TAA ZA MJASIRIAMALI
SEHEMU YA 4: KAULI MBIU YA MAISHA (Mission statement).
Kauli mbiu ni Ni muhtasari rasmi wa malengo na vipaumbele vya mtu binafsi, kampuni au taasisi.
Kwa maneno mengine unaweza kusema; Kauli mbiu ni Nakala ya maandishi yenye malengo na shabaha ya Taasisi au mtu binafsi ambayo mara nyingi hubaki bila kubadilika.
> Pamoja na kwamba tunakuwa hatuna uhakika wa maisha yetu kwamba yatakoma lini bado ni muhimu sana kuwa na kauli mbiu binafsi, kauli mbiu katika biashara zetu na kauli mbiu katika taasisi zetu. Kauli mbiu itakuwezesha kuwa na msimamo katika vitu unavyovifanya.
SIFA KUU ZA KAULI MBIU (MISSION STATEMENT).
1. Inafanya kazi kama chujio linalotenganisha vitu ambavyo ni muhimu na vile ambavyo siyo muhimu.
2. Huonesha walengwa wa huduma unayoitoa.
3. Kuonesha mwelekeo wa mtu taasisi au kampuni husika.
> Kuna tofauti gani kati ya kauli mbiu na maono (vision)?
Kauli mbiu ni tofauti na naono (vision) kwa sababu maono ni kisababishi (cause) wakati kaulimbiu ni matokeo. Kaulimbiu ni kitu unachotaka kukitimiza wakati maono ni namna utakavyokifikia au kukikamilisha.
Kauli mbiu sio kitu kinachofanana katika kila hali bali hutofautiana kulingana na mlengwa, Kuna kauli mbiu ya mtu binafsi, kauli mbiu ya kibiashara au kaulimbiu ya Asasi au taasisi n.k
KAULI MBIU YA MTU BINAFSI.
Huu ni muhtasari wa Imani, malengo na matamanio, shabaha au vitu ambavyo mtu amelenga kuvitimiza katika siku za maisha yake. Inahusisha vipaumbele ambavyo mtu amejiwekea katika maisha na kwamba anataka afanye nini ili awe mtu anayetaka kuwa. Ni njia ya kuweka shabaha, nguvu, vitendo, tabia na maamuzi binafsi juu ya vitu ambavyo ni vya muhimu kwa mtu mwenyewe.
Kauli mbiu binafsi kwa namna nyingine tunaweza kusema kuwa ni maandishi au kiapo ambacho mtu hukiweka kabla ya kuanza kazi au hatua fulani ya maisha. Mfano: mtu anaweza kujiwekea kiapo fulani pindi anapoanza masono ya chuo kikuu na kadhalika.
UMUHIMU WA KAULI MBIU BINAFSI.
1. Inakupa mwelekeo.
Kauli mbiu hukusaidia kuzielekeza shughuli zako katika njia iliyo sahihi, ina umuhimu mkubwa katika kusaidia kufanya maamuzi sahihi katika shughuli zako ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwako. Bila kuwa na kauli mbiu biashara zako zinaweza kukosa mwelekeo pale utakapokutana na changamoto.
2. Husaidia kuwa na Sababu mahususi.
Kwenye kauli mbiu ni lazima kuwepo kidokezo cha sababu kwa nini unataka kufika unapotamani kufika? Wewe na hata wadau wengine wa biashara yako wanahitaji kufahamu kama biashara yako inafanya uchaguzi sahihi au La! Na ni kwa jinsi gani unatimiza malengo yako. Hii itasaidia kuondoa sintofahamu zinazoweza kujitokeza kwa wadau kuhusu biashara yako.
3. Kauli mbia inaweza kusimama kama motisha kwa wafanyakazi wa kampuni ama taasisi. Husaidia wafanyakazi wote kufanya kazi kwa nia na lengo moja tu ambalo lina manufaa kwa taasisi na wao binafsi.
4. Hizi kwa kifupi ni kanuni zinazokuongoza wapi unapokwenda na unataka uwe sehemu gani katika mwisho wa Maisha yako.
5. Kauli mbiu husaidia kuonesha thamani yako. ( Uthamani wako). Huu ndio mwanga wako binafsi unaokuwezesha kubaki katika mstari wa ndoto yako. Kila baada ya Mwezi mmoja ni vizuri ukakaa chini kwa masaa machache na kuandika kanuni tano au kumi ambazo zitaongoza maisha yako na kukufanya ubaki katika shabaha yako muda wote. Mfano: Nitajituma kusaidia wengine, aNitakuwa raia ninayejari wengine, Nitakuwa tajiri mkubwa, Nitakuwa kiongozi mkubwa n.k.
KAULI MBIU YA KISIASA.
Kauli mbiu ya kibiashara ni lazima iongoze nyendo zote za taasisi au kampuni, ielezee malengo makuu, kuelekeza njia na kuongoza taasisi katika kufanya maamuzi.
Huu ni muhimili ambamo kutoka humo mipango mikakati ya kampuni inaweza kutolewa. Kwa ufupi haya ni malengo ambayo kampuni husika inapanga kuifanya kwa ulimwengu.
FEATURES OF COMMERCIAL MOSSION STATEMENT.
SIFA ZA KAULIMBIU YA KIBIASHARA
> Kwa mjibu wa Chris Bart kauli mbiu ya kibiashara ina sehemu kubwa tatu.
1. Soko kuu: Elezea wateja wako wakuu, ieleze kwa ujumla kama inawezekana.
2.Mchango wako: Eleza, Ni bidhaa gani au huduma ambazo unahitaji kuwapa wateja wako.
3. Upekee wa bidhaa: Ni kitu gani ambacho kinaifanya bidhaa yako kuwa ya kipekee ili wateja wako waipende na kuichagua.?
What to do with your mission statement?
Kitu gani kifanyike katika kauli mbiu yako.?
Vyovyote vile kauli mbiu yako itakavyokua., ipitie na kuirudia mara kwa mara. Kila unapohisi kitu fulani kinapojaribu kukuvuta kando ya ndoto zako, jitahidi sana kurudi katika njia sahihi haraka na ujihakikishie kabisa kuwa umerudia katika njia yako uliyoichagua.
MFANO:
KAULI MBIU YANGU: KUHAMASISHA NA KUAMSHA ARI YA KUJITAMBUA NA KUJITAWALA NDANI YA VIJANA KWA MAISHA BORA YA SASA NA YA BAADAYE.
> Rafiki yangu ninakusihi, tengenesa kauli mbia yako sasa! Haijarishi upo katika hali gani, haijalishi upo mazingira gani! Tafadhali tengeneza saasa.Create your own mission statement now. Please do it now, whatever you are, wherever you are, do it.
If you can't fly, run! If you can't run walk! , walk! If you can't walk craw! Do whatever you can but keep moving.
" Live inspired life "
Robert Lucas
+255764075392 (whatsapp)
+255713056903
+255625605820
lucastrngwakwa@gmail.com