Ticker

6/recent/ticker-posts

UKWELI USIOPINGIKA
SEHEMU YA 1: KUZALIWA.
Ni ukweli usiopingika kwamba hadi kufikia uzaliwe unakuwa umepigana pambano kubwa sana na kushinda ndiyo maana ukazaliwa. Kwa hiyo KILA ALIYEZALIWA NI MSHINDI.
KWA NINI NI MSHINDI?
Kati ya mbegu zaidi ya million 250 wewe peke yako ndiyo hukuawa na asidi zilizo katika mfumo wa uzazi, uliweza kuvumilia safari ndefu sana hadi ukalifika yai, ni UKWELI USIOPINGIKA kuwa hata ulipofikia yai haukuwa peke yako mlikuwa wengi lakini bado wewe peke yako ukafanikiwa kuitoboa ile ngome ngumu ya yai kabla ya wote nawe ukaibuka mshindi. Ni KWELI USIOPINGIKA kuwa wewe ni MSHINDI TAYARI.
Baada ya kushinda pambano hilo ulitamani sana kuikabili dunia na bila shaka tumaini lako lilikuwa ni KUIBUKA MSHINDI tena hata katika dunia hii.
 Naam, baada ya miezi kukamilika ulizaliwa na ukafanikiwa kuuona ulimwengu, NI UKWELI USIOPINGIKA Kuwa ulilia maana mazingira uliyokutana ambayo yalikuwa  magumu na ya kukatisha tamaa. Hukuzoea kuvuta hewa ambayo imechanganyikana na uchafu, vumbi n.k damu yako pia ilitakiwa kufuata njia yake binafsi, moyo wako alikabiliwa na jukumu la kusukuma damu muda wote bila kuchoka, Jotoridi linalobadilika badilika pia lilikuwa linagusa ngozi yako ULILIA. Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA ulitamani urudi ndani ya tumbo la mama lakini uchaguzi wako ndio uliokufanya ukutane na haya.
Kwa kweli kuzaliwa ni UCHAGUZI na NADRA lakini ukishazaliwa kuishi ni lazima. Ni UKWELI USIOPINGIKA kuwa hauchagui sehemu ya kuzaliwa na mazingira ya kuzaliwa, wala mzazi wa kukuzaa.
Kama ambavyo ulipambana kabla hujazaliwa mpaka ukazaliwa pia unatakiwa kupambana katika ulimwengu huu ili uweze kuibuka mshindi katika dunia hii. Ni UKWELI USIOPINGIKA Kuwa mlizaliwa wengi lakini nikuhakikishie kuwa WEWE PEKE YAKO ndiwe MSHINDI. Usimwangalie Mtu mwingine ushindi wake hautakuwa wa kwako ushindi WAKO NI WAKO, pigana kwa ajili yako. Wewe ni was PEKEE Tafuta upekee wako, Weka mipango, IBUKA MSHINDI.
Mazingira uliyokutana nayo baada ya kuzaliwa ni Zawadi na Fursa kwako, usilaumu mazingira uliyoyakuta yapende na uyageuze kuwa siraha yakoo ya ushindi.  Kuzaliwa katika mazingira ya umaskini ndiyo Fursa ya kuonesha badiliko linaloonekana ONESHA UTOFAUTI.
Tafakali hatua za kuzaliwa moja baada ya nyingine chambua mafunzo unayopata ukilinganisha na maisha unayoishi naamini bila Shaka utauona ushindi na upekee ulionao.
>Siku ya Leo naomba nikukumbushe kuwa wewe ni NAMBA MOJA, Usikubali kupoteza nafasi yako.
>Mungu hakupanga uzaliwe MNYONGE, Mungu ni mwenye nguvu na huumba viumbe wenye nguvu pia. Hebu Fanya Mungu ajivunie kwa kuumba kiumbe chenye nguvu kama wewe.
>Ni UKWELI USIOPINGIKA kuwa Wewe ni KIUMBE MWENYE NGUVU, WEWE NI KIUMBE WA PEKEE, WEWE NI MSHINDI.

JIVUNIE KUWA MSHINDI! TETEA USHINDI WAKO.

"LIVE AN INSPIRED LIFE"

Ndimi ,
Lucas Robert
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com