Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUWA WA PEKEE KAMA ULIVYOZALIWA UWE

JINSI YA KUWA WA PEKEE KAMA ULIVYOZALIWA UWE. 
Kazi ngumu ambayo kila mmoja Anayehitaji kufanikiwa anayo ni kuwa wa pekee katika Ulimwengu Unaokulazimisha kufanana na wengine. Mafanikio ya kweli hayatapatikana mpaka pale utakapofanikiwa kuwa wa pekee tofauti na wengine na kuweza kufanya kile ambacho walio wengi au mtu mwingine yoyote hawezi kukifanya. 

>Victor E.Frankl alisema "Kila mtu anayao kazi maalumu au lengo maalumu katika maisha; kila mtu lazima achukue wajibu mgumu ambao unahitajika kukamilishwa. Nafasi yake haitaweza kuchukuliwa na mtu mwingine, wala maisha yake hayatajirudia tena, hivyo wajibu wa kila mtu ni wa kipekee kama fursa yake maalumu kuweza kuutelekeza"

> Siku ya leo ninataka nikuambie kwamba huwezi kufanikiwa mapaka pale utakpoacha kufanya mambo ya kawaida na kuamua kuwa wa kipekee kwa kufanya mambo ya kipekee. Uwepo wako duniani siyo ajari bali upo kwa makusudi maalumu kabisa na una wajibu ambao ni wewe pekee unatakiwa kuufanya na wala hakuna mwingine atakayeziba pengo lako. Tafadhali usimwangushe Mungu ambaye aliruhusu uwepo duniani.

Kama unahisi unafanana na yeyote hapa duniani na unaona  kuna mtu ambaye tayari ashafanya kile Ulichotakiwa kufanya, basi hakukuwa na sababu ya wewe kuzaliwa. (samahani kwa kutumia maneno magumu lakini huo ndio ukweli).
 "Maisha huanaza pale Unapotambua kusudi la uwepo wako duniani"

Aidha siku ya leo nataka nikushirikishe njia tisa (9) za kuwa wa kipekee na wa ajabu kama ulivyozaliwa uwe ili uweze kuishi naisha ya upendo, Yenye uhalisisia na Yenye nguvu ya kweli.

NAMNA YA KUWA WA PEKEE NA WA AJABU KAMA AMBAVYO ULIZALIWA UWE.
1. Jiachie uvunjike vunjike. 
Kama ambavyo huwezi kujenga nyumba mpya juu ya nyumba ya zamani, pia huwezi kujenga maisha mapya kwa kuendelea kushikilia yale ya zamani. Ruhusu utu wako wa kale ufe ili na ruhusu utu upya uzaliwe. Kubali kuzaliwa upya.“



2.Jitambue
Fahamu wewe ni wa pekee.  Hata kama ndiyo Umezaliwa, tambua kuwa wewe ni tofauti na mtu yoyote duniani. Watu Fulani ni tofauti Sana na wengine,  lakini sote tuna tabia na uzoefu tofauti na mwingine yoyote duniani. Hakuna aliye na akili kama zako, hakuna anayefikiri kama wewe,wala hakuna Anayeweza Kufanya jambo Fulani kama wewe Uwezavyo.

3.Kuwa wewe.
Ili uweze kuwa tofauti inavyowezekana, unatakiwa kuwa wewe na wala sio kivuli au nakala ya mwingine. Kama hujui wewe ni nani, kazi ya kuwa wa pekee itakuwa ngumu Sana. Ili uweze kuwa a pekee, ni lazima utambue wewe ni nani? Unafananaje? Unafanana na kitu gani? Una kuwa je pindi ambapo upo peke yako?
Ni muhimu pia Kujipenda na kujikubali namna ulivyo. Kama Hauridhiki na namna ulivyo Utaishia kuiga mtu mwingine, au kuishi kwa kuwapendeza wengine.

4. Chagua namma gani unataka kuwa wa pekee. 

Baada ya kugundua Utofauti ulionao, Namna gani Utaweza kuufikia? Chagua namna ambavyo Utaweza kujitoa katika kundi la Marafiki zako ambao Mmezoea Kufanya Mambo Fulani fulani. Unaweza kuwa tofauti nao kwa namma tofauti tofauti. Namna Unavyotumia muda, namna unavyovaa na Kadhalika. 

5 Tambua Mazingira yako.
Ili kutambua namna ya kuwa wa pekee ni lazima pia uzingatie Mazingira yako. Kutambua Mazingira yako kutakufanya uwe na uwezo wa Kuhimili msukumo kutoka nje ambao kama usipotambua Utajikuta unalazimishwa kufanana na wengine. Mila na tamaduni za jamii zetu Zisikuzuie kuwa wa pekee.

6.Tumia muda mwingine kuwa peke yako.
Mara nyingi siku hizi tunakumbana na kusambaratishwa na vichocheo kutoka nje, ambavyo huweza kuwa watu wanaotuzunguka au vitu kutoka katika runinga. Hivyo ili uweze kurejea katika Uhalisia wa kuwa wewe unahitajika kutumia muda fulani peke yako. Jitenge na kila kitu, simu, runinga na hata watu wa karibu. Tafakari Yale Yanayokuhusu wewe na Yale Yaliyo ya muhimu kwako.
Mara zote huwa tunaambiwa namna ya kuvaa, namna ya kula, vitu vya Kufanya, vitu vya kusoma, na vitu vya Kutazama. Hebu jaribu kuwa peke yako, utajikuta bila Uongozi wala maelekezo. Utapata hisia mpya, kaa tafakari ni kitu gani utakikosa kama hautavaa kama, hautakula kama au Hautaangalia tena kile Ulichokuwa unapenda kuangalia. 

7. Fanya kile unachokipenda. 
Ili mradi unafanya kile ambacho unakipenda, utapata muunganiko wa kitu ambacho ni cha pekee kwako. Ikiwa unapenda upishi, unapenda kuimba unapenda kucheza mpira wa miguu n.k fanya hicho kwa moyo wako na akili zako zote na utashangaa namna unavyokuwa wa pekee katika kile Ukifanyacho. Haijalishi wengine wanasema nini juu yako, kama unafurahia fanya usisubiri mwingine akuambie cha kufanya. 

8.Jaribu vitu vipya.
Mara nyingi tumekulia na kukuzwa katika makundi, hivyo tumezungukwa na vitu ambavyo wengine Wamevikubali. Vitu hivyo vinaweza kuwa ni vizuri, lakini mara nyingi utajikuta unafanya bila hata kuvijua vizuri, jambo hili siyo baya lakini ili uweze kuwa wa pekee ni lazima kujaribu vitu vipya. Tafuta vitu vipya ambavyo unahisi Kuvipenda na jaribu kuvifanya. 

9. Simamia kile Unachokiamini. 
Msimamo imekuwa bidhaa adimu sana kwa binadamu Wanaoishi siku hizi. Hauwezi kuwa wa pekee ikiwa Utakubali Kupeperushwa na kila upepo unaokuja. Kusimamia, Kukitetea na Kupambana katika kile unachoiamini kutakufanya uwe wa pekee na kufungua milango ya mafanikio. 

"Picha yako binafsi ikiwa chanya na Imara ni Maandalizi kwa ajili ya mafanikio" Joyce Brothers. 
Kwa hiyo mafanikio ni lazima yaandaliwe kwa Juhudi za makusudi za Kutafuta kuwa wa pekee ili uweze Kujitofautisha na wengine. 

Mchezaji wa Brazil wa muda wote "Pele" Ambaye jina lake halisi ni Edson Arantes do Nascimento anasema "Mafanikio siyo ajari, mafanikio ni Juhudi, uvumilivu, kujifunza, kujitoa na zaidi ya yote, penda kile unachofanya au kile Unachojifunza Kufanya"
Ukweli ni kwamba ili ukipende kile unachokifanya, kitu cha kwanza ni lazima utambue upekee wa kile na unachokifanya, Hapo utaepuka kuiga vya  wengine maana kile unachokifanya ni cha pekee na unakipenda. 
Chagua kuwa wa pekee ili uweze Kutimiza kusudi ambalo ulizaliwa Kulitimiza. 

"Sharing is caring, share with others to inspire "

Lucas Robert
+255764075392
lucastrngwakwa@gmail.com

"Live an inspired Life"