Ticker

6/recent/ticker-posts

TAA ZA MJASIRIAMALI, SEHEMU YA 3: CURRICULUM VITAE - CV

TAA ZA MJASIRIAMALI
SEHEMU YA 3: WASIFU BINAFSI( PERSONAL PROFILE)
Hiki ni kitu ambacho kinakutambulisha kuwa wewe ni nani na una sifa gani. Hii inaweza kuhusisha maandishi, Picha na video fupi (clips). Wasifu mzuri ni Muhimi sana kwa kila mtu ambaye anahitaji kuwa mjasiriamali mkubwa. Kwa sababu wasifu unaweza kumtangaza mjasiriamali na bidhaa au huduma anazotoa. Pia wasifu unaweza kumsaidia mtu kutengeneza mtaji kabla ya kuanzisha biashara anayoitaka. Mtaji huu mtu anaweza kuupata kwa kutumia taaluma yake kwa kuajiriwa kwa muda katika taasisi fulani.
> Hivyo basi kutokana na kutambua umuhimu wa chanzo hiki cha mtaji nimeamua kukueleza namna ambavyo utaweza kuandika wasifu wa kitaaluma (ACCADEMIC CURRICULUM VITAE - CV), Kipo kitu kimoja kinanishangaza sana zipo taasisi na makampuni mengi sana Yanatafuta watu wa kuwaajiri wakati huo huo kuna watu wengi sana wanatafuta kazi, tatizo liko wapi? Kwa nini haya makampuni yasiwaajiri hao watu? Sababu kuu ni CV!!! Makampuni mengi hasa ya kigeni yanapotafuta watu wa kuajili na wanapoangalia CV zao kwa kweli hayavutiwi kabisa kuwaajiri!. Unakuta mtu amefanya kazi nyingi, ana ujuzi Mwingi, maarifa mengi na Ana uzoefu Mwingi lakini hajui namna ya kuyaweka madini hayo katika karatasi ili kuwavutia waajiri.
Rafiki hakuna njia nyingine ni lazima tujifunze namna ya kuandaa CV kwa usahihi.

NAMNA YA KUANDIKA CV (CURRICULUM VITAE).
Wasifu au CV ni inatokana na neno la kilatini lenye maana ya "kozi ya maisha"  Wasifu au Curriculum Vitae (CV)  Ni nakala fupi ya maandishi yenye vitu muhimu vinavyoelezea kwa ufupi kuhusu maisha yako yaliyopita, taaluma yako ya sasa na uzoefu ulionao katika sehemu fulani ya maisha yako. Lengo kuu la nakala hii ya maandishi Ni kuonesha kwamba unayo maarifa au ujuzi wa kufanya Kazi ambayo unaomba kuifanya. Kwa Maelezo mengine tunaweza kusema wasifu Ni namna ya kuuza kipaji, upeo, maarifa na ujuzi wako.

VITU MUHIMU VINAVYOHITAJIKA KWENYE WASIFU.
>Wasifu au CV kwa sehemu kubwa inahusisha taarifa zako binafsi, Elimu yako, vigezo vyako ulivyo navyo, uzoefu wa kazi, vitu unavyopendelea, mafanikio yako, ujuzi wako na marejereo ya taarifa zako (Wapi unaweza kupata ukweli wa taarifa zako).
> Kitu cha kwanza kabisa cha kuangalia wakati unaandaa CV ni aina ya kazi unayotaka kuomba kufanya. Hangalia malengo makuu ya taasisi au kampuni unayohitaji kuomba kufanya kazi na kisha Angalia namna ambavyo wasifu wako au CV yako itakavyosaidia taasisi husika kufikia malengo yake.
>Kitu cha pili cha kuzingatia ni kwamba Andika wasifu kwa mfumo unaoendana na wakati (mfumo wa kisasa), ingawa hakuna mfumo maalumu wa uandishi wa wasifu (CV).

> Kitu kingine cha muhimu kstika CV ni Orodha ya kazi ulizowahi kufanya, unazofanya na uzoefu mbalimbali ulio nao katika kazi.

> Pia Kitu cha muhimu unachotakiwa kukizingatia ni Orodha ya vitu ambavo unapendea kuvifanya (Hobbies and interests). Hapa unaweza kuhusisha vitu vyote ambavyo wewe binafsi unajisikia amaniamani kabisa kuvifanya kwa Muda wako. Cha muhimu zaidi viwe na uwezo wa kuonesha kitu ambacho mwajiri wako atanufaika ikiwa atakuajili. Kwa mfano kama wewe ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu, mwajiri wako anaweza kukuajili kwa sababu anafahamu kuwa unaweza kuunda timu na wafanyakazi wenzako na hivyo kusaidia kutangaza taasisi husika kupitia michezo. Mfano mwingine: unapokuwa unaomba kazi katika nyumba ya uchapaji, Ni vizuri ukaonesha kuwa wewe ni mpenzi wa kusoma.

> Andika ujuzi ulio nao! Ujuzi huo unaweza kuhusisha ujuzi wa kompyuta ( MS word, microsoft Powerpoint, microsoft publisher, window and computer programme, skills in design etc). Hii itakupatia uwanja mpana zaidi kutegemea na kampuni husika! Kumbuka mwajili huhitaji mfanyakazi kilaka, mwenye ujuzi mwingi na Anayeweza kufanya kazi tofauti tofati kuliko mwenye ujuzi wa kazi moja tu. Bila kusahau lugha unayoweza kuiandika na kuiongea vizuri na uzoefu wa lugha hiyo.

SEHEMU KUU ZA CV.
Kabla hatujaangalia sehemu kuu za CV ebu tuangalie kitu ambacho ni cha kwanza kabla ya yote :-
Chagua mfumo au format ya Cv yako. Kama ambavyo nimeeleza katika sehemu ya kwanza hapo juu ni kwamba ipo mifumo mingi ya uandishi wa Cv hivyo unatakiwa kuchagua mfumo ambao ni wakisasa na unaoendana na mahitji ya kazi unayotaka kuomba!
Mfano: unahitaji kuweka kila kipengele katika kibox maalumu!? Au anataka kuorodhosha tu taarifa zako? N.k. Ila tu cha kuzingatia ni kwamba Cv yako isiwe ndefu sana.

Sehemu ya 1: TAARIFA BINAFSI
Hii huwa juu kabisa katika ukurasa wa kwanza. Sehemu hii inakuwa na Jina lako, Anwani yako, Namba yako ya simu, na Anwani ya barua Pepe (E-mail). Ni vizuri jina likawa na maandishi makubwa kuliko mengine ili liweze kuonekana kiurahisi. Kwa mfumo wa kisasa jina linaweza kuwekwa katikati mwa karatasi wakati anwani zote na namba za simu zikiwa mkono wa kushoto.

Sehemu ya 2: WASIFU BINAFSI.
Kipengele hiki siyo cha lazima na wakati mwingine kinaweza kuunganishwa katika sehemu ya kwanza. Hapa ndipo unapojaribu kufunia taarifa zako zaidi, wewe ni nani na unahitaji kufanya nini. Hapa ndipo unaandika mtazamo na matarajio au kaulimbiu yako ya kimaisha (Mission statement), Hapa ndipo unapoweza kuonesha ubora ulionao.

Sehemu ya 3: HISTORIA YA KIELIMU.
Hiki kipengele kinaonesha historia ya Elimu yako. Andika Historia ya Elimu yako kuanzia juu kwenda chini. Mfano: anza na digrii kama umebahatika kuwa nayo na kushuka chini.

Sehemu ya 4: UJUZI NA MAFANIKIO.
Hapa unahitajika kuandika vitu ulivyofanikiwa kuvifanya katika kazi zako zilizo pita, na maarafa ambayo umeyapata kupitia kazi hizo. Katika sehemu hii ni vizuri ukaandika kama kuna majarida ama kazi zozote ulizoziandika. Katika sehemu hii ni muhimu kuandika kama kuna cheti chochote cha ujuzi ulichopata.

Sehemu ya 5: VITU UNAVYOVIPENDA.
> Hapa utaandika vitu vichache muhimu unavyovipenda ambavyo unahisi vitsaidia kufanya ufanikiwe katika kazi utakayoomba kama nilivyoeleza hapo juu.

Sehemu ya 6: TAARIFA NYINGINEZO.
Kama kuna taarifa za ziada unahitaji kuziweka katika CV yako hapa ndipo Mahali pake. Sehemu hii unaweza kuandika hata kipindi ambacho uliacha kazi kwa ajili labda kuhudumia watoto washio mazingira magumu n.k.

Sehemu ya 7: WADHAMINI.
Hawa ni watu ambao umefanya nao kazi kama vile walimu wako wa chuo, Waajili wako wa zamani n.k. ambao unahisi walikuwa wanatambua juhudi na mchango wako katika kazi. Kwa hiyo mwajili wako mpya Anaweza kuwasiliana na watu hawa ili kupata taarifa zaidi kuhusu wewe pia. Ni viziri zaidi kabla hujamfanya mtu kuwa mdhamini wako ukawasiliana naye ili kupata ukubali wake na kama bado anakukumbuka na kujiridhisha kwamba bado anatumia mawasiliano hayo hayo. Utaweka namba zao za simu Anuani zao na Barua pepe zao.


MWISHO:
Pitia kile ulichoandika ili kujiridhisha na usahihi wa taarifa ulizoandika, Rekebisha makosa yote ya kiuandishi. Hakikisha kama majina Ya watu na Makampuni umeyaandika kwa usahihi. CV nzuri ni ile ambayo ni fupi na yenye taarifa muhimu tu. Waajiri wengi huvutiwa na CV zenye vitu vingi tofauti tofauti kuliko zilizorudia vitu vichache mara nyingi. Rudia tena na tena ili kujua ni kitu gani unaweza kukiondoa na kipi unaweza kukiongeza kutegemea na kampuni unayoomba.

Kwa sample za CV unaweza kuwasiliana nami nitakusaidia.

LUCAS ROBERT
+255764075392 (WhatsApp)
+255625605820
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com.

"Live an inspired  Life"