UKWELI USIOPINGIKA!
SEHEMU YA 2: MSINGI IMARA
NI UKWELI USIOPINGIKA Kuwa Kila mtu aliyezaliwa na mwana hatutegemei abaki kama alivyo, tunategemea akue na kufikia ndoto zake. Ili mtu aweze kufikia mafanikio ni lazima aanze kwa kutengeneza/ kujenga msingi bora na Imara.
Nyumba nzuri na bora ni yenye msingi bora. Ubora wa nyumba unategemea sana ubora wa msingi. Nyumba yenye msingi mkubwa na bora, inaweza kwenda juu zaidi na kudumu zaidi. Msingi ni muhimu sana kwenye nyumba, ndio maana unaweza kuchukua gharama kubwa na muda mrefu kulinganisha na sehemu zingine za nyumba.
Ni UKWELI USIOPINGIKA Kuwa Msingi katika ujenzi ndio sehemu ngumu katika kujenga. Kwenye ujenzi wa nyumba, msingi unapoisha ni rahisi sana kumalizia sehemu nyingine ya nyumba. Msingi unahitaji umakini wa hali ya juu, kwa sababu unapoharibu msingi unakuwa umeharibu jengo zima.
>Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA ni rahisi sana kufanya marekebisho kwenye sehemu nyingine ya nyumba kama kutakuwa na makosa, lakini ni ngumu sana na gharama zake zitakuwa kubwa kurekebisha makosa kwenye msingi. Inaweza kupelekea nyumba kubomolewa kabisa na kuanza ujenzi upya. Huu ndio umuhimu wa msingi.
Kama ilivyo katika ujenzi wa Nyumba, MAFANIKIO pia yana msingi wake. NI UKWELI USIOPINGIKA kuwa Msingi wa mafanikio unapokuwa imara hata mafanikio pia yanakuwa bora. Msingi unapokuwa mbovu na mafanikio yanakuwa mabovu. Unaweza kuyapamba mafanikio kadiri unavyoweza, lakini kama msingi ni mbovu hautafika mbali. Kuna siku utaanguka tu.
Ni UKWELI USIOPINGIKA Kuwa uaminifu, upendo, uadilifu, imani, tabia bora, utii, Ni baadhi tu ya MAWE, KOKOTO, NA MATOFALI IMARA kabisa yanayojenga msingi imara wa mafanikio. Msingi wako unapojengwa na mambo haya, mafanikio yako yatakuwa bora. Ukikosa mambo haya kwenye msingi wako, unaweza fanikiwa kwa kipindi tu ila baada ya muda lazima utarudi nyuma.
Kama tulivyoangalia namna ilivyo vigumu kujenga masingi NI UKWELI USIOPINGIKA kuwa Ukiumaliza msingi wako mapema ndivyo utakavyojenga mafanikio yako kwa haraka zaidi.
>Hivyo ndugu msomaji ni muhimu sana KUJENGA MSINGI WAKO MAPEMA KABISA (wakati ukiwa bado una nguvu).
>Naam, NI UKWELI USIOPINGIKA Kuwa MSINGI IMARA Ndio unaoleta mafanikio makubwa zaidi.
Wito: Jenga msingi mapema, pata
Mafanikio makubwa na mapema zaidi.
LUCAS ROBERT
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com
"LIVE AN INSPIRED LIFE"
