UKWELI USIOPINGIKA
SEHEMU YA 7: CHANGAMOTO
Changamoto ni hali ambayo mtu hukutana nayo maishani ambayo huhitaji juhudi kubwa ya kiakili na kimwili ili kuweza kufanikiwa. Changamoto ya mtu mmoja hutofautiana na changamoto ya mtu mwingine hii ni kwa sababi changamoto ni "fundisho la mtu binafsi Na ni kwa sababu tunatofautiana katika kila kitu, historia ya maisha, uwezo wa akili na mwili na hata mitazamo ya namna tunavyochukulia maisha.
> Ni UKWELI usiopingika kuwa changamoto zinakuwepo ili kukuza na kupima uwezo au nguvu Yako ya ndani. Changamoto hutufanya tukue huku tukiwa tunajitambua na kutufanya tutoke tukiwa tunang'aa kama dhahabu.
Martin Luther king JR (1929 - 1968) Aisema "kipimo cha mtu sio mahali anaposimama katika nyakati za amani Bali ni wapi anaposimama katika kipindi cha changamoto na kuchanganyikiwa"
Kipindi dhoruba isiyotarajiwa inapojitokeza na kukupata kwa ghafula hebu ione kama funzo.
> Kama changamoto zipo katika ukubwa sahihi na ukafanikiwa kuzishinda ndipo unapopata furaha na amani ya moyo na utashawishika kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto.
UMUHIMU WA CHANGAMOTO.
1. Hukufanya uwe mwajibikaji.
Ni ukweli usiopingika kuwa Uwajibikaji wa mtu hupimwa kipindi cha changamoto kwa sababu katika kipindi kama hicho ikiwa hautawajibika bila shaka matokeo yake yatakuwa makubwa na yataonekana kwa kila mtu.
Mfano kipindi ambapo uongozi wa juu napobadilika bila shaka kama hutawajibika ipasavyo ni wazi kuwa utashindwa kusonga mbele na utaanguka kabisa.
2. Changamoto hukupa mwaongozo.
Kuna watu ambao wanafurahia kuogelea ndani ya habari iliyotulia lakini kipindi mawimbi yanapoanza katika bahari ni lazima uchague upande ambao unataka kwenda. Na kwa hiyo changamoto ndiyo hukufanya uchague njia yako mwenyewe kwa manufaa yako binafsi bila kuangalia wengine wanasemaje na wanaona nini katika changamoto hizo.
3. Changamoto hukusaidia kukikaribia kile unachotarajia kukifikia.
Ni UKWELI usiopingika kuwa kupitia changamoto ndipo unapata nguvu zaidi ya kupambana na hivyo pale utakapopita kwenye changamoto hiyo utakuwa umeongeza gnuvu ya ziada ambayo itakusukuma kwa kasi kuweza kikaribia ndoto yako.
NAMNA YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO.
> Kila mtu hupenda maisha rahisi yasiyokuwa na changamoto kubwa. Lakini ni ukweli isiopingika kuwa changamoto ni jambo lisilokwepeka maishani na ni sehemu ya maisha kwa sababu changamoto hukuwezesha kutumia rasirimali zilizopo ndani yake. Hivyo ni vyema ukafahamu namna ya kukabiliana na changamoto kumbuka "changamoto ndiyo maisha yenyewe".
Zifuatazo ni baadhi ya njia za kukabiliana na changamoto:-
1. Ikubali changamoto.
Namna ya kwanza kabisa ya kuikabili changamoto ni kuikubali na kuichukulia kama jambo ambalo ni la lazima na haliepukiki na hivyo huna budi kupambana nayo hadi uishinde. Simaanishi kuwa changomoto ikufanye mnyonge na ujisikie kuwa huna nguvu Bali jifunze namna ya kuibeba kwa ujasiri kama sehemu ya maisha na kuaonga mbele. John kabat alisema "Huwezi kuyazuia mawimbi kupiga Bali unatakiwa kujifunza namna ya kuyakabili"
2. Tambua kwamba njia nzuri ya kutoka kwenye changamoto ni kutembea ndani yako. Ni UKWELI usiopingika kuwa usipotembea ndani ya changamoto huwezi kufika uendako. Utakuwa sawa na mtu aliyekatikiwa na ndala njiani naye akakaa chini na kuanza kulaumu kwa nini hii ndala imekatika hapa, badala ya kubeba ndala na kendelea na safari.
3. Acha mitazamo yako yote iyeyuke na kuchemka mpaka iwe mvuke na kupotea. Ni UKWELI usiopingika kuwa mtazamo ndiyo adui mkuu wa ndiyo mafuta ya injini ya maisha yako, ikiwa mtazamo wako ni kwamba pindi unaputana na changamoto unaona huwezi kuendelea mbele basi acha mitazamo hiyo iyeyuke. Robert kiyosaki alisema, "Ili ifanikiwe ni lazima hamu au tamaa ya mafanikio iwe kubwa kuliko hofu ya kushindwa".
4. Tambua kuwa kuna somo unatakiwa ujifunze kupitia changamoto hiyo.
Unapokuwa kwenye changamoto sio wakati wa kuchanganyikiwa na kumtafuta mchawi wa mafanikio yako, Bali ni wakati wa kukaa chini na kutafakati kile ambacho unatakiwa kujifunza. Ni UKWELI usoipingika kuwa changamoto ni mwalimu mzuri sana katika maisha yetu ya kila siku hasa pale tunapotembea kuyaelekea mafanikio yetu. Tafadhali usiiache changamoto yoyote ile ipite bila kukufundisha kitu.
5. Tafuta hatua sahihi inayotakiwa kuichukua. Usahihi wa hatua ya kuchukua ni jambo la muhimu sana, sio kila changamoto inayojotokeza ni lazoma uanze kupambana nayo papo hapo Bali tumia hakima na mazingira na wakati mwingine utatakiwa kusonga mbele tu na kuruhusu muda useme. Kwa hakika utaona matokeo yake.
Hivyo basi namna nzuri ya kukabili changamoto ni kuikibali changamoto na kutambua kuwa njia sahihi ya kutoka humo ni kutembea ndani yake huku ukiiacha mitazamo yako yote iyeyuke na kuchemka wakati ukifanya juhudi kutambua somo unalotakiwa kujifunza kupitia changamoto hiyo Na kisha kuchukua hatua sitahiki kuhusu changamoto hiyo.
Mafunzo 7 Unayojifunza kupitia changamoto za Maisha.
1. Unahitaji kujifunza.
Kuna wakati ambapo vitu huenda ndivyo sivyo na wengi wetu hujaribu kukwepa na kuupinga ule UKWELI ambao maisha yetu halisi yanauonyesha. Wakati matatizo yanapojitokeza Ni UKWELI usiopingika kuwa kuna kitu hakiko sawa. Mfano; unaweza kuugua kwa sababu hukufata kanuni fulani za afya kama kula vizuri, au unaweza kuwa na madeni kwa sababu unaishi nje ya uwezo wa kipato chako, mchumba wako anaweza kukuacha kwa sababu unaonesha ubabe n.k.
Kwa hiyo badala ya kuyalalamikia maisha angalia maisha yako na utaona kitu ambacho unahitaji kukiboresha.
Kushindwa kukubali ukweli ambao maisha yanakiambia utajikuta katika mtego ambao hutaweza kutoka wala hakuna mtu atakayeweza kukutoa.
Mo seetubtim alisema kwamba "Kitu cha kukosesha amani hutokea maishani ili kutufundisha kwa sababu mabadiliko huwa hayaji kama kama hakuna kitu cha kukoseha amani"
2. Huwezi kuyarekebisha maisha Bali unatakiwa kujirekebisha wewe mwenyewe.
Ni UKWELI usiopingika kuwa kuna mazingira ambayo we we huna nguvu juu yake, mfano: kuzaliwa katika familia ambayo haina uwezo, Kufiwa na ndugu au rafiki, kupata ajali isiyotarajiwa n.k.
No seetubtim pia alisema kuwa "wakati unapokuwa unapitia changamoto za maisha una uchaguzi wa kuanguka na kuwa mhanga wa mazingira au kuinuka zaidi kuliko wengine"
>Kwa vyovyote vile haijalishi ni kitu gani kitatokea ikiwa unaweza kujizuia mwenyewe, hautapuuzia changamoto zinazojitokeza Bali uatzitumia kama ngazi ya kukupandisha juu kufikia mafanikio yako.
Jijengee mwenyewe mazingira yenye afya, jitengenezee nguzo yako mwenyewe, jizungushie wewe wigo wa vichocheo vizuri, jijengee maarifa na ujuzi wala usichoke kujiendeleza kwa sababu "maisha siyo ya kwako bali maisha ni kwa ajili yako.
3. Huwezi kubadili namna vitu vilivyo Bali unaweza kubadili mtazamo wako juu ya vitu.
"Huwezi kubadilisha chochote juu vitu vinavyokutokea Bali unaweza kubadilisha mtazamo wako wako juu ya kile kinachotokea kw a namna hiyo utakuwa mtawala wa mbadiko wala sio mtawaliwa wa mabadiliko" Hayo ni maneno ya Brian Tracy.
Ni UKWELI usipingika kuwa kushinda changamoto za mausha inahitaji nguvu, nguvu za kiakili na nguvu za kimwili pia kwa sabavu vyote huenda kwa pamoja. Unahitajika kufumu kuwa na nguvu, Na hivyo unahitaji msaada kutoka kwa ndugu na msaada kutoka kwa marafiki, na muhimu zaidi unahitajika kubadili mtazamo wako wa nje kuhusu maisha.
> Tonny Robbin alisema "siri kubwa ya mafanikio ni kujifunza namna ya kutumia raha na maumivu badala kuruhusu raha na maumivu vikutumie" Tumia maimivu kukupa motisha, kuwa na malengo zaidi na kufanya juhudi zaidi ili kufanikiwa.
4. Wewe ndiwe mtu mwenye nguvu zaidi. Mazoea yako ya nyuma ndio mtaji wako wa ushindi kwa kila jambo unalokumbana nalo.
Oliver Wendell Holmes , Jr. Alisema akili ambayo imetanuliwa kwa kujazwa mawazo na mazoea mapya haitaweza kurudi tena katika hali yake ya awali.
"Kufahamu kuwa wewe ni mtu mwenye nguvu ni Baraka tosha kwa sababu nguvu ya akili ndiyo nguvu kubwa kuliko zote.
5. Wewe ndiyo ndiye adui mbaya na ndiye rafiki mzuri zaidi wa nafsi yako mwenyewe.
Adui yako hawezi kukudhuru kama ambavyo akili yako isiyokuwa na ulinzi inavyoweza kukudhuru.
Kuna kipindi ambapo maisha yanakupiga na kukufanya ujichukie nafsi. Unajichukia kwa sababu ya wale walio kitendea ubaya katika siku zilizopita. Unajichukia mwenyewe kwa kukosa nidhamu ya kufanya vitu sahihi, unajichukia kwa sababu ya makosa katika maisha yako yaliyopita, Inasikitisha na kuhuzunisha kwa vile usivyoweza hata kujisamehe mwenyewe.
Ikiwa unataka kwenda mbele jipatie msamaha mwenyewe kwa Yale yote uliyokosea na usonge mbele.
>Unaweza kichagua kuwa rafiki wa nafsi yako mwenyewe ama kuwa adui wa nafsi yako mwenyewe. "Fanya uchaguzi kwa makini".
6. Unawafahamu marafiki zako wa UKWELI.
Unapokuwa katika hali mbaya marafiki zako wanakufahamu ulivyo hats unapokuwa katika hali nzuri bado marafiki zako watafahamu ulivyo. Ni UKWELI usiopingika kuwa katika nyakati za raha marafiki huwa ni wengi sana, lakini wakumbuke sana wale marafiki wanaobaki na wewe hata unapokuwa katika hali mbaya. Marafike wale ambao wanaweza kuwekeza muda wao na rasirimali zao ili kuweza kukuinu hao ndio marafiki wa UKWELI. Marafiki wa UKWELI hutembea na wewe pindi dunia nzima inapokukimbia. Wakati mzuri mno maishani ni pale unapifahamu yupi ni wa muhimu zaidi na yupi si wa muhimi zaidi. Wakati unapofahamu marafiki zako wa kweli wakumbatie, maana ni vigumu sana kuwapata.
7. Kutambua vitu vya muhimu na vile visivyo vya muhimu.
Unapokuwa vizuri kiuchumi utapendekea kwenda baa, kufanya manunuzi katika maduka makubwa, kusafiri na kutalii. Lakini pale maisha yanapokuwa magumu kiuchumi hutaweza kufaya yote hayo Bali itakubidi kufanya uchaguzi juu ya kipi ni cha muhimu zaidi na kipi si cha muhimu zaidi. Unatakiwa kujifunza kuishi maisha rahisi na kuyafurahia naana pindi Yale ya starehe unayoyafurahia yatakaposhindikana hutakuwa na furaha tena. Jifunze kufurahi na marafiki zako muda mwingi maana rafiki wa UKWELI hufurahi nawe hata katika ßhida.
Mpendwa msomaji ni UKWELI usiopingika kuwa utakuwa umejifunza kitu Fulani kuhusu changamoto na bila shaka kuanzia sasa utakuwa na mtazamo mpya kuhusu changamoto. Nami nakusihi ruhusu mtazamo wako wa zamani uyeyuke ili uwe na mtazamo mpya. Angalia Fursa au funzo lililo katika kila changamoto.
Nawe utaona mafanikio yanavyokujia kwa haraka.
LUCAS ROBERT
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com
"Live an inspired life"
