Ticker

6/recent/ticker-posts

UKWELI USIOPINGIKA
SEHEMU YA 4: KUJITAMBUA
Kujitambua ni kitendo cha kung'amua au kuwa na uelewa juu yako binafsi wewe ni nani?, kwa nini upo hapo?, unatoka wapi na unaelekea wapi? unapaswa kufanya nini?, kwa sababu ipi?, lini na katika muktadha upi? Kwa ufupi ni hali ya kuwa na utambuzi juu yako mwenyewe, uwepo wako, hisia zako, mawazo yako, mtazamo wako, njozi zako na hulka yako.
>Ni IKWELI USIOPINGIKA kuwa ikiwa utakuwa na uwezo wa kupata majibu sahihi juu ya maswali hayo hapo juu utakuwa umejitambua.
Saikolojia ya kujitambua tunaweza kuifuatilia na kuikuta kuanzia miaka ya 1972 ambapo wanafalisafa SHELLEY DUVAL na ROBERT WICKLIND'S walitengeneza nadharia kuhusu kujitambua (theory of self-awareness) wakisema
         "Pale tunapokuwa tumegeuza umakini wetu juu yetu wenyewe, tunapopima na kulinganisha tabia zetu za sasa na viwango vyetu vya ndani na thamani yetu, tunakuwa tumejitambua".
Chanzo cha kujitambua ni nguvu ya mwanga juu ya kusudi la kujifunza pamoja na mazoea binafsi.
>Wanafalisafa huamini kuwa kujitambua ndicho kitu cha muhimu kuliko vyote katika ulimwengu, Ni zaidi ya pesa, ni zaidi ya kila utajiri kwa sababu kuna watu ni matajiri au wamezungukwa na utajiri wa kila namna lakini bado hawajajitambua tu.
> Ni UKWELI USIOPINGIKA kuwa "Maisha huanza pale unapojitambua" pale unapokuwa na uwezo wa kuunganisha akili yako na ulimwengu. Ikiwa ulisoma sehemu iliyopita kuhusu UKUAJI tulisema kuwa katika hatua ya tano ya ukuaji ndipo ambapo MTU hupata UELEWA BINAFSI na kwa maana hiyo hapo ndipo maisha yanapoanzia.

UMUHIMU WA KUJITAMBUA.
Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA kujitambua ni muhimu katika nyanja zote za maisha, kiafya, kiakili., kijamii na kiuchumi. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida za kujitambua:-
1). Kujitambua Husaidia kutawala hisia zetu. Kwa mujibu wa Daniel Goleman anasema "uwezobwa kutawala hisia zetu na mawazo yetu kila wakati hutokana na kujitambua vyema.
2. Kujitambua hukuwezesha kuridhika kwa namna ulivyo. Unakuwa na amani kwa namna ulivyo na kujiamin  na hivyo unaweza kulinda mawazo yako, hisia zako, na tabia zako kabla hazijaleta athari.
3. Kujitambua hukuwezesha kutenda kwa weledi kuliko kutenda kwa kukurupuka. Ukijitambua utaweza kufanya maamuzi ya kudumu na yenye kuleta faida katika maisha yako.
4. Kuwa na afya njema ya kisaikolojia na kuwa na mtazamo chanya kuhusu maisha. Ukijitambua utaepuka msongo wa mawazo katika maisha yako na hivyo kuboresha afya yako ya kiakili/ kisaikolojia. Mtu akijitambua atakuwa na mazoea mazuri na anajipatia amani na kuwa mleta amani kwa wengine.
5. Kujitambua hukusaidia kuchagua njia sahihi ya mafanikio. Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa kujitambua ni tabia wu siga muhimu ya wafanyabiashara wenye mafanikio. Hii ni kwa sababu wajua wao ni akina nani na wanatambua vitu ambavyo wanaweza kivifanya vizuri dhidi ya vile wavyoviweza.

KWA NINI NI VIGUMU KUJITAMBUA?
Ikiwa tumjifunza na pengine tunafahamu kabisa umuhimu wa Kujitambua, kwa nini hatujitambui sasa?
> Jibu rahisi ni kwamba muda mwingi kwa ufupi ni kwamba huwa hatupo kujitàzama wenyewe. Kwa maneno mengine ni kwamba huwa hatutilii maanani kile kinachoendelea kutuzunguka na  ndani yetu.

>Wanasaikolojia Matthew Killingsworth and Daniel T. Gilbert waligundua kuwa zaidi ya nusu ya muda tunapokuwa katika mfumo huria (automatic pilot) kile tunachofanya., tunachokihisi au kukifiria kinakuwa ni tofauti na cha wakati huo na pale tulipo, akili zetu zinakuwa sehemu nyingine kabisa.
>Upendeleo katika ufahamu wetu pia huathiri uwezo wetu wa kujitambua kwa usahihi zaidi.

NJIA TANO ZA KIJITAMBUA.
1.JITENGENEZEE NAFASI.
Ikiwa utakaa katika chumba kidogo chenye giza na kisicho na madirisha, Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA Sio rahisi sana kuona vitu vilimo humo ndani. Nafasi ninayoisemea hapa ni kuhakikisha unatoboa ukuta ili kuruhusu mwanga kuingia ndani. Kila siku hakikisha unajipa muda na nafasi, mfano nusu SAA asubuhi au jioni kabla ya kulala unakaa mbali na vifaa vya kisasa kama simu TV n.k, unatumia muda huo peke yako (faragha) ukisoma, ukiandika au ukijitafakarisha wewe mwenyewe.

2. JIZOEZE KUWA MYAKINIFU
Uyakinifu ndio ufunguo wa kujitambua. Jon Kabat-Zinn alielezea Uyakinifu ni kutilia maanani kwa namna fulani, kwq sababu Fulani, kwa wakati huo na bila kuhukumu. Kwa kuendekeza uyakininifu utajijengea uwezo wa kuwepo na kutazama mile kinachoendelea ndani yako na nje yako. No kile kitendo cha kuweza kuyatuliza mawazo yako. Unaweza kufanyia mazoezi uyakinifu wako kwa kusikiliza kiyakinifu, kutembea kwa uyakinifu na kula Kiyakinifu.

3. TENGENEZA MAKALA (JOURNAL). Uandishi sio kwamba husaidia kutengeneza fikra  zetu tu Bali pia hutufanya kujisikia amani au kupata amani ya nafsi. Uandishi piia hukusaidia kutengeneza nafasi kichwani mwako kwa vile unavyoruhusu mawazo yako kutiririka kwenda na kutoka kwenye karatasi zako. Ni UKWELI USIOPINGIKA kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika hivi karibuni unaonyesha kuwa kuandika vitu hata vile ambavyo unapambana navyo hukufanya uwe na FURAHA na utoshelevu.
>Unaweza kutumia makala hiyo kurekodi hali yako ya ndani (your inner state).
>FANYA ZOEZI HILI: Tafuta nusu ya siku mwishoni mwa juma, Elekeza umakini wako katika hali yako ya ndani, namna unavyojisikia, Namna unavyopenda kujisemea, Andika kila utakachokuwa unakiona kila baada ya lisaa, Unaweza ukashangaa kile ambacho utaandika, lakini hivyo ndivyo hali ilivyo kwa kila MTU akiamua.

4. Jizoeze kuwa msikilizaji mzuri.
Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA kusikiliza sio sawa na kusikia. Kusikilizo ni kuwa hapo au kuonesha uwepo na kuwa makini kwenye hisia, muonekano na muindoka wa mwili na lugha ya watu wengine. Ukiwa msikilizaji mzuri utakuwa na uwezo wa kuijisikiliza hata wewe mwenyewe vizuri na hivyo utajenga urafiki mzuri ndani yako (kati yako na nafsi yako) ila sijamaanisha kuwa uwe mbinafsi.

5. Tafuta mrejesho. Wakati mwingine tunaweza tukawa waoga sana kuuliza namna ambavyo watu wanatufikiria tulivyo, lakini wakati mwingine mrejesho inaweza kuwa ni wa upendeleo au usiokuwa na uaminifu, lakini utakuwa na uwezo wa kuutofautisha na hali halisi na namna unavyojifunza na kujifahamu wewe mwenyewe.
>Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA kila mtu ana sehemu au sifa ambazo hata yeye mwenyewe hajui kama anazo (Blind spot), kwa hiyo kupata mrejesho hutusaidia kupata picha nzima kuhusu sisi wenyewe. Sisi kama binadamu hàtuwezi kujifahamu sisi wenyewe kwamba tupo hivi au tutakuwa vile. Lakini tu ni safari endelevu ya uchunguzi, uelewa na kuwa sisi wenyewe ndicho kinachofanya maisha yetu yanakuwa na THAMANI.

MPENDWA msomaji ningependa kupata mrejesho kutoka kwako, lakini kabla sijasikia kutoka kwako ngoja niseme kidogo kuhusu ukweli huu usiopingika kuhusu kujitambua. Kujitambua hukupa uwezo wa kutambua kama unachokifanya kinaendana na wewe au unafanya kitu cha MTU mwingine, je mafanikio uliyo nayo yanaendana na wewe au la! Unaweza kuwa umefanikiwa lakini kumbe kama ungekuwa umejitambua mafanikio yako yangekuwa makubwa zaidi ya hayo.
>Kujitambua ndiko kutakuonesha njia sahihi ya mafanikio yako. Kama utagundua kuwa wewe ni mwalimu mzuri basi tumia ualimu wako kukuletea mafanikio, kama wewe ni mwandishi mzuri tumia tumia kalamu yako kukuletea mafanikio, kama were ni mbunifu tumia ubinifu wako kujiweka kileleni.
Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA kujitambua ni MUHIMU sana kwa sababu ndio hulufanya uwe MTU. Kwa sababu kama hujui kuwa wewe ni TAJIRI huwezi kuwa TAJIRI Kwa sababu hutajua kuishi namna ambavyo matajiri wanaishi.
Watu wengi wamefahamu umuhimu wa kujitambua ndiyo maana waandishi wengi sana kama kina Anthon Luvanda, Erick shigongo, Fred Msungu, Adam Ngamange, Erick Chrispin n.k wameamua kujikita katika kuwaelimisha watanzania kuhusu lujitambua maana Elimu hii inaonekana ni adimu sana kwa vijana wa kitanzania, Naona muda si mrefu watafanikiwa nami nawapongeza kwa juhudi zao.

Ndugu msomaji, Je umeona nguvu ya kujitambua katika Kazi yako unayofanya?
Andika maoni uako kwenye kibox kilichoandikwa "WRITE YUOR COMMENT"

LUCAS ROBERT
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com

"Live an Inspired Life"