Katika safari ya maisha Mara nyingi huwa kuna kuanguka au kuporomoka kutoka katika hali ya juu uliyokuwa nayo kiroho au kiuchumi. Mara nyingi hali hii husababishwa na kujisahau au kupuuzia mambo ambayo yamekufanya ufike pale ulipokuwa. Pamoja na hiyo zifuatazo ni miongoni mwa sababu muhimu sana zinazoweza kupelekea anguko katika hali yoyote ya Maisha:-
1.Roho ya kiburi na kujitukuza.
Kuna msemo mmoja ambao sikumbuki ulisemwa na nani unasema "Ukiona mbwa yupo juu ya paa la nyumba ujue kapandishwa" Msema huu unamaana kubwa katika safari ya mafanikio. Ukiona uko juu lazima ukumbuke kuwa Luna watu ambao walikuweka hapo juu hivyo usimdharau ambaye yupo chini kwa sababu siku utakaposhuka Luna uwezekano usipande tena na pengine utakaposhuka Yeye ndiye atapanda. Kwa hiyo unapopanda juu kumbuka kuwa Luna watu ambao walikuweka hapo juu kama siyo Mungu mwenyewe. Unyenyekevu siyo unyonge, unyenyekevu kwa Mungu na kwa wanadamu utakuweka juu zaudi
" Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa" (Mathayo 23:12).
2.Kupenda sifa kupita kiasi.
Sifa hazitafutwi Bali zinakuja zenyewe baada ya kufanya vizuri kwa sehemu yako. Kama utapenda sifa kupita kiasi katika Maisha yako utakuwa unafanya kwa ajili ya kuwapendeza wengine na hivyo utapoteza mwelekeo na kukosa shabaha ambako kutapelekea anguko.
Pia kama unapenda sifa kupita kiasi kitu kingine kitakachopelekea ushuke chini ni kukata tamaa baada ya kufanya ukitegemea watu watakusifia na badala yake wasikusifie au wakakupinga kabisa - bila shaka utajisikia vibaya na kukosa shauku ya kufanya zaidi.
3. Kudanganyika na starehe na Kuridhika.
Starehe na Kuridhika ni adui Mkubwa wa mafanikio yetu. Starehe ni kama saratani ambayo inauwezo wa kutafuna mafaniko ya MTU taratibu lakini kwa uhakika. Kila senti na sekunde unayoitumia kwa starehe haitarudi mpaka unatoweka duniani. Starehe na kufurahia Maisha ni vitu viwili tofauti, Unatakiwa kufurahia Maisha lakini siyo kufanya anasa au kufanya matumizi yaliyo nje ya uwezo wako.
Kwa upande mwingine Kuridhika au kujiona umefika ni kama moshi au utando unaohafifisha uwezo wako wa kufikiria mbinu mpya za kufanikiwa, Inahafifisha ubunifu wako na kukufanya ubaki pale pale na hatimaye kuanguka. Watu wanaobaki kuwa na mafanikio ni wale wanaotamani kupiga hatua ndogongo kula siku bila kurudi nyuma.
4.Kushirikiana na watu wenye mtazamo tofauti na wako (Watu wenye mitazamo hasi).
Marafiki wanamchango Mkubwa katika kufanya upande juu au ushuke juu, katika kubaki juu au kubaki chini. Mara nyingi watu wako wa Karibu ndio ambao wamekufanya uwe hivyo ulivyo. Kuna msemo usemao "Nioneshe marafiki zako nami nitakuambia tabia yako" Kama ukiwa na marafiki ambao wao mtazamo wao ni hasi bila shaka watakufanya uwe na mtazamo hasi na utashindwa kufikia malengo yako Na wakati mwingine utapoteza hata kile ulicho nacho. Kwa mfano kama ukiwa na marafiki ambao starehe zao ni ulevi na wanawake bila shaka baada ya muda na wewe utakuwa mlevi na mpenda wanawake vitu ambavyo vitakushusha hadhi yako.
Hivyo ni vyema kukaa mbali kabisa na watu wenye mitazamo hasi pamoja na watu wenye mtazamo tofauti na wako maana wao hawajui uendapo.
5. Imani potofu.
Utafiti wa kisaikolojia umebaini kuwa akili yako bila wewe mwenyewe kujitambua huwa inafanyia kazi kile inachokisikia ukisema. Akili yako na mwili wako vitakuelekeza katika kile ambacho unakiamini. Kuna watu wanaoamini kuwa kuna kiwango ambacho huwezi kuzidi katika mafanikio na kama ukifanikiwa kuzidi jambo baya litakupata. Kwa sababu ndivyo unavyoamini akili yako haitajishughulisha zaidi baada ya kufikia kiwngo kile ambacho wewe unaamini ni cha juu, Hivyo itakuwa rahisi sana kuanguka kwa sababu "Ndoto ambayo haipaliliwi hufa".
Anguko linaweza kutoka katika maisha, lakini ukiangalia kwa sehemu kubwa linaweza kusababishwa na mtu mwenyewe. Sababu nilizozieleza hapo juu kwa sehemu kubwa zipo ndani ya uwezo wa mhusika. Ni muhimu sana kujua kumjua adui yako ili ujue namna ya kupambana naye. Hao ndio maadui ambao wanaweza kuyatafuna mafanikio yako, haijalishi mafanikio uliyofikiria ni madogo au makubwa kiasi gani hauna budi kuyalinda dhidi ya maadui hao kwa kujichunguza kila siku.
>Ukiona kiburi kinakunyemelea ujue kinataka kutafuna mafanikio yako shituka, Ukiona unapenda kusifiwa kwa kila unalofanya Amka haraka sana Huyo ni adui anayevizia mafanikio yako, Ukijihisi kupenda starehe gutuka utajuta baadaye, kama marafiki ulionao wanafikira hasi ni muda wa kufanya mile unachokiamini, Kama kuna kaimani ambako kako tofauti na malengo yako ni muda wa kuamini katika ndoto yako kwamba inawezekana.
Hizi ndizo sababu zilizositirika zinazotafuna mafanikio ya walio wengi.
" Live an inspired life".
lucastrngwakwa@gmail.com
Lucas Robert.



