TABIA 5 ZA WATU WENYE MAFANIKIO ZAIDI.
Tunafahamu kuwa tabua zinaweza kuchochea au kurudisha nyuma maendeleo yako katika Maisha.
Tabia mbaya zinaweza kukua na kuwa mfumo wa maisha utakaokufanya ushindwe kufanya vitu vitakavyokuletea maendeleo, Lakini tabia nzuri itakufanya uwe na maisha yaliyojaa vitendo na mawazo chanya na Yenye utoshelevu.
> Kama utawaangalia watu ambao wanaheshimika, watu ambao wana mafanikio, utaona kwamba huwa wanatumia siku yao kufanya vitu vitakavyowasaidia kufikia malengo yao. Hii haimanishi kuwa wao ni watu wakamilifu, maana hakuna aliye mkamilifu, Lakini pamoja na uwepo wa vitu ambavyo siyo vikamilifu katika maisha yao bado huendelea kufanya vitu ambavyo vina matokeo chanya katika maisha. Na hii huanza na tabia zao za kila siku.
>Naam, Hata kama tungejifunza tabia hizi za kimafanikio bado itakuwa haina maana kama hatutazifanya au kuzitekeleza.
>Zifuatazo ni tabia tano za kila siku za watu wenye mafanikio zaidi, ambazo unaweza kuziiga ili kutengeneza maisha ambayo unayahitaji:-
1. Watu wenye mafanikio hupanga shughuli za kesho yake kabla ya kulala.
Ni rahisi sana kutoka nje ya njia na kupoteza mwelekeo wa mafanikio kama huna mipango.
> Bila kupanga namna siku yako itakavyokuwa, utaamka bila kujua vitu gani unahitaji kuvitimiza kwa siku hiyo. Watu wenye mafanikio hutumia muda kidogo wakati wa usiku kuangalia vitu vinavyohusu mafanikio yao na kuweka malengo yao katika siku inayofuata. Na baada ya kuamka ni kuanza kutekeleza tu yale waliyopanga kuyatekeleza.
Inaweza kutokea kwamba Orodha uliyoipanga isitekelezeke kama ilivyopangwa lakini kwa kuwa na mipango unaweza ukarekebisha haraka na ukafanikisha lengo la siku hiyo bila kuchoka.
2. Watu wenye mafanikio husoma vitabu vingi vya Hamasa.
Usomaji ni jambo muhimu sana katika mafanikio, Katika vitabu kuna maarifa mbalimbali. Elon Musk, mzaliwa wa Afrika kusini, mjasiriamali, Na mgunduzi wa vitu mbalimbali, ikiwemo mfumo wa malipo wa mtandaoni (paypal), Na magari ya kuchaji kwa umeme, Ambaye alichukua uraia malekani mwaka 2002, Na mshauri binafsi wa Raisi wa sasa wa Marekani Donald Trump, Yeye kwa sasa hutumia angalau masaa 4 kusoma vitabu. Angalia mafanikio yake kama nilivyoelezea hapo japo kwa ufupi sana.
Watanzania wengi hasa vijana hatuna muda wa kusoma vitabu, lakini tuna muda wa kuvinjari kwenye mitandao ya kijamii.
Mtu mmoja alisema "Ukitaka kukificha kitu mtanzania asikione kabisa kifiche kwenye maandishi/kitabu" Hatakiona kirahisi.
Ndiyo maana hatufanikiwi na badala yake tunakalia kulalamika tu. Nani atakwajili kwenye kampuni yake mtu ambaye hupendi kusoma ili kujiongezea maarifa, si utaua kampuni yako kwa kufanya kazi kwa mazoea bila kuwa na maarifa mapya (up to date knowledge?)
Zama katika vitabu uone kama akili yako haijabadilika na kuacha kulalamika kuhusu maisha.
> Hakuna muda maalumu kwa ajili ya kusoma lakini kujenga tabia ya kusoma inasaidia kuwa na maarifa na kusaidia katika safari yako ya mafanikio.
> Maisha hayawezi kubadilika kwa kukaa sehemu moja tu, Bali maisha hubadilika kwa kuamua kutoka sehemu ulipo kiakili na kwensa sehemu nyingine. Kitabu kinaweza kukutoa sehemu ulipo na kukupeleka sehemu nyingine
3. Kipaumbele cha mtu mwenye mafanikio ni Afya yake.
Kile unachokula na namna unavyofanya mazoezi huathiri karibia kila sehemu ya maisha yako.
> Watu wenye mafanikia hutumia muda wa mazoezi kama muda wa kujipanga upya. Na hufanya uchaguzi wa vyakula kwa usahihi, huchagua chakula ambacho kitawapa nguvu ya kukamilisha yale waliyopanga kukamilisha.
** Huwa unakula nini wakati wa jioni? Je kufanya mazoezi ni sehemu ya ratiba yako? >>>>>Fanya uchaguzi sahihi..
4. Watu wenye mafanikio huwa hawasumbuliwi na kile ambacho wengine wanafanya.
Safari ya mafanikio ya mtu fulani inaweza kuwa ni ya kuhamasisha sana, unaweza kujifunza vingi, wapi walikosea, wapi walifanikiwa, nini cha kufanya na nini si cha kufanya. Lakini kama utaanza kulinganisha mafanikio yako na ya kwao, badala ya kutumia mafanikio yao kama hamasa, utawaonea wivu, utajipa msongo wa mawazo na unaweza hata kujishusha thamani.
Watu wenye mafanikio wqnatambua kuwa safari yao ni ya pekee, haiwezi kulinganishwa na ya mtu mwingine. Hivyo chukua tahadhali usije ukajikuta unajilinganisha na wengine. >>>>"Baki katika malengo yako"
5. Watu wenye mafanikio huona kila siku kama ndiyo siku ya mwisho.
Maisha yana shughuli nyingi za kufanya, kuna mambo mengi yanayoharibu, Na hivyo unahitajika kulenga katika maisha yajayo, na ndivyo tunavyofanya. Lakini unapopanga ni muhimu kupanga mipango ya "sasa hivi" - Maisha ni mafupi na haijulikani kwamba yatakoma lini. Watu wenye mafanikio huishi kana kwamba kila siku ndiyo siku yao ya mwisho na hujitahidi kufanya kila linalohitajika kufanyika kwa wakati huo - siyo kwamba hufanya bila utaratibu bali hufanya kwa utaratibu kila linalowezekana, Na wewe unaweza kufanya pia.
> Unapotazama malengo makubwa sana, Unaweza kubabaika na vitu vidogo ambavyo unavifanya kwa sasa. Lakini ka kila siku utaamka na malengo ya kujenga tabia njema, utakuwa unajipatia nafasi nzuri ya mafanikio.
*** Hivyo basi tumia hizo tabia tano za watu waliofanikiwa kama sehemu yako ya kuanzia katika safari yako ya mafanikio.
LUCAS ROBERT
+255764075392
lucastrngwakwa@gmail.com
*"Live an inspired Life"*


