Mwaka huu una maana yoyote kwako?
Kama hauna maana yoyote na kama ulikuwa hujapanga kuuangalia kwa namna tofauti basi na sawa na 2019 tu.
Mwaka 2020 una maana gani kwako?
Ni swali la msingi sana ambali kila mtu alitakiwa kujiuliza kabla ya kuushangilia mwaka mpya.
Wengi tunaushangilia mwaka mpya bila kujua tunachokifanya, tunatakiwa kufanya vitu vifuatavyo ndipo tutakuwa na haki ya kusema huu ni Mwanka mpya.
1. Mwaka uliopita umekufundisha nini?
Wazungu wanasema " the past is a teacher before the future exams" ni lazima uwe umejifunza kitu kutoka kwenye mwaka uliopita ili uweze kukabiliana na mitihani inayokuja mwaka huu.
2. Umefanikiwa kufanya yapi mazuri yenye mafanikio kwako mwaka uliopita?
Mtu mwenye mafanikio ana tabia ya kufanya tathimini ya kile alichokifanya, Tathimini humsaidia kugundua wapi pakurekebisha na wapi pa kuongeza juhudi zaidi, bila tathimini huwezi jua ni kwa kiasi gani umepiga hatua.
3. Je malengo yako yalifanikiwa katika mwaka uliopita? Ni vyema kuangalia malengo uliyokuwa umejiwekea kama yametimia kwa 100%
Kama hayakutimia jiulize maswali yafuatayo:
(a) Hayajatimia kwa uzembe wangu?
b) Kama sio uzembe wangu, Je kuna vikwazo gani vilivyofanya nisitimize malengo yangu?
c) Je vikwazo hivyo viko ndani ya uwezo wangu au la?
d) kama vikwazo hivyo haipo ndani ya uwezo wangu, je kuna msaada wa kuviondoa?,
e) Je malengo yako yalikuwa mazuri? Je yalikuwa yanafikika?
4.Je una malengo yapi katika mwaka unaokuja?
Mtu asiyekuwa na malengo ni sawa na mtu anayetembea bila kujua anakokwenda. Malengo ni kama ramani inayokuwezesha kufika unakotakiwa kufika. Chora ramani bora katika akili yako ili uweze kufika sehemu bora.
SIFA ZA MALENGO BORA.
1. Malengo lazima yawe yanavutia na kuamsha mwili na akili kufanya juhudi na bidii ili kuweza kuyafikia.
2. Malengo lazima yawe yanafikika, au yawe ni yale yaliyo ndani ya uwezo wako. Huwezi kuweka malengo ya kujenga nyumba ya milioni 200 wakati mshahara wako ni laki mbili kwa mwezi hayo ni malengo yasiyofikika.
3. Malengo yawe na njia zaidi ya moja kufikika ( alternative ways to reach)
Usiweke malengo malengo yanayokulazimisha kupita njia moja tu sio rahisi sana kuyafikia, maana pale njia hiyo ikikwama bila shaka utakata tamaa na kushindwa kutimiza malengo
4. Malengo yako lazima yawe yanaanzia sehemu ndogo kwenda kubwa ( diverging rays of objectives)
Mfano weka malengo ambayo ukifanikisha kitu kidogo ndani ya muda mfupi kinakiuandaa kufanikisha kitu kingine kikubwa baadaye.
5. Malengo shirikishi. Malengo bora ni yale ambayo unaweza ukashirikisha kitu zaidi ya kimoja au mtu zaidi ya mmoja katiaka kuyatimiza.
Achana na malengoa ya kukumbatia kitu kimoja, au malengi ya kujitwisha peke yako wakati kama ungemshirikisha mtu kidogo malengo yako yangetimia haraka sanaa.
6. Malengo lazima yawe ni yale yanayokupa amani ya moyo (peace of mind) Usiweke malengo ambayo moyo wako haufurahii, Yatakuumiza bure na hata utakapoyatimiza Nafsi yako haitaburudika.
Usikose siku nyingine tutakapoangalia
NAMNA YA KUTIMIZA MALENGO ULIYOJIWEKEA
Hizo ni baadhi ya sifa za malengo bora maishani , zipo nyingi lakini hizo ni chache ambazo ni za muhimi zaidi. Panga malengo bora katika mwaka huu na uweke mikakati ya kutimiza kwa wakati chini ya uongozi wa Mungu.
Nawatakia Mwaka mpya wenye mafanikio Mema, Mwenyezi Mungu awe nanyi mnapojipanga kutimiza malengo mliyojiwekea.
Makala hii imeandaaliwa na Robert Lucas
0764075392/0629085619
lucastrngwakwa@gmail.com
