TAA ZA MJASIRIAMALI.
SEHEMU YA 5: KADI YA BIASHARA
Kadi ya biashara ni Kipande kidogo cha karatasi chenye mawasiliano muhimu kati ya mjasiriamali au mfanya biashara na mteja wake/mshiriki wa huduma yake. Kadi ya biashara pia huonesha taarifa muhimu kuhusu huduma na biashara inayotolewa.
VITU MUHIMU KWENYE KADI YA BIASHARA (Bussiness Card).
Kadi ya biashara inaonyesha taarifa muhimu za mawasiliano kama namba ya simu, barua pepe, anuani ya posta, mitandao ya kijamii, tovuti, anuani ya mahala pamoja na huduma/ bidhaa zinazotolewa na mjasiriamali husika. Kadi ya biashara inaweza kuonesha pia ari au kauli mbiu ya mfanya biashara huyo au mtoa huduma na huduma zake.
Hivyo kadi ya biashara sio kwa ajiri ya mawasiliano tu, hutumika kuonyesha/kutambulisha bidhaa/ huduma zinazotolewa na mhusika.
UMUHIMU WA KADI YA BIASHARA KWA MJASRIAMALI.
1. Kumtambulisha mfanyabiashara kwa mteja wake.
Kitu cha muhimu ambacho wafanyabiashara wengi wanakipuuza na kutambulika kwa wateja wao, na badala yake wanataka kwanza bidhaa ndo itambulike kwanza kwa wateja ndipo wao wafuate hilo ni kosa kubwa. Mteja anahitaji sana kumfahamu yule anayetoa huduma au bidhaa na akishamtambua na kumuamini ndipo ataweza kuwa mteja wa kudumu wa bidhaa yako. Hivyo basi wewe kama mjasiriamali ni muhimu sana ukawa na kadi ya biashara inayokutangaza vizuri na kukutambulisha kwa mteja.
2. Huonesha ubobevu, umahiri na uzoefu wa mtu katika biashara husika.
Mtu mwenye kadi ya biashara ataonekana kuwa anao uzoefu katika biadhara hiyo ndiyo maana amejiamini hata akachukua muda wake na gharama zake kutengeneza kadi ya biadhara na hivyo huyu ataweza kuaminiwa kirahisi sana na mteja wake kiliko ambaye hana kadi ya biashara.
3. Humfanya mteja ajisikie kujaliwa na kuthaminiwa.
Mteja anapopewa kadi ya biashara huiona kama zawadi kwake, Na hivyo ipo siku atakupigia kuulizia huduma unayotoa kama njia ya kutoa shukrani kwa zawadi uliyompa. Pia mteja anapopewa kadi ya biashara atajisikia kuheshimiwa kwa kutokupotezewa muda wa kuandikiwa namba kwenye makaratasi au kuandikiwa sehemu yoyote. Kwa kadi ya biashara huonesha heshima kwa mteja.
4. Hutoa taarifa muhimu kuhusu huduma au bidhaa yako.
Kadi ya biashara ni mihimu ikadokeza walau kidogo tu umuhimu wa huduma unayotoa. Mteja akiona umuhimu wa bidhaa unayotoa atahamasika kujaribu kutumia huduma yako. Badala ya kukaa chini na kueleza biashara yako kwa kila mtu, kupitia kadi alya biashara utaweza kumpatia ujumbe ulioandikwa vizuri na kwa ufipi kila mtu ambaye utahisi unauhitaji wa huduma unayotoa.
5. Huchora picha ama Taswira ya Biashara au huduma husika.
Kutokana na taatifa zitakazokuwepo katika kadi ya biashara ndizo ambazo zitaonesha ukomavu au uchanga wa huduma inayotolewa. Pamoja na kwamba kutengeneza kadi ya biashara haichukui muda na pesa nyingi, bado mtu ambaye atakuwa na kadi ya biashara ataonekana kukomaa kifedha kitu ambacho kitamfanya mteja asione kwamba unakula njama ili upate kumchuna pesa zake bure. Hivyo hasi ni muhimu kutengeneza kadi ya biashara inayochora biashara yako vizuri ili mteja avutiwe nayo.
> Kadi ya biashara inaonesha namna gani ulivyo nadhifu, Namna gani usivyopenda michezo na kupoteza muda, Namna gani unavyojari namna gani unaheshima kwa wateja wako, Namna gani unapenda kwa karibu na wateja wako na ulivyo tayari kutumika. Ujasiriamali ni kitendo cha kujitoa kuwatumikia watu wanaohitaji huduma yako, mjasiriamali ni mtu anayehudumia jamii!!,
Kwa kuyatambua hayo, Kwa mjasiriamali yoyote ambaye anampango wa kupanua na kukuza biashara yake hana budi kuwa na kadi ya biashara kwa ajili ya faida yake mwenyewe na mteja wake pia.
Kadi ya biashara (business card) Ni Tangazo, Ni zawadi, ni kivutio na mawasiliano kati ya mfanya biashara au mtoa huduma na mteja wake.
LUCAS ROBERT
+255764075392 (WhatsApp)
+255625605820 ( call & sms)
*"Live An Inspired Life"*