Ticker

6/recent/ticker-posts

KILIMO CHA TIKITI MAJI.
Tikiti maji ni tunda au mboga ambazo zimekuwa na umuhimu mkubwa katika katika ulimwengu wa sasa hii ni kutokana na faida za kiafya ambazo hutokana na kuwepo kwa virutubisho vingi katika tunda hili.
Tikiti maji lina umuhimu kuanzia majani mpaka tunda lake. Kutokana na uhitaji mkubwa wa tikiti maji katika soko la nje na ndani kuna umuhimu mkubwa wa kulima zao hili kwa wingi ili kutosheleza mahitaji ya jamii. Hivyo kutokana na soko lake kuwa kubwa unaweza kukusanya pesa nyingi kwa muda mfupi kupitia kilimo hiki cha tikiti maji.
MAHITAJI MUHIMU KWA KILIMO CHA TIKITI MAJI.
HALI YA HEWA; Hali ya hewa kwa kilimo cha tikiti maji ni ,jotoridi la nyuzi za sentigredi kati ya 22 na 30.
                            Mvua ya kiwango kati ya milimita 400 hadi 600. Kipindi kizuri kwa ajili ya kilimo cha tikiti
                           Maji ni kuanzia mwenzi wa tatu (march) hadi wa tisa (September).
UDONGO; Tikiti maji husitawi vizuri katika udongo wa kichanga ulio changanyikana na tifutifu. Maeneo mazuri kwa kilimo cha tikiti maji maeneo Dar es salaam, Kahama –Shinyanga, Geita , mkoa wa Pwani na baadhi ya maeneo katika mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro.
VIPIMO KATIKA UPANDAJI; Umbali kati ya shina na shina na kati ya msitari na msitari hutegemea aina ya mbegu n hli ya udongo. Kwa mfano; tikiti maji aina ya sugarbaby kwenye udongo wenye rutuba hupandwa kwa vipimo vya, mita 1 shina hadi shina, na mita 2 au tatu msitari hadi msitari.
MUDA HADI KUKOMAA; Tikiti maji huchukua kuanzia siku 75 hadi miezi minne kukomaa kutegemea na ain ya mbeguhusika.
GHARAMA ZA UENDESHAJI WA KILIMO CHA TIKITI MAJI.
1.Kukodi shamba, Tshs.60,000/= hadi Tshs 100,000/= kutegemea na maeneo shamba linakopatikana.
2.kulimiwa shamba, Trekta Tshs 50,000/=, ng’ombe TShs 35,000/= au jembe la mikono kulingana na maelewano na mhusika.
3.kununua mbegu, kilo moja ya mbegu aina ya sugar baby ni Tshs.50,000/= kwa ekari moja unahitaji kununua kilo tatu ambazo ni sawa na gharama ya Tshs.150,000/=
4.Dawa za kupulizia wadudu, hizi hutegemea na hali ya hewa ya eneo na wakati, kwa maeneo yenye wadudu wengi na ukungu mwingi unaweza unaweza kupuliza dawa z kuulia wadudu kila wiki na dwa za ukungu kutegemea na hali ya hewa ambapo kwa wiki unaweza kutumia dawa za Tshs 10,000/= Hivyo ukipuliza mara nane gharama yake itakuwa ni Tshs 80,000/=.
5.Kama kilimo ni cha umwagiliaji unaweza kumwagilia mara mbili au mara tatu kwa wiki ambapo kila mar utatumia litre 5 kwa gharama ya Tshs 10,000/= kwa miezi miwli na nusu utaweza kuwagili mara 20, kwa hiyo gharama za umwagiliaji ni Tshs. 200,000/=
6.Mbolea; ukinunua aina tatu za mbolea kwa gharama ya Tshs 30,000/= @= Tshs90,000/=
7.Gharama za mlinzi na usafiri, tunaweza kukadiria kutumi Tshs 200,000/= kutegemea na umbali wa soko na kwa wakati mwingine gharama hizi zinaweza zisitumike kabisa.
.*.Jumla ya gharama zote za uendeshaji ni Tshs 850,000/= kwa uangalizi mkubwa wenye kutoa mazao makubwa na bora kabisa. Hizi gharama zinaonekana kuwa kubwa kwa sababu kila kitu nilikuwa naagiza tu bila kushughulika mwenyewe, ndugu jamaa na marafiki, nikishiriki ni lazima zitapungua tu.
      NAMNA YA KUENDESHA KILIMO HIKI.
1.Lima shamba vizuri, Ondoa nyasi na takataka zingine shambani.
2.Tengenez matuta yenye ukubwa wa kawaida kama ni kipindi cha mvua, Kama unategemea umwagiliaji tengeneza majaruba kwa ajili ya kukinga maji wakati wa umwagiliaji.
3.Chimba mashimo kwenye majaruba au matuta yako ukizingatia vipimo kama ilivyoelekezwa hapo juu, (45 cm -1m shina hadi shina Na 2-3m msitari hadi msitari).
4.Weka mbolea ya kupandia aina ya DAP au SAMADI kama inapatikana na baada ya hapo panda mbegu zako kwenye mashimo hayo yenye mbolea tayari (Weka mbegu tatu au mbili kila shimo).
          Aina za mbegu za tikiti maji ambazo ni nzuri:-
                 (i)Sukari F1 (sugarbaby)
                (ii)Mshidi
                 (iii)JULIANA ETC.
               .Aina zote hizi za mbegu huchukua miezi mitatu.
5.Wiki ya pili au ya tatu baada ya mbegu kuota weka mbolea ya kukuzia aina ya CAN au UREA.
6.Pulizia dawa ya wadudu kila unapoona wana tembea kwenye majani, hivyo uwe na tbia ya kuchunguza mimea yako kwa makini. Pia puliza dawa ya ukungu kila unapoona kuna dalili ya ukungu angani, usisubiri majani yaanze kujikunja ndipo upilizie dawa ya ukungu, UTAKUWA UMECHELEWA.
                Dawa za kuua wadudu kwa tikiti maji:-
                     (i)Selecron
                    (ii)Match
                   (ii)KARATE
                   (iv)DUDU ALL.
DAWA ZA UKUNGU:-  (i)BLUEE COPPER
                                       (ii)EBONY
                                       (iii)Mancozeb.
ZINGATIA: Usipulize dawa wakati wa mchana ili kuepusha kuua wadudu kama nyuki ambao husaidia katika uchavushaji,,, Puliza dawa asubuhi sana au jioni sana. Usisahau pia kuchanganya dawa ya fangasi (FUNGICIDE).
7.Mimea ikianza kutoa matunda weka mbolea aina ya NPK ili kuboresha matunda. Matunda yakishatokea unaweza kukata tawi linaloendelea kukua ili kufanya matunda yakue kwa afya zaidi.

                       FAIDA ZA TIKITI MAJI .
(a)Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamin, mfano vitamin A- Ambayo huboresha afya ya macho pamoja na kuondoa sumu mwilini. Vitamini C pia hupatikan katika tikiti maji, Ambayo huimarisha kinga ya mwili na kuboresha afya ya meno na fizi. Vitamini B6 – husaidia ubongo kufanya kazi vizuri na kubadili protin kuwa nishati.
(b)Tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene ambayo huongeza madini ya potassium mwilini.
(c)Tikiti maji lina amino aside na virutubisho vingine ambavyo husaidia kurahisish mtiririko wa damu kwenye mishipa ya damu.
(d)Tikiti maji lina sifa ya kipekee , lina uwezo wakuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kunywa juisi iliyokamuliwa bila kuondoa maganda yake hii husaidia kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
(e) Huimarisha misuli , vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya potasiam kama tikiti maji huimarisha misuli ya mwili na kuwafaa sana wana michezo.
(f)Husaidia kupunguza uzito wa mwili. Tikiti maji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa sana cha maji , Hivyo kwa mtu anayetaka kupunguza uzito anaweza kula kwa wingi na kujaza tumbo bila kuwa ameshiba sana, hivyo kuwa rahisi kujizuia kula vitu vingine zaidi hata kutwa nzima maana tumbo litakuwa limejaa.
(g)Huimarisha kinga ya mwili . Kirutubisho ch arginine kilichopo kwenye tikiti maji husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
(h)Huondoa sumu mwilini . arginine pia hufanya kazi ya uponyaji wa madonda na kuondoa ammonia na sumu zingine mwilini ambazo zikizidi mtu hujisikia uchovu na kupelekea ugonjwa wa figo na ini.
Hizo ni faida muhimu sana kati ya nyingi za tikiti maji.


 MAZAO NA MAUZO YA TIKITI MAJI.
Kwa shamba lilopandwa 1m shina hadi shina na 2m msitari hadi msitari , kutakuwa na mashina (35X70) = mashina 2450. Kwa kawida shina moja linaweza kutoa matunda kuanzia manne hadi sita.
Tukadirie kila shina litoe matunda mawli jumla (2X2450) =matunda 4900.
Ukiuza kila tunda Tshs 2,000/= utapata (2000X4900) = Tshs 9,800,000/=
Ukichukua pesa iliyopatikana-Matumizi (9,800,000 – 850,000) = Faida Tshs.8,950,000/= (apprx 9 Mill)
Faida hii ya milioni tisa inapatikana ndani ya miezi mitatu tu. Hivyo kama ukiamua kuwekeza katika kilimo hiki na ukafanikiwa kulima angalau mara tatu kwa mwaka tayari utakuwa mtu wa hadhi nyingine kabisa.  Sioni sababu ya kijana kama wewe kukaa ukilalamikia ukosefu wa ajira wakati ardhi iko ya   bure tu.

                       SOKO LA TIKITI MAJI.
-Soko la kwanza kabisa ni wewe mwenyewe kutokana faida zake bila shaka hutaacha kulitumia kwa chakula na familia yako pamoja na watu wanaokuzunguka.
-Safirisha matunda kwenda kwenye masoko makuba na madogo na uza kwa jumla na rejareja.
-Kama mazao ni mengi ongea na watangazaji wa redio au televisheni mtengeneze kipindi cha kijamii kwa ajili kuelimisha jamii kuhusu namna ya kuepuka tatizo la ajila kwa kujiingiza katika kilimo cha tikiti maji, pia mtaeleza umuhimu wa tikiti maji kwa afya. Tafadhali sana usipeleke kama tangazo la biashara maana gharama zitakuwa kubwa sana , baada ya mahojiano acha mawasiliano na utashangaa namna utakavyopata wateja kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi na utauza kwa bei unayoitaka.
-Tengeneza uhitaji wa zao hilo katika jamii inayokuzunguka ikiwa ni pamoja na kuwaonyesha faida za bidhaa yako.
“CREATE A PROBLEM AND THEN SOLVE IT”


                      CHANGAMOTO KATIKA KILIMO CHA TIKITI MAJI.
-Tikiti maji zinahitaji maji mengi hasa kipindi cha kuota na kipindi cha kutoa matunda, Hivyo wakati ambao siyo wa mvua nyingi hulazimu kutumia pesa nyingi katika aidha kuvuta maji kwa jenereta kama shamba liko karibu na vyanzo vya maji , au kununua maji kutoka mamlaka ya maji ambapo gharama zake huwa ni kubwa na wakati mwingine mtu anaweza kushindwa na kusababisha mazao kuharibika.
-Magonjwa kama ukungu wa unga (powderly mildew), ukungu wa chini (downy mildew), ambapo kama mkulima asipokuwa makini kugundua tatizo na kutafuta dawa kwa kwenda kwenye duka la pembejeo na sampuli ili aweze kupatiwa dawa sahihi vinginevyo mimea yake inaeza kuharibika.
-Ukosefu wa mtaji. Wengi wa vijana hulalamika kuhusu ukosefu wa mtaji , lakini mtaji sio tatizo maana mtaji mkubwa ni nguvu zako mwenyewe. Unachotakiwa ni kuwa na mipango tafuta shamba na mbegu hata kama ni kwa kupiga kibarua ,  baada ya hapo unaweza kuanza kulima kidogo kidogo na naamini mahitaji mengine yatapatikana wakati kazi ikiwa inendelea.

                             MWISHO.
-Kijana mwenzagu wa AMKA huu siyo wakati wa kukaa na kuilalamikia serikali kuhusu ajira. Fursa ziko nyingi na kazi yako ni kutengeneza mifereji ya pesa tu kuelekea ndani ya mifuko yako. ACHA UVIVU usiwe kama mtu aliyeweka mkono wake kwenye sahani ya chakula kasha akaona vigumu kupeleka kinywani.( Mithali 26:15)    Biblia kama kitabu kitakatifu imekemea vikali sana kuhusu uvivu, Angalia mafungu yafuatayo;Mithali 6:9-11, mithali 10:4 , mithali 6:6, 2Thesalonike 3:6-9. Mathayo 25:26 , mithali 12:24 na Kutoka 20:8.
“BE POSITIVE, WORK HARD, MAKE IT HAPPEN”.
Preprepared by, Mwl. Robert, Lucas,
                             University Of Dar es salaam,
                             0764075392,
                            0713056903