NAMNA YA KUISHI KWA MUDA ULIOPO.
Kuishi kulingana na muda humaanisha kuwa uelewa wako wote unakuwa umeelekezwa sehemu ulipo na kwa wa wakati huo tu, Hautishiki na mambo yajayo ama kuwaza sana mambo yaliyopita. Kuishi kwa wakati pia humaanisha kuwa mahali ambapo maisha yanaendelea. Mambo yajayo au yaliyopita ni dhahania tu, ila kiuhalisia hayapo. Kuna msemo usemao "Kesho haitafika kamwe" Kesho ni fikra tu, Kesho ipo kwenye kona fulani inasubiri kuja, lakini ukichungulia kwenye kona hapo utaona kivuli tu na hauhitaji mwanga ili umulike kuondoa kivuli cha kesho.
"Siri ya kuwa na Afya njema ya Kiakili na kimwili siyo kujilaumu kwa yale yaliyopita, Kuwa na wasiwasi kuhusu yaliyopiata bali ni kuishi kulingana na maisha yaliyopo""
> Moja ya Matokeo mazuri sana ya kurahisisha maisha yetu ni kukubaliana na maisha ya wakati uliopo au maisha yaliyopo.
> Kuendelea kuishi katika maisha taliyopita au kuishi maisha ambayo hujayafikia haikuzuii kuyafurahia maisha ya leo tu, bali pia hukuzuia kuishi maisha yako halisi..
" Wakati wa muhimu zaidi ni huu ulopo"
> Ikiwa una malengo akilini mwako, Vifuatavyo ni vitu muhimu vinavyoweza kukusaidi kuanza kuishi maisha mazuri leo:-
1. Usimiliki vitu ambavyo si vya muhimu.
> Kuondoa vitu vinavyokukumbusha mambo au maisha ya zamani hutufanya tuwe huru kutoka katika maisha ya zamani na kuanza kuishi kulingana wakati uliopo.
2. Tabasamu.
Kila siku imejaa matazamio mapya yasiyo na mwisho. Ni muhimu kuanza siku yako kwa tabasamu. Tabasamu huonesha ni namna gani ulivyo na nguvu, Unao uwezo wa kusimamia mtazamo wako na hisia zako kila asubuhi, Endelea kuwa mwenye matumaini na matarajio mapya kila asubuhi.
3. Kubaliana na Leo yako.
> Zama katika vitu vya leo, Ingiza vitu vinavyotokea leo, angalia vitu vya leo sikiliza vitu vya leo, Nusa vya leo (kuwa na tarifa za leo), Hisia, machungu na ushindi wako uwe ni wa leo leo.
"Ithamini sana siku yako ya leo kana kwamba hutapata siku nyingine, maana hata hivyo kesho ni fumbo"
4. Samehe maumivu ya zamani.
Kama unaendeleza chuki kwa watu wengine kwa sababu ya maumivu yaliyipita, Amua kusamehe leo na usonge mbele. Madhara yalikuwa kwao waliokuumiza , lakini kuendelea kutunza chuki hiyo inakuathili wewe na maisha yako ya sasa.
"Mzigo wa kutokusamehe na visasi ulivyobeba ndivyo vinavyokuvuta chini usipande juu kwenye mafanikio yako"
5. Penda kazi yako.
> Kama kazi uliyonayo inakufanya uendelee kuwa hai tu ukisubiri juma lingine lije na hatimae mwisho wa mwezi, Ndugu yangu unapoteza 71% ya maisha yako (5 out of 7 days). Hili ni tatizo, na kuna njia mbili za kulitatua:-
1. Tafuta kazi mpya ambayo utaifurahia, kazi ipo hapo nje inakusubiri.
2. Tafuta kitu ambacho unakikubari kulingana na kazi uliyosomea, Taaluma au ujuzi wako wa sasa na uwekeze hapo na kuondokana na mawazo hasi.
6. Kuwa na ndoto za baadaye lakini Fanya kazi kwa bidii leo.
"Kuwa na ndoto kubwa uwezavyo, weka malengo na mipango mizuri ya baadaye". Kumbuka kufanya kazi kwa bidii ndiyo hatua ya kwanza ya kutambua ndoto zako za kesho. "
Usiruhusu ndoto zako za kesho kuathiri maisha yako ya leo".
7. Usiishi kwa yale uliyoyafanya jana.
Kama bado unajilaumu na kuongelea yale uliyoyafanya jana, bila shaka utakuwa hujafanya mengi leo ndiyo maana unakumbuka yaliyopita.
"Fanya mambo mengi leo ili kufunika yale uliyoyafanya jana".
8. Ondoa wasiwasi/Usiogope.
Kama una wasiwasi sana na kesho hutakuwa na uwezo wa kukubaliana na leo yako. Tambua kwamba
"Kesho ni lazima ije haijarishi unaihofia au la"
Katika maisha hofu haijawahi kamilisha chochote kwa mtu yoyote, cha kufanya ni kuelekeza nguvu za akili mahali pengine.
9. Fikiria zaidi njia za utatuzi za zamani zinavyoweza kuwa na matatizo.
Dunia inabadirika kwa haraka sana kiasi kwamba njia za utatuzi wa matatizo za jana hazifa kutatua matatizo ya leo. Usikalie kusema
"mbona ndiyo huwa tunafanya hivyo kila siku". Njia ulizozitumia jsna kutatua tatizo siyo zinazotumika leo na pengine hazifai hata kesho.
10. Pambana na Uraibu (Addictions).
Uraibu hushikiria maisha yako na kukufanya ushindwe kuishi kwa uhuru leo. Tafuta msaada, fuata hatua unazoelekezwa, ili uweze kuondoa athari za uraibu katika naisha yako.
> Tatizo linalowafanya watu wengi washindwa kufanikiwa ni kulazimisha kuyaishi maisha ya jana leo na kukimbilia maisha ambayo bado hujayafikia na oulazimisha kuysishi leo.
"Kitu kitakachokusaidia kufanikiwa kwa haraka ni kufanya vitu kwa wakati"
Waswahili walisema
"Linalowezekana leo lisingoje kesho"
Lucas Robert
lucastrngwakwa@gmail.com
*"Live an inspired Life"