa maji kabla ya mlo pia huweza kusaidia kupunguza kula kupitiliza kwani hufanya ujisikie kushiba haraka.



NYAKATI NNE MUHIMU ZA KUNYWA MAJI

1) Baada ya kuamka.



Kunywa glasi moja ya maji baada ya kuamka husaidia kuamsha viungo vya mwili na kuondoa sumu kabla hujala chochote.


2) Kabla ya chakula



Kunywa glasi moja ya maji dakika 30 kabla ya mlo husaidia mmeng'enyo wa chakula. Kumbuka usinywe maji muda mfupi sana kabla na baada ya chakula kwa sababu maji hupunguza kiwango cha vimeng'enya (Dilute enzymes).

Hivyo ni vyema kunwa maji nusu saa au saa 1 baada ya kula ili kusaidia virutubisho kufyonzwa ndani ya mwili.


3) Kabla ya Kuoga.



Kunywa glasi moja ya mwili kabla ya kuoga kusaidia kushusha shinikizo la damu (blood pressure).


4) Kabla ya kulala



Kunywa glasi moja ya maji kabla ya kulala kufidia upotevu wa maji unaoweza kutokea wakati umelala.


P.S: Kuna baadhi ya watu wanaokunywa maji mengi kila siku lakini bado wanasumbuliwa na matatizo yanayoashiria upungufu wa maji. Sababu mojawapo inaweza kuwa ni kushindwa kutumia maji kwa wakati sahihi hivyo maji mengi hutoka nje ya mwili kabla ya kufanya kazi iliyokusudiwa.

Kunywa maji mengi katika utaratibu unaofaa inakusaidia kupunguza uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa nyemelezi mara kwa mara na kuboresha utendaji kazi wa mwili wako kwa ujumla.

Niandikie umejifunza nini kuhusu matumizi ya maji?

Nini mpango wako sasa kuhusu matumizi ya maji?


Imeandaliwa na Lucas Robert


"Live an inspired life"