Ticker

6/recent/ticker-posts

KUMBUKUMBU ZENYE MNATO.

KUMBUKUMBU ZENYE MNATO.
Kumbukumbu ni mawazo au marejeo ya kitu kilichopita, Ni taswira au picha ya jambo au tukio lililopita.
Bila shaka kina jambo ambalo ukilikumbuka linagusa sana hisia zako, jambo hilo linalogusa hisia zako ndizo mojawapo ya KUMBUKUMBU ZENYE MNATO.
Kila hatua unayoipiga katiaka safari yako ya Maisha unatengeneza historia isiyofutika hata milele. Historia za watu mashuhuri na maarufu duniani hazikutokea kwa bahati mbaya,  Bali ni makusudi na juhudi binafsi ambazo watu hao waliwekeza ili kufanya ziweze kuwa za kipekee kama ambavyo unazisoma.
Nafasi ambazo watu hao walikuwa nazo ni zile zile ambazo hata wewe unazo,  ni siku ile ile yenye masaa 24 ndiyo ambayo walikuwa nayo, Pengine wewe ukawa na rasilimali nyingi na muda mwingi sana wa kutengeneza historia nzuri saaaana na yenye mguso wa kipekee kwa wengine. Amua Leo sasa kwa Kumshirikisha Mungu ili uweze kutengeneza KUMBUKUMBU ZENYE MNATO.
> Watoto wako na vizazi vijavyo vitavutiwa sana na kufurahi sana endapo watakuta historia nzuri na inayovutia nao watatamani kuishi kama mtangulizi wao alivyoishi. Bali watoto wako na vizazi vijavyo vitahuzunika sana wala havitavutiwa kuishi kama ulivyoishi kama historia yako itakuwa haivutii maana KUMBUKUMBU zake HAZINATI katika bongo zao.
> Hivi leo tunafurahia na kujivunia kusoma historia za Maisha ya watu mashuhuri duniani Mfano kina Martin Luther King JR, Isack Newton SIR, Julius Kambarage Nyerere mwl, Albert Einstein, Dr. Benjamin Carson, Yesu kristo -Masihi na wengine weeengi ambao wewe unawafahamu, Hao wote bila shaka unavutiwa sana kwa ushujaa na umahiri wao na pengine unatamani sana kuishi kama wao.
Katika historia hizo za watu Mashuhuri na maarufu waliotangulia yapo mengi sana ya kujifunza. Hayo yote unaweza kuyapata kupitia kusoma vitabu vya Kumbukumbu zao. Kwa mfano Kupitia Biblia tunapata historian za watu mashuhuri kama Daniel, Yusufu, Musa Na Yesu kristo, wengi wao walikuwa ni wasomaji wazuri wa vitabu na machapisho mbalimbali hii iliwasaidiakujipatia maarifa ambayo yaliwafanya waandike historian zenye kugusa maana walitambua njia ambazo ni sahihi wakazifuata na njia ambazo si sahihi wakaziacha. Hii ni mifano Anuwai kabisa ambayo Hata kwetu hivi Leo kama tunataka kutengeneza historia ambazo zitakuwa zinagusa maisha ya watu katika siku za Usoni ni lazima tuwe WASOMAJI au wasikilizaji wazuri sana.

> Naam, Sitaishia hapo tu napenda pia kukukumbusha kuwa hizo historia au maandishi tunayofurahia kuyasoma hivi Leo tusingeyapata ikiwa yasingeandikwa ama kuhifadhiwa kwa Namna ya kipekee. Wapo watu ambao walikuwa na uwezo wa kuandika historia zao wenyewe, mfano Musa mwandishi mmoja wapo wa Biblia, Dr. Benjamin Carson katika kitabu chake cha GIFTED HANDS na Kile cha THINK BIG, Dr. Carson Ameandika Mengi sana na bado yu Hai mpaka sasa nasi tunafurahia kusoma historia hizo, Lakini wapo wale ambao wao hawakuandika historia zao kwa mikono yao lakini kutokana na watu wengine kuvutiwa na mfumo wa Maisha yao wakaamua kuandika kwa niaba yao ili kutunza mifano ambayo ni hai. Ninajaribu tu kutoa mifano ambayo ni Rahisi ili tupate kuelewana.

>Mpendwa na Rafiki yangu wapo watu ambao walikufa miaka maelfu iliyopita lakini mpaka leo matendo yao bado yanaishi.
> Wito wangu kwako leo ni kwamba hakikisha kila sehemu unayoishi unaacha KUMBUKUMBU ZENYE MNATO, Ikiwa unaweza anza kuziandika sasa, yapo matukio mengi sana mazuri ambayo kama ungekuwa uneyaandika mahali fulani yangekuja kuwa masomo mazuri sana kwa vizazi vijavyo. Tumia vizuri kalamu na Notebook yako kuandika kumbukumbu zako ambazo ni nzuri ipo siku hata wewe mwenyewe utafurahia kufanya marejereo ya nyakati zilizopita. Naam si wote wenye tabia ya kuandika andika, ikiwa huwezi kuwa ROLE MODEL kwa wengine, ishi maisha yenye mfano nakuhakikishia wapo watu ambao wataiandika historia yako hata kama utakuwa ushakufa bado matendo yako yatabaki hai maana walikuwa wanavutiwa na maisha yako.
Ujana ndicho kipindi ambacho huchukua kurasa nyingi sana katika vitabu vya historia vya watu mbalimbali mashuhuri. Ikiwa wewe ni kijana tengeneza KUMBUKUMBU ZENYE MNATO sasa katika kipindi hiki ambacho unaweza kufanya mambo mengi kwa muda mfupi na kwa usahihi zaidi.
> Inasikitisha sana ikiwa mpaka sasa kijana mwenzangu utakuwa hujui sababu ya kuwa hai hivi Leo, Hujui kwa nini upo hai Leo!? Naam, ikiwa hutambua nakusihi kuanzia wakati huu unaposoma makala hii tafuta kujua kusudi LA Kwanini ulizaliwa na kwa nini upo hai mpaka sasa. Ikiwa ulikuwa hujafanya jambo lolote ambalo ikiwa utakufa Leo hakuna atakayekukumbika kwa lolote, basi anza sasa! Anzia hapo hapo ulipo, anza hivyo hivyo ulivyo, kila unavyozidi kusubiri muda huo unaufanya kuwa historia.

Na huu ndio utakuwa mwisho wa ufafanuzi wangu kuhusu KUMBUKUMBU ZENYE MNATO. Nakutakia kila Lakheri unapoanza maisha mapya ili kutengeneza kumbukumbu zenye Mnato.
Na karibu tena siku nyingine.

LUCAS ROBERT

+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com

"Live an inspired life"