Ticker

6/recent/ticker-posts

UKWELI USIOPINGIKA.
SEHEMU YA 9: HATIMA YAKO.
Hatima yako ni mahali unapotamani sana kufika. Bila shaka kila mtu anatamani kuwa na hatima njema katika kila nyanja, kiuchumi, kiroho na kijamii. Ni UKWELI usiopingika kuwa hakuna mtu yoyote aliye na dhamana ya kukutengeneza hatima yako, mtu wa kuamua hatima yako ni wewe mwenyewe. Na ieleweke kuwa kila hatua unayoipiga maishani mwako inaandika historia  isiyoweza kufutika na hatua hizo unazozipiga ndizo zitakazoamua hatima ya maisha yako. Ikumbukwe kuwa japokuwa maisha yako yaliyopita hayawezi kufutika lakini hayana thamani yoyote katika hatima yako kile unachopanga kukifanya kwa sasa ndicho kitakachoamua hatima ya maisha yako. Wengi huamini kuwa hatima ya maisha yao hujengwa na matukio fulani makubwa, hii si kweli, kama ambavyo mti hauwezi kukua na kuzaa matunda kwa siku moja kutokana na maji mengi yanayoweza kumwagiliwa kadhalika hatima ya mtu haijajengwa katika tukio moja tu hata kama likiwa ni la kusisimua kiasi gani bali ni hatua ndogo ndogo na matukio yenye mvuto wa manufaa.
> Ukubali au usikubali watoto wako wanatamani kukuta historia ambayo watajivunia na watatamani kuishi maisha ambayo uliishi. Kadri matukio yenye manufaa yanapokuwa mengi ndivyo hatima yako itakavyowavutia wengi. Tengeneza hatima ambayo itabaki hai baada ya wewe kuwa umepita.
> Ni UKWELI usiopingika kuwa kila mtu ana hatima yake binafsi, na hatima yako inatofautina na ya mtu yeyote, ni muhimu sana kutambua ni wapi ambako unaelekea ili kuamua hatima yako. Huwezi kufika kule unakotaka kufika kwa bahati mbaya, Bali kuna vitu ambavyo ni lazima uvifuate ili kutengeneza barabara iliyonyooka ili kukuwezesha kufikia hatima yako yaani pale unapotamani kufika au namna unavyotamani kuwa.

Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vitakavyo kusaidia kufikia pale unapotamani kufika:-
1. Tambua pale unapoelekea.
Ni UKWELI usiopingika kuwa ikiwa hufahamu mahali unapoenda huwezi kwenda popote. Kadhalika hats katika maisha pia iko vile vile. Kama huna malengo mahususi, na NDOTO zinazofikika ni dhahiri kuwa wewe utakuwa hujaanza kuyaishi maisha Bali utakuwa unaisha tu na hakuna chochote ambacho utakifanikisha katika maisha yako.

2. Chora picha au ramani ya kukufikisha uendako.
Kufahamu kule uendako hakukufanyi uweze kufika pale kwa kutengeneza njia yako yoyote tu. Kuwa na taswira au ramani inakusaidia kupanga njia ya kupita na kukufanya ujiamini kuwa uelekeo ulio nao ni uelekeo sahihi. Malengo pekee yake hayakufanyi ufanikiwa, Bali ni mpango mkakati ndio hukufanya utekeleze mambo yatakayokufanya ufike ulipopanga kufika. Mpango mkakati ndio hukutaarifu hatua inayofuata kila baada ya kumaliza hatua moja na hatua kwa hatua unaanza kufikia malengo. Kwa ufupi kutengeneza ramani ni kuvunja vunja malengo ili kutengeneza mipango tendaji midogo midogo iliyojengeka ndani ya malengo yayak.

3. Fuata njia yako.
Watu wengi wanafahamu kile wanachokihitaji maishani na tayari wanayo mipango mikakati ya kuwafikisha pale wanapohiaji kufika, lakini zipo baadhi ya sababu ambazo huawafanya watoke katika njia zao binafsi. Kwa watu wenye busara hali kama hii inapojitokeza huwa wanajitahidi kurudi katika njia yao haraka sana, lakini mtu mwingine kwa kutokufikiria vyema huamua kuendelea katika njia hiyo hiyo yenye makosa na kujikuta maisha yao yanaishia kuwa yenye maumivu makali na yasiyo furahisha kabisa. Ni UKWELI usiopingika kuwa kila mtu huwa anacho kitu anachokifurahia zaidi maishani mwake, kitu ambacho unakifurahia zaidi ndiyo njia yako ya mafanikio usiige njia za watu wengine kuna uwezekano wao peke yao ndiyo wanazifurahia lakini wewe hutazifurahia hivyo unatakiwa kutafuta njia inayokufurahisha wewe itakayokufikisha kwenye hatima yenye furaha.


4. Ondoka hapo ulipo.
> Unaweza kuwa unaifahamu njia, una picha halisi ya malengo yako, na umeshachagua njia ya kupita lakini kama hutaamua kuondoka utabaki pale ulipo wala hutafika kule unakotaka kufika. Mwandishi mmoja aliyeandika kwa kiingereza aliandika akisema: "If you you don't step forward you're always on the same place and if you don't ask the answer is always No" akimaanisha "Kama hutapiga hatua Siku zote utabaki pale pale na ikiwa hautauluza jibu siku zote Ni HAPANA". Watu wengi wana mawazo chanya na wanafahamu wanapotakiwa kufika na namna wanavyotakiwa kufanya ili wafike wanapitakiwa kufika, lakini kutokana na HOFU, UVIVU, AU KUKOSA NIDHAMU YA MAISHA ndiyo maana mpaka sasa hawajaamua kuanza.

Ndugu msomaji Tafadhali usiwe miongoni mwa watu kama hao. Anza Leo kutengeneza hatima yako, usisubiri mtu mwingine akuamulie hatima yako. Ni UKWELI usiopingika ikiwa hautachagua mausha mtu mwingine atakuchagulia maisha, kama hutaamua hatima yako basi mtu mwingine atakuamulia.

> Inuka sasa anza kidogo kidogo, tafuta nguvu, na uwe na nia moja mpaka ufike unapitamani kufika.
"Kesho yako inajengwa na Leo"

Nakutakia kila rakheri unapoamua na kutengeneza hatima yako.

LUCAS ROBERT
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com

"Live an inspired life".