Ticker

6/recent/ticker-posts

NGUVU YA UCHAGUZI MAISHANI.
Uchaguzi ni uamuzi wa kuchukua kitu kimoja (alternative) Kati ya vita ulivyo navyo. Uchaguzi ndiyo huamua hatima ya Mtu. Ukichukua uchaguzi sahihi utafanya vitu sahihi na utafika mahali sahihi. Kiukweli hivi nilivyo au hivyo ulivyo ni kutokana na uchaguzi uliofanya kipindi fulani cha nyuma, kama unafanya kazi fulani ni matokeo ya uamzi fulani ambao wewe au Mtu fulani alifanya ndiyo maana upo hapo ulipo. Hivyo basi, kwa sababu uchaguzi wetu ndiyo kitu kinachoamua hatima ya maisha yetu hatuna budi kukiangalia kwa jicho la tatu.
Hebu tuangalie namna ambavyo uchaguzi unaamua hatima yako katika mambo yafuatayo:
1. Muda (Time).
Muda ni kitu ambacho ukikosea kuchagua matumizi yake hutaweza kuyabadili matokeo yake. Fanya chaguzi wenye manufaa kwenye namna unavyotumia muda wako, Mtaalamu wa science ya maendeleo Mr. Brian Tracy alisema kuwa "Hauwezi kuupoteza muda bali unaweza kuutumi muda tofauti". Muda wa muhimu ni huu ulionao sasa ukishapita huo sio muda tena, ni vyema ukaangalia kile ambacho unakifanya saizi ndicho kinachotakiwa kufanya kwa muda huu? Sitakufundisha namna ya kuchagua muda kwa sababu kila Mtu ana umbali wake tofauti wa kukimbia ili aweze kufikia malengo yake. Chagua muda wa kulala, chagua muda wa  kusoma, chagua muda wa kupalilia ndoto. Nafikiri hata unapokuwa kuwa umechagua kutumia muda wako kusoma maandishi haya umefanya uchaguzi ulio sahihi kabisa nami nakukaribisha uendelee na uchaguzi wako tunapoendelea kuangalia namna ya kuchagua.

2. Fursa (Opportunity).
Fursa ni kitu kinachokuja maishani Mara chache (Nadra), Na kinapotokea unatakiwa kufanya uchaguzi ulio sahihi ili uweze kuondokana na hali uliyonayo. Tofauti zetu za kiuchumi zilizopo ni kutokana na uchaguzi wetu tunaofanya pindi fursa zinapotokea. Sio kila fursa inayotokea katika maisha yako ni sahihi kwako, ila kila fursa ipo sahihi na ni kwa ajili ya Mtu. Jiangalie wewe ulivyo na ujipime kulingana na fursa hiyo Kama inakufaa au la! Fikria kwa haraka na uchukue uamzi kwa haraka kama ni kuendelea na fursa hiyo au kutafuta fursa nyingine. Mara nyingi Fursa huwa hazitufuati na tunapozifuata tunakutana nazo nyingi tu na hapa ndipo tunatakiwa kufanya uchaguzi. Fursa zipo nyingi uchaguzi ni wako, lakini usichelewe kuchagua.

3. Marafiki.
Marafiki wana mchango mkubwa Sana katika kufanikiwa kwako au kutokufanikiwa kwako. Marafiki uliowachagua watakusaidia kutimiza malengo yako upo msemo usemao "If you want to walk faster walk alone, but if you want to walk longer walk with friends" Kwa hiyo marafiki ni muhimu Sana Katika safari yako ndefu ya mafanikio, lakini chagua marafiki kwa makini. Hapa nitasema nitatoa ushairi juu ya marafiki wapi wa kuchagua na wapi uachane nao.
....Usichague marafiki ambao wameshakata Tamaa kwa sababu hao watakukatisha tamaa tu, bali chagua marafiki ambao siku zote ndoto zao ni kufanikiwa hata kama hawajafanikiwa kwa sasa maana hao siku zote watakutia moyo na kukupa tumaini la kusonga mbele.
.... Usichague marafiki ambao ni waoga, waoga wa kujaribu, waoga wa kushindwa hao watakufanya uwe muoga na uogope kushindwa ili hali kushindwa ni hatua moja wapo kuelekea mafanikio.
.... Chagua marafiki ambao wana nidhamu, Nidhamu ya muda, Nidhamu ya matumizi ya pesa hao hawatakuweka katika vishawishi vya kutumia pesa zako au muda wako vibaya.
Naam, hiyo ni mifano tu ya marafiki unaoweza kuchagua lakini kwa ujumla, Chagua marafiki ambao wana malengo ya kufika unakotaka kwenda pia bila shaka hao mtatembea wote kwa pamoja huku mkitiana moyo kusonga mbele zaidi.

4. Chagua maisha.
Baada ya kujifunza kuchagua muda, kuchagua fursa, kuchagua marafiki, Ni lazima sasa uchague maisha unayotaka kuishi. Chagua maisha yanayoendana na wewe, usichagua maisha ya Mtu mwingine. Wapo watu wanaochagua maisha ambayo hawawndani nayo kabisa Mtu anafanya kazi ya kutumia akili lakini unakuta mtu huyo anachagua maisha ya kushinda njaa bila kula, Rafiki hayo maisha hayaendani na wewe hutafika mbali utachoka mapema. Wapo pia ambao wanachagua maisha ya kutumia pesa zao kwa anasa au kufanya mambo ambayo sio ya msingi hao nao uchaguzi wao sio sahihi ikiwa Bado wanatumikia pesa na pesa haziwatumikii wao.
Hakuna Mtu aliyefanikiwa bila kuchagua maisha sahihi anayoendana nayo. Chagua maisha yanayokupatia afya na nguvu ya kusonga mbele.

Wanasema kupanga ni kuchagua. Chagua kufanikiwa nawe utafanikiwa. "Uchaguzi ni wako, fanya uchaguzi wala usichelewe"
Usipochagua mwenyewe kuna mtu atakuchagulia muda wako, kazi yako, marafiki zako na atakuchagulia maisha ya kuishi pia.

Imeandaliwa na Mwl. Robert Lucas
  +255764075392
    +255713056903
    Email : lucastrngwakwa@gmail.com

Motto: Internal power can change the world.