UKWELI USIOPINGIKA.
SEHEMU YA 5: VIPAUMBELE.
Kipaumbele ni kile kitu cha muhimu ambacho kinafanywa kwanza kabla ya vitu vingine (kitu cha muhimu zaidi kinapewa nafasi ya kwanza).
Kuweka kipaumbele maana yake ni kuchagua kitu kimoja cha kufanya katika vitu vingi ambavyo unaweza kufanya katika wakati fulani. Hii ina maana kwamba katika wakati wowote ule unaweza kufanya hata vitu kumi, lakini wewe unaachana na vitu vingine vyote na kuweka akili yako yote, mawazo yako yote na moyo wako wote kwenye kufanya kitu kimoja tu. Kitu hicho kinaweza kuwa na manufaa kwako au kisiwe na manufaa.
Kama kuna tabia moja ambayo inaweza kukufanya wewe uendelee kubaki kwenye mstari utakaokufikisha kwenye mafanikio, basi ni tabia ya kuweka kipaumbele.
Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA pindi unapojua vipaumbele hukusaidia kufanya uchaguzi sahihi ambao utakuretea manufaa.
> Maisha yetu Ni uchaguzi wetu. Ninachokiamini ni kwamba kila MTU anawajibika kwa ajili ya Maisha yake mwenyewe, anawajibika kwa maamuzi yoyote anayofanya katika maisha na matokeo ya maamuzi hayo.
>Pia naamini kwamba tunaweza kuepuka makosa mengi sana katika maisha ikiwa tutapanga vitu vyetu viziri na kutambua vipaumbele vyetu. Unapokuwa umeweka vipaumbele unakuwa umetengeneza TASWIRA nzima ya maisha yako. Na baada ya hapo unaweza ukawa unajazia vitu vidogo vidogo katika mhimili wa taswira uliyoiweka na kufanya maisha kuwa ya kupendeza. Ni UKWELI USIOPINGIKA KUWA huwezi kuanza kwa kuweka vitu vidogo kwanza katika maisha kabla ya kutengeneza mhimili wa maisha yako.
Hivyo basi ni muhimu sana kutambua vipaumbele vyako na kutengeneza mazingira mazuri kuzunguka vipaumbele hivyo.
Watu waliowengi wameweka vipaumbele vifuatavyo maishani mwao: (sijavipanga katika mtiririko maalumu)
#* Taaluma
#** Familia
#***Afya
#**** Marafiki na matakwa binafsi (self interesting).
#***** Mahitaji ya kiroho
#******Pesa.
NB: Unaweza kuongeza kipaumbele kingine chochote unachofikiri ni muhimu.
Kitu cha pili hapa ni kuchagua namna ya kuvipanga hivyo vipaumbele. Haiwezekani ukavitilia maanani vipaumbele vyote kwa wakati mmoja.Ni ukweli usiopingika kuwa katika maisha unahitajika kuacha baadhi ya vitu ili kuweza kuleta usawa katika vipaumbele. Mfano , Mara nyingi huwa tunahitajika kuweka kando matakwa binafsi ili kuweza kuweka kipaumbele cha pesa mbele kwanza.Wakati mwingine unahitajika kuchagua kipi Ni cha muhimu zaidi: kula chakula na kufurahi na wanafamilia wenzako au kuhudhuria semina/ kikao na wafanya Kazi wenzako?
Kiukweli siwezi kukupangia namna ya kuweka vipaumbele, kwa sababu kila mtu ana njia yake ambayo anatakiwa kupitia ili kufikia NDOTO zake. Hakikisha kipaumbele chako kikuu Ni kufikia NDOTO yako.
UMUHIMU WA KUWEKA VIPAUMBELE
Ni ukweli usiopingika kuwa siyo kwamba kila MTU ambaye hajafanikiwa kwamba hafanyi Kazi kwa bidii, Hapana wanajibidisha sana lakini tatizo Ni kwamba hawajui namna ya kuweka vipaumbele.
Zifuatazo Ni faida za kuweka vipaumbele katika maisha:-
1. Hukufanya uweze kubaki katika njia yako ya mafanikiwa. Duniani Luna vitu vingi sana vya kufanya ambavyo vina manufaa lakini Ni UKWELI USIOPINGIKA kuwa ikiwa utaamua kuvifanya vyote kwa wakati mmoja mafanikio kwako yatakuwa Ni magumu sana. Ikiwa utaweka vipaumbele bila shaka utajizuia kufanya vitu amvavyo vinakutoea katika msitari hivyo kuwekeza nguvu zaidi katika kitu kimoja ulichokichagua kwa ajili ya manufaa yako.
2.Hukuwezesha kuwa na uwezo wa kuukomboa wakati. Ikiwa umeshaweka vipaumbele hautapoteza muda kufanya vitu ambavyo sio vya muhimu kwako. Hautarukaruka kutafuta au kuchagua cha kufanya kati ya vitu vingi vilivyopo mbele yako.
3. Ukiweka vipaumbele utaweza kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati. Maamuzi yote ambayo utakuwa unayafanya yatakuwa yanakuelekeza kwenye vipaumbele vyako na hivyo hutahitajika kukaa chini kila Mara na kuamua cha kufanya Bali utakuwa tayari una orodha ya vitu unavyotakiwa kuvifanya na kwa wakati gani.
3. Kuweka vipaumbele hukufanya usiwe mtumwa wa mazingira. Mazingira yanabadilika na wakati mwingine yanaweza kukulazimisha kufanya vitu ambavyo viko nje ya mpango wako wa kila Siku. Hivyo kama umeweka vipaumbele vyako utweza kuyatawala mazingira. Hapa sijamaanisha kuwa usiendane na mabadiliko yanayotokea katika mazingira Bali ninachosema Ni kwamba kabla hujabadilika kulingana na mazingira angalia vipaumbele vyako Ni kwa namna gani vitaweza kuathirika na mabadiliko hayo na ndipo ufanye mabadiliko kidogo kuendana na mzingira. Lakini pia sio lazima uendane na kila mabadiliko hayo Bali unatakiwa uangalie namna ya kuzikabili changamoto zinazoletwa na mazingira kwenye vipaumbele vyako. (Keep it balanced!).
Naomba nikukumbushe kitu kimoja kuhusu vitu unavyo vifanya.
Ni UKWELI USIOPINGIKA kuwa Sifa za kazi tunazozifanya zinaangukia kwenye mojawapo ya ya makundi manne ya Kazi kama ifuatavyo:-
1. Kazi zaraka na muhimu
2. Muhimu lakini sio za haraka
3. Haraka lakini sio muhimu.
4. Sio za haraka wala sio muhimu .
Haraka na muhimu.
>Mfano wa kazi za muhimu na za haraka ni kumshughulikia mgonjwa, kuzika mtu wako wa karibu, kushughulikia nyumba yako iliyotetekezwa na moto. Mtoto wako aliyeibwa, nk
>Muhimu lakini sio za haraka
Mfano wa kazi za muhimu lakini hazina haraka ni kazi zote za kupanga hasa zile za muda mrefu kama kupeleka watoto shule wewe mwenyewe kwenda kusoma zaidi, kulima shamba, kujenga nyumba nk
>Haraka lakini sio muhimu.
Mfano wa kazi za haraka lakini hazina umuhimu ni kupokea simu ambazo hukuzitegemea, wageni wasiotarajiwa, kuchangia harusi, sendoff, kupewa mwaliko wa safari au tafrija kwa notice ya muda mfupi nk.
>Sio za haraka wala sio muhimu
Mfano wa kazi zisizo na haraka na umuhimu ni kulewa, kupiag zoga, kucheza bao, kuchat kwenye mitandao, kulala nk. Ili kazi ziwe ni za kupoteza muda ni lazima ziwe hazijapangwa na hazina umuhimu wowote. Kama zimepangwa na zinalenga kuleta ufanisi wa kiafya au kikazi nk hizo sio vipoteza muda
Unaweza sasa kutumia dhana hiyo hapo juu kama kazi ni ya muhimu, haraka, sio muhimu au sio haraka kuweka vipaumbele vya kazi zako zote.
Naam, mpendwa msomaji vipaumbele vyako Ni dira ya mafanikio yako hivyo Ni muhimu sana kuweka vipaumbele vyako hasa katika mfumo wa maandishi.
Ili kuweza kuandika vipaumbele vyako vizuri lazima ujue kule unakoelekea na kwa nini unataka kufika huko. Na haya yote utaweza kufanya tu ikiwa utakuwa na MISSION STATEMENT yako.
Kama hukusoma makala iliyokuwa unaeleza UMUHIMU WA MISSION STATEMENT UNAWEZA KUBOFYA HAPA CHINI ili uisome kwanza kabla hujaweka vipaumbele maishani mwako.
http:/ngwakwaufanisi.blogspot.co.ke/2017/03/importance-of-mission-statement-in-life.html?m=1
"Nioneshe vipaumbele vyako nami nitakuonesha mafanikio yako"
LUCAS ROBERT
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com
"Live an inspired life
