SIRI AMBAZO ZINAMFANYA MASKINI AENDELEE KUBAKI MASKINI.
A. MAANA YA UMASKINI
Awali ya yote ningependa tujifunze maana ya umaskini na MASKINI.
Umaskini ni Hali ya mtu au jamii ya watu kushindwa kupata mahitaji muhimu ya kila siku kama vile Chakula malazi na mavazi. Mtu aliye katika Hali hiyo ndiyo anaweza kuitwa maskini.
Kwa mujibu wa benki ya Dania, Umaskini ni njaa. Umaskini ni ukosefu wa makazi. Umaskini ni kuwa na maradhi na kushindwa kumuona daktari. Umaskini ni kutokuwa na uwezo wa kwenda shule na kutokujua kusoma. Umaskini ni ukosefu wa kazi, Ni hofu juu ya wakati ujao, kutokuwa na matumaini ya kesho.
Umaskini una sura nyingi, maana yake inaweza Kubadilika kutoka sehemu moja hadi nyingine na umekuwa ukielezwa kwa namna tofauti tofauti. Mara nyingi, umaskini ni hali ambayo kila mtu hutamani kuikwepa. Umaskini ni wito wa kuchukua hatua-kwa maskini. Umaskini ni wito wa kuubadili Ulimwengu ili wengi zaidi waweze kupata Chakula cha kutosha, malazi na mavazi safi, wapate elimu, afya na ulinzi dhidi ya Unyanyasaji, na wawe na sauti dhidi ya kile kinachotokea katika jamii zao.
B.SABABU ZA UMASKINI
Umaskini ni janga ambalo halitokei kwa bahati mbaya pasipo kujua chanzo au sababu zake. Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazoweza kupelekea umaskini kwa mtu au jamii;
1. Kukosa Elimu.
2. Kukosa Ardhi
3. Kuridhika na hali ya Umaskini
4. Matumizi mabaya ya fedha
5. Uoga
6. Imani potofu.
C. TATIZO KUBWA LA MASKINI
Tajiri wa tatu nchini China na mwanzilishi wa mtandao wa Alibaa alisema "ukichukua fedha zote ulimwenguni na ukizagawa sawa sawa kwa kila mmoja, baada ya mda hela zitawarudia wale walio kuwa nazo mara ya kwanza" Kwanini?
Maskini ni watumiaji wakati matajiri ni wawekezaji.
Anasema, " Niambie Nikuoneshe mtu maskini, nitakuonyesha mtu anae pishana na fursa mara kwa mara. MTU anayeona changamoto ndani ya kila fursa badala ya kuona fursa ndani ya kila changamoto".
Kuwa MWANAUME sio cheo, ni jukumu. Inamaanisha unapaswa kuwwajibika kiuchumi Asubuhi, Mchana na Usiku.
Maana halisi ya utu uzima siyo umri, Ni majukumu.
Lazima uchukue maamuzi magumu ili upate matokeo makubwa.
Unapaswa kupanga na kuweka mikakati, lazima uthamini faida na fedha kidogo unayoipata. Lazima uwe makini na mwenye nia kama unataka kufanikiwa.
Watu wabaya kabisa kuwahudumia au kuwasaidia hapa duniani ni WATU MASKINI.
Albert Einstein alisema pia " Dunia ni mahali hatari sana kwa kuishi, so kwa sababu ya watu wanaotenda maovu Bali ni kwa sababu ya watu wasiofanya chochote".
MASKINI ni watu ambao hawafanyi chochote, Kwa sababu:
1) ukiwapa bure, watahisi ni mtego.
2) ukiwaambia ni mradi mdogo wawekeze, watakwambia hauwezi ukaleta faida
3) ukiwambia waingie kuwekeza katika ukubwa, watakwambia sina hela
4)ukiwaambia wajaribu vitu vipya, watakwambia hamna uzoefu: umewahi kuona wapi hichi kitu kimefanikiwa? Nani amewahi kufaidika nacho?
5) Ukiwaambia ni biashara ya kawaida ya kila siku, watakwambia ni kazi ngumu sana hiyo
6) ukimwambia ni mpango biashara mpya, atakwambia mimi huwa siongeagi sana na watu alafu ni kwa miaka mingapi sasa huu mpango biashara umekuwepo?
7) ukimwambia afungue duka, atakwambia nitakosa uhuru ntashindwa kufanya mambo mengine.
Sasa mwambie afate mpango wa biashara yake kwa mwaka mmoja, atakwambia ni mda mrefu sana huo, siwezi subiri.
9) ukimuuliza ni ni anaweza kufanya, atakwambia "naweza kufanya chochote"
10) wanapenda kuwauliza marafiki zao, ambao ni kama wao juu ya mtazamo wao. Hata maandiko takatifu yameeleza kuwa vipofu, kamwe hawaongozi vipofu wenzao.
11) wanafikiri zaidi ya mkufunzi wa chuo kikuu na wanafanya kidogo kuliko kipofu.
Changamoto kubwa sana watu maskini walio nayo, ni kukosa kuchukua hatua
Wanafurahia kasehemu kasiko na mahangaiko. Wanakwea katika dimbwi la ulimwengu wa dhiki na ufahamu wao mdogo.- Jack Ma
Kujaribu vitu vipya ni hatari, lakini kutokujaribu vitu vipya ni hatari zaidi.
Kwa makala zaidi soma,
http://ngwakwaufanisi.blogspot.com
Lucas Robert
+255764075392
lucastrngwakwa @gmail.com