FAIDA 10
ZA KITUNGUU MAJI(ONION)
Kitunguu kina madini mengi Kama vile sulfur, zinc, na Iron, ambayo ni muhimi mwilini. Kitunguu kina faida nyingi kiafya ikiwa maandalizi yake yatafanyika vizuri bila kuharibu virutubisho vilivyopo kwenye kitunguu.
FAIDA NA MATUMIZI YA KITUNGUU.
zifuatazo ni baadhi tu ya faida ya kutumia kitunguu japokuwa zipo nyingi Sana zaidi ya hizi nitakazoeleza hapa:
1. Kutibu ama huzuia maumivu yatokanayo na kuumwa na Nyuki, Nyigu, Nge na wadudu wengine wenye sumu.
Namna ya kutumia :pakaa juisi yake au maji maji yake katika sehemu ambayo mdudu amekuuma. Baada ya muda mfupi tu maumivu yataisha kabisa, Pia huvuia kuvimba baada ya kung'atwa na mdudu.
2.Maumivu ya sikio.
Namna ya Katibu sikio linalouma : Chemsha kitunguu kwenye maji au jiko la kuokea (Oven), Baada ya hapo funga kwenye kitambaa safi na uweke kwenye sikio linalouma.
3.Husaidia kushusha au kupunguza kiwango cha sukari mwilini. Kitunguu kina chemikali iitwayo Allyl propyl disulphide (APDS) Ambayo hufanya kazi pamoja na insulini ili kubadili sukari kuwa gulukagoni hivyo kupunguza kiwango cha sukari mwilini.
Namna ya kutumia : Unaweza kutafuna kitunguu chenye rangi nyeupe kila siku asubuhi.
4.Husaidia Mfumo wa mzunguko wa damu. Chemikali zilizopo kwenye kitunguu huzui kuganda kwa damu. Pia sulfur iliyopo kwenye kitunguu huongeza seli za damu.
5. Huondoa sumu mwilini.
Kitunguu kina Methionine na cystine ambazo huondoa heavy metals Kama vile mercury (Hg), Lead (Pb), Cadmium (Cd). Vitamini C kwenye kitunguu pia hufanya kazi ya kuondoa sumu. Vitamini zote huwa zina uwezo Wa kuwa katika hali ya mvuke kirahisi. Kwa hiyo hakikisha vitunguu vyako havipigwi na jua au joto Kali.
6. Husaidia Afya ya kinywa.
Tafuna vitunguu vibichi ambapo huua vimelea vya magonjwa ya meno kuzuia meno kuoza.
7. Afya ya Ngozi na nywele.
Osha nywele kwa juisi ya kitunguu husaidia nywele zisikatike. Sulfur iliyopo kwenye kitunguu hupambana na vimelea vya magonjwa yakiwemo magonjwa ya ngozi.
8. Husaidia kuimarisha mifupa na kuzuia upotevu au uwazi kwenye mifupa ( Osteoporosis).
9. Hupambana na kansa. Kutokana na uwezo wa kitunguu kuondoa sumu na kuzuia seli zisizo rasmi kuzalishwa mwilini ambazo ndio chanzo cha cancer.
10. Husaidia mmeng'enyo wa chakula. Vitunguu ambavyo havijaungua husaidia mmeng'enyo wa chakula kufanyika kwa ufanisi.
Hizo ndizo faida za vitunguu kwa afya ya binadamu. Kitunguu ni kiungo muhimu Sana kwenye chakula lakini hakikisha hauviunguzi maana ukiviunguza unakuwa umetengeneza sumu.
Imeandaliwa na Mwalimu, Robert Lucas
+255764075392
+255713053903
lucastrngwakwa@gmail.com
