Ticker

6/recent/ticker-posts

UKWELI USIOPINGIKA.
SEHEMU YA 10: WARAKA.
Nakuandikia wewe kijana kwa sababu bado una nguvu, macho yako bado yana nguvu, mikono yako bado ina nguvu, miguu yako bado ina nguvu, neno utakalolisema ukiamua kwa kumshirikisha Mungu linatendeka.

>Katika waraka huu ambao ndio sehemu ya mwisho kabisa katika mwendelezo wa UKWELI USIOPINGIKA, Nitapenda kuelezea kuhusu uwezo na nguvu alizonazo kijana namna anavyotakiwa kuzitumia.
>NI UKWELI USIOPINGIKA kuwa kundi ambalo linatakiwa kuonesha umakini Mkubwa katika utendaji wa mambo yote ni kundi la vijana, ukipoteza umakini katika kipindi hiki ni wazi kabisa uzee wako utakuwa na taabu zisizoelezeka.

Kwa nini maamuzi katika kipindi cha ujana yanatakiwa kufanyika kwa Makini?
1. Maamuzi anayofanya kijana ni kwa ajili ya manufaa kwa maisha yake ya baadaye. Pamoja na kwamba kijana huwa ana nguvu Fulani ambayo humshawishi kujifurahisha kwa wakati huo Bali ni vyema sana kila maamuzi anayoyafanya yakawa na faida kwa maisha ya baadaye kuliko faida ya muda kitambo tu.

2. Kipindi hiki cha ujana ni kipindi cha kuchagua. Kipindi cha kuchagua Kazi, kuchagua marafiki, kuchagua maisha, kuchagua mwenzi na kuchagua mtindo wa maisha. Bila shaka ukiambiwa kuchagua kitu miongoni mwa vitu ni lazima utakuwa makini kwa kutafiti ubora na udhaifu uliomo baina ya hivyo vitu.

3. Kijana anakuwa anajiandaa kuchukua nafasi za wazee wao. Unapotakiwa kuchukua nafasi ya mtangulizi wako ni lazima ufatilie kwa umakini wa hali ya juu kuhusu kile ambacho amekifanya mtangulizi wako, itabidi utambue mazuri aliyofanya na namna alivyofanikiwa kufanya hivyo. Utambue makosa aliyofanya na ujifunze namna utakavyofanya ili usirudie makosa aliyofanya. Pamoja na kwamba kwa mtazamo wa kijana kwa haraka haraka akiangalia wazee waliomtangulia anaweza akaona wanakosea karibia kila mahali lakini kama hatakuwa makini kujifunza kupitia kwao anaweza kufanya makosa makubwa kuliko waliyofanya.

4.Kipindi ambacho mabadiliko makubwa hutokea ni kipindi cha UJANA. Hisia na mihemuko huwa huwa juu sana katika kipindi hiki cha ujana, Fikira hubadilika na kufikiri kuwa wao ni bora kuliko wengine. Mabadiliko hayo ikiwa hayataangaliwa kwa umakini yanaweza yakaharibu kesho ya kijana. Mabadiliko hayo yanapotokea ni kiashiria kuwa unatakiwa kujifunza kujitegemea na kujiandaa kubeba majukumu au kuwajibika. Katika kipindi hiki kijana hutakiwi kuufuata mwili, Unatakiwa kutambua na kuzitii hisia zako, LAKINI kila maamuzi utakayofanya yawe yamepita kwenye ubongo na kupimwa kwa uzito wake kama ni muhimu au la.

Nini Cha kufanya katika kipindi hiki cha ujana!?
1. Kila jambo upatalo kulifanya lifanye kwa nguvu zako zote na Akili yako yote.
Ni Ukweli usiopingika kuwa kijana amepewa nguvu na maarifa ya kila namna, Nguvu hizo ulizonazo kijana hazitadumu milele, ikiwa hautazitumia kitafika kipindi ambapo zitaondoka na wala hutaweza tena kufanya yale ambayo ungeyeweza kuyafanya. Kwa yule ambaye ataamua kuzitumia nguvu zake za ujanani kwa hekima na uadilifu atakapifikia kipindi cha uzeeni bado ataonekana ana nguvu bado kwani nguvu alizozitumia kipindi cha ujanani zitafanya kazi badala take naye ataona matunda ya taabu yake.

2. Tafuta maarifa. Katika kipindi cha ujana ndio kipindi cha kutafuta maarifa. Ni Ukweli usiopingika kuwa maarifa hupatikana katika KUSOMA. Jijengee tabia ya kujisomea Vitabu, magazeti na makala mbalimbali. Usipoteze muda wako kwa kuchart, kubishana kuhusu mbambo yasiyo na msingi wala kupiga soga za kipuuzi hakuna chochota unachojifunza zaidi ya kuujaza ubongo wako mataputapu tu.
>KAMA vijana wangewejeza muda wao mwingi katika kusoma akili zao zingebadilika sana na wasingetumia nguvu nyingi sana katika kuyasaka mafanikio. "Boresha ubongo kuza mafanikio"
> NI UKWELI USIOPINGIKA KUWA mtu anayetumia akili atamtawala mtu anayetumia nguvu ya misuli.
**Narudia tena Wekeza katika kusoma ili uongeze maarifa.***
Ukiona mtu anaweza kusimama mbele za watu na kuongea kitu cha kueleweka au kutoa hotuba yenye kugusa hisia za watu, Huyo mtu ni MSOMAJI MZURI.

3. Tambua Umuhimu wa Muda.
Muda ni Rasilimali muhimu sana katika maisha hii ni kwa sababu muda ukishapotea haurudi tena. Mtu mwenye mafanikio ni lazima awe na ufahamu umuhimu wa rasilimali muda. Unapokuwa unampa mtu muda wako tambua kuwa unampa sehemu yako ya maisha ambayo hutaweza kuirudisha tena. "Hivyo basi kabla hujampatia muda wako tambua kuwa unajitoa muhanga kwa ajili yake"
>Ni ukweli usiopingika kuwa ukiwa na uwezo wa kupanga muda ni unakuwa na uwezo wa kupanga maisha. "Time managemante is life management". Kucheza na muda ni kucheza na maisha yako binafsi.

Ndugu msomaji huu ndio mwisho wa kiunga chetu cha UKWELI USIOPINGIKA, Natumaini umejifunza kitu katija mwendelezo wa makala 10 ambazo zilikuwa zinakufikia kila mwishoni mwa juma kupitia blog yako bora kabisa ya NGWAKWA UFANISI, Na Facebook page ya LIVELONGER.

Nikukaribishe tena katika kiunga kinachofuata cha ambacho kitaenda kwa jina la TAA 7 ZA MJASIRIAMALI. Hii si ya kukosa SUBSCRIBE sasa katika blog yangu ya NGWAKWA UFANISI Ili uweze kupata makala hizo kila mwisho wa week.

    KARIBU SANA
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com

"Live an inspired life"