Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHITAJI YA MJASIRIAMALI: ELIMU

HITAJI LA NNE : ELIMU.
Kwa miongo kadhaa kumekuwepo malumbano kuhusu kama wasomi ni watu sahihi kutoa elimu ya Ujasiriamali, Na kama ndiyo Ni vitu gani wanavyotakiwa kuvifundisha?.
Upande mwingine unasema, Mambo ya ujasiriamali yanatakiwa kufundishwa na wajasiriamali wenyewe kupitia kufanikiwa kwao na kushindwa kwao pamoja na kushirikisha wengine uzoefu halisi.
Wengine husema ujasiriamali hauwezi kufundishwa; bali mjasiriamali mwenye mafanikio anazo tabia za asili zilizo ndani yake Na watu wa namna hii wamejaliwa kuweza kuziona fursa na kuzifuata kwa ubunifu na kwa mtazamo mpya kabisa.
> Ukweli ni kwamba unapofikiri kuhusu elimu ya ujasiriamali uatagundua kuwa kuna sehemu inayohusisha vitendo zaidi (practical experiences) ambavyo huhusisha vitu kama vile utafiti wa masoko, mipango biashara na ujuzi wa makubaliano na mauzo. Hata hivyo wakati wa kutoa programu ujasiriamali unatakiwa kwenda zaidi ya hapo na kuangalia namna ya kufundisha kuhoji na tabia za kijasiriamali.

ELIMU AMBAYO MJASIRIAMALI ANAHITAJI
Elimu ya darasani siyo lazima itufanye tuingie katika ujasiriamali wala kuwa matajiri, Badala yake mjasiriamali huwa anahitaji elimu tofauti na hiyo. Elimu anayoihitaji mjasiriamali inaweza kugawanywa katika sehemu tano, Nazo ni kama ifuatavyo:-
1.Elimu Kuhusu namna ya kufikiri kama mjasiriamali.
Ukweli ni kwamba wajasiriamali 'hufikiri tofauti' Huwa wanauliza maswali ya kichokozi na Ya kibiashara kwa ubunifu mkubwa.

Saras Sarasvathy katika uchunguzi alioufanya kwa kuwauliza wajasiriama kutoka makundi mbalimbali aligundua kuwa "Wajasiriamali wana mtazamo wa kijasiriamali tofauti na wasimamizi (managers) kwa sababu wanafikiria matokeo: wanaini katika vitu ambavyo bado havijatokea ambavyo vinaweza vikatengenezwa na binadamu kwa namna anavyitaka"
>Kiuhalisia zipo aina mbili za namna ya kufikiri.
a) Kufikiri sababu kabla ya matokeo (Causal thinking)
(b) Kufikiri matokeo kabla ya sababu (effectual thinking)
Mfumo wa Elimu ya kawaida duniani unafundisha wanafunzi kuhusu kufikiri kivisabishi (thinking causally), hufundishwa namna ya kuweka malengo na baada ya hapokutafuta namna na rasirimali za kuweza kufikia malengo kwa ufanisi zaidi. Kwa upande mwingine wale wanaofikiria kimatokeo (wajasiriamali) huanza na namna ya kufikia lengo na baada ya hapo huruhusu mipango kuchipua na baada ya muda kukua kufikia malengo. Kwa mfano, Google haikutokea kama ilivyo sasa, bali ilianza kama mradi mdogo kurahisisha utafutaji kwenye maktaba, ikifuatiwa na ugunduzi mwingine mdogo mdogo ambao ulipelekea mpaka ikawa shughuli ya kibiashara.
>Sarasvathy anaendelea kusema, "Aina ya kufikiri kivisababishi hujihusisha zaidi na mantiki, kiasi kwamba tunaweza kubashili kitakachotokea lakini hatuwezi kukithibiti, Ndiyo maana wasomi hutengeneza vifaa vitakavyowawezesha kugunfua kitakachotokea. Ingawa hata Kufikiti komatokeo pia kumejikita katika mantiki, Lakini hapa hakuna haja ya kutabiri nini kitakachotokea kwa sababu kipo mikononi mwetu" Kwa kusema hivyo majisiriamali huwa anafikiria kubadili hali ya baadaye kuwa namna atakavyo kwa sababu huamini ipo mkononi mwake. "Kesho ipo mkononi mwako.

2.Elimu ya ujasiriamali hufundisha kuwa na mtazamo mpana.
>Elimu ya kawaida duniani humfundisha mwanafunzi kufuata maelekezo tu tofauti na elimu ya kijasiriamali ambayo humlazimu mwanafunzi kufanya vitu kwa mtazamo wake mwenyewe kama alivyoelewa. Katika shule za kawaida wanafunzi hutuzwa kwa kuwa na uwa kufananisha kile wanachofundishwa lakini kwenye ujasiriamali mtu hutunukiwa tuzo kutokana na uwezo wake wa kutumia maarifa ya Awali kupata maarifa zaidi.

3.Elimu kuhusu Maarifa na ubunifu.
Mjasiriamali hajifunzi maarifa na ubunifu kwa kukaa darasani bali ni kwa uzoefu na Kufikiri kwa ubunifu mkubwa. Kwa mjibu wa mwanafalisafa wa kiingereza Ken Robinson Anasema "Tunajifunza kuwa wabunifu na wajasiriamali kwa kuchunguza, maswali ya kujihoji, kujenga taswira pamoja na kutengeneza Taarifa sahihi. Katika shule za kawaida huwa tunafundiswa kufanya kama wengine wanavyofanya".
> Ukweli ni kwamba wajasiriamali wagunduzi na wabunifu kama vili Larry page & Sergei Brin - Waanzilishi wa google,
Will Wright - mgunduzi wa michezo ya video (videogame).
Jimmy wales - Mgunduzi wa wikipedia na wengine walianzia Elimu zao kwenye mfumo wa Shule za Montessori ambapo walijifunza kufuata ubunifu wao na kufikiri tofauti na wengune. Katika kitabu kinachoitwa INNOVETOR'S DNA , Hal Gregersen, Mtugenzi wa MIT Leadership Centre, Prof. Jeff Dyer,  “Wajasiriamali wenye uvumbuzi wa hali ya juu walipata bahati ya kukulia katika mazingira ambapo ubunifu ulikuwa ukihimizwa sana. Hujari kufanya majaribio na kufanya ufuatiliaji na uchunguzi". Elimu hii ndiyo ambayo kila mjasiriamali, Elimu kuhusu ubunifu, Elimu juu ya kufanya majaribio na kufuatilia matokeo ya kile ambacho umejaribu, hii itakusaifia kutambua madhaifu na makosa katika kile ulichokuwa unafanya na hivyo kurekebisha na kusonga mbele.

4. Elimu kuhusu Tabia za mjasiriamali.
Elimu ya kijasiriamali ni ile ambayo huhamasisha kujifunza tabia za wajasiriamali na kuwaweka katika mazingira ambayo huwapatia mawazo ambayo huwafanya wafikirie tofauti na kuwa na tabia tofauti.
> "Hapa majasiriamali hutakiwa kujikubali kama alivyo na kukubaliana na utofauti kati yake na wengine, Na inapobidi mjasiriamali hulazimika kutengeneza njia itakayomfanya kuwa na tabia ya kipekee".

5. Elimu kuhusu changamoto.
Mjasiriamali hufundisha namna ya kukabili changamoto na kubwa zaidi na namna ya kuziona changamoto kama fursa. Mjasiriamali huwa hakatishwi tamaa na changamoto bali huweza kuona matokeo ambayo atayapata baada ya kuvuka changamoto hizo.

Elimu tunazojifunza katika shule za kawàida hazitufanyi kuwa wajasiriamali au kuwa matajiri, Bali hutufundisha tu kutafuta maarifa kutoka kwa wajasiriamali wenyewe. Mwalimu wa kawaida hawezi kufundisha Elimu ya kijasiriamali wakati yeye siyo mjasiriamali, Mtu sahihi kufundisha elimu ya ujasiriamali ni mjasiriamali mwenyewe hii ni kutokana sababu kwamba Elimu hii huhitaji vitendo zaidi kuliko na nadharia. Kupitia uzoefu wa mfundishaji mwenyewe na mazingira husika mjasiriamali mwanafunzi atajifunza mengi na kutafuta njia yake binafsi kufikia Lengo.
> Mjasiriamali haridhiki na maarifa au Elimu aliyonayo bali anayo kiu ya kutafuta maarifa zaidi kila kunapokucha. Hujibidisha katika kutafuta kitu kipya ambacho kinaendana na wakati na mazingira.
*Kumbuka mazingira hubadilika hivyo, Hivyo hata ujuzi katika ujasiriamali ni lazima vibadilike kuendana na mazingira.

Kitu cha muhimu zaidi kwa mjasiriamali ni kusoma mabadiliko kwa haraka na kufanya kulingana na uhalisia.
         "SI KILA ELIMU ITAKUFIKISHA UENDAKO, TAFUTA ELIMU SAHIHI"

Ni mimi
LUCAS ROBERT
+255764075392
lucastrngwakwa@gmail.com

*Live an Inspired Life*