SEHEMU YA PILI: CHAPA / BRAND NAME.
Katika safari yoyote ambayo unahitaji kusafiri unahitaji mwanga ili uweze kuiona njia vizuri na uweze kutembea kwa kujiamini bila kuwa na hofu ya kujikwaa. Mathalani katika safari ya mjasiriamali ambapo wakati mwingine hufunikwa na Giza kuu ni muhimu sana kuwa na chanzo cha mwanga (taa).
Ikiwa unatamani kuwa mjasiriamali ni lazima utambue umuhimu Wa Taa ijulikanayo kamakama (CHAPA) BRAND NAME (Au jina Taambulishi) namna ya kufanya branding, na aina IPI ya branding itakayokufanya ung'ae sokoni.
Nini maana ya brand?
Brand name ni Alama au jina tambulishi la bidhaa, Huduma au wazo ambalo hutofautisha bidhaa au Huduma miongoni mwa bidhaa zinazofanana. Jina tambulishi au brand name pia humaanisha Jina la mtu ambaye ni maarufu ambaye anajulikana kitaifa au kimataifa kutokana na kazi anazofanya, bidhaa au Huduma anazotoa.
Branding Uwekaji Chapa au utengenezaji Wa Jina tambulishi la biashara ni namna ya unavyoielezea na kuitambulisha biashara yako kwako binafsi, watu wako Wa karibu na kwa Wateja wako Wa nje. Brand name ndio utambulisho Wa biashara yako, Hiki ndicho kinaelezea namna ambavyo biadhara husika ilivyo na thamani au ubora wake.
Katika biashara yoyote kitu ambacho Wateja wanakihitaji ni kumfahamu mfanyabiashara au mtengenezaji kuliko kuifahamu bidhaa ubora Wa bidhaa unafuata baada ya kuifahamu jina la muuzaji. Mteja kupenda Brand au chapa ni sawa na watu wawili wanapokuwa wameingia katika mapenzi. Mtu akipenda kweli kweli kutoka moyoni Mara nyingi huwa anakuwa na upofu Wa kutokuona kasoro za mpenzi wake. Hivyo ndivyo ilivyo kwa mteja na brand name ya bidhaa au Huduma. Utakuta mtu anasema kaniletee unga Wa Ngano Chapa AZAM Sio kwamba una kitu cha pekee sana Bali ni Hiyo Chapa yake ndiyo inayomvutia mnunuzi au mtumiaji.
VITU MUHIMU KWENYE CHAPA(BRAND)
1. Jina Tambulishi.
2. Rangi zinazohusika.(Associated colours)
3.Alama zinazohusika (Logo and symbols).
> Alama hizo ziwe za kuvutia na zinazoendana na uhalusia Wa Huduma au bidhaa.
4. Maekezo mafupi ya mtoa Huduma au bidhaa.
>Hapa unaweza kuambatanisha Mawasiliano na mahali unapopatikana
5.Maelezo mafupi kuhusu ubora na usalama Wa bidhaa au Huduma.
>Kama bidhaa yako imefikia hadhi Fulani ya ubora ni vyema ukaonesha. Mfano kama hoteli yako inatoa Huduma za Hadhi ya nyota tano ni vizuri kusema au kuitambulisha kwa mteja.
SIFA ZA CHAPA AU BRAND NZURI
Ili bidhaa yako iweze kukubalika sana sokoni ni Ni muhimu sana wewe kama mzalishaji au mtoa Huduma kuipa bidhaa yako jina sahihi. Jina au chapa inaweza kuwa nzuri au mbaya, kutegemeana na uvuri au ubaya Wa chapa au jina tambulishi la bidhaa yako inaweza kuongoza au kupunguza kiwango cha mauzo. Kwa sababu jina na Chapa ndivyo vinavyotoa picha, hisia, mwanga na utambulisho Wa bidhaa kwa ujumla.
>Kiuhalisia kubuni na kutengeneza chapa au jina tambulishi siyo kazi rahisi. Lakini pamoja na ugumu huo, zifuatazo ni baadhi tu ya sifa au vitu muhimu vya kuzingatia wakati Wa kutengeneza Chapa au brand nzuri:-
1. RAHISI NA NYEPESI KUITAMKA.
Chagua jina rahisi linalitamkika kirahisi Na linaeleweka kirahisi kwa kila mtu au mteja wako. Mfano: MSOMI CENTER. Lazima liwe na uwezo Wa kutamkwa na watu wote, Msomi na Asiye msomi, mdogo kwa Mkubwa, mtu Wa kabila na lugha yoyote. Kama umeamua kutumia jina la kilugha au lugha za kigeni tafuta lile ambalo ni rahisi kutamkwa hata na mtu ambaye siyo Wa kabila hilo. Mfano: FUMO YISE (kisukuma), SAVER POINT (English). N.k
2.JINA LIWE FUPI.
Jina zili ni lile ambalo ni fupi maana ni rahisi kulitamka na kulikumbuka. Jina likiwa fupi pia inakuwa rahisi hata kilichapa kwenye nafasi ndogo tu.
3. INAYOTAMBILIKA NA KUKUMBUKWA KIRAHISI.
Rangi, na jina razima liwe linakumbukwa na kutambulika kirahisi. Jina zuri ni lile ambalo mtu akiliona tu hata kwa Mbali analitambua na kulikumbuka kwa mida mrefu.
4. LIWE JIPYA NA LINALOVUTIA.
Ili bidhaa yako iweze kukibalika sokoni ni lazima iwe na jina na chapa inayovutia, Ikiwa chapa ya bidhaa mpya itaonekana sokoni na ikawa na ubora Wa juu bila shaka jina hilo litasambaa kwa urahisi na kuongeza mauzo. Usiige jina Ambalo tayari lishazoeleka kwa wateja tafuta jina ambalo ni Jipya kabisa au ambalo halijazoeleka ili kufanya bidhaa yako kuwa ya kipekee.
4. LIENDANE NA UHALISIA WA BIDHAA.
Jina linaloendana na uhalisia au aaili ya bidhaa litamfanya mteja kukumbuka Umuhimu au matumizi ya bidhaa yenyewe. Mfano: Sweet Dreams, Fikira tulivu, Maisha mrua n.k linaweza kuwa jina linaloashiria Sehemu nzuri Ya kupumzika.
6. LIWE LINAPENDEKEZA.
Bidhaa lazima itoe pendekezo Fulani kwa mteja, ili kwamba mteja anapolisikia spate picha ya umuhimu au ulazima Fulani Wa kutumia bidhaa hiyo.
7. LIWE LIMESAJILIWA AU LINALOTAMBULIKA KISHERIA.
Wakati unachagua jina ni vizuri kujihakikishia kama jina hilo halitumiwi na shirika au kampuni lingine. Kuasijili kunakupatia ulinzi Wa jina na chapa yako dhidi ya matumizi mabaya. Pia hii itasaidia mtu mwingine asiweze kulitumia kwa ajili ya kujinufaisha au kujipatia faida kupitia mgongo wako au jina na chapa yako.
8. LISISHAMBULIE AU KUPONDA BIDHAA ZA WENGINE.
Ikiwa jina lako litakuwa na maudhi kwa mtengenezaji Wa bidhaa nyingine au mtumiaji sio rahisi sana kukubalika kwa sababu lipo kundi kubwa sana la Wateja ambao kwa wakati huo linatumia bidhaa Fulani na Wateja hao hà o ndio ambao unahitajika kuwavuta kwako, kwa hiyo unavyomponda mtoa Huduma wao utakuwa unawaponda pia. "Wateja ni wetu sote" usimuudhi mtoa Huduma mwenzako au mteja.
Pamoja na sifa hizo hapo juu jina ni lazima Liwe la kiuchumi na linaloendhana na muktadha au mazingira. Hivyo basi vingezo hapo juu ni lazima vichagulwe kwa umakini Mkubwa ili kuweza kupata jina zuri lenye mvuto na mwonekano Wa kibiashara.
UMUHIMU WA CHAPA AU BRAND.
Chapa au brand ni kitu cha muhimu sana ili kuweza kupanua na kutangaz biashara yako. Brand INA umuhimu Mkubwa katika pande zote mbili za biashara, Yaani upande Wa mteja au mtumiaji Wa bidhaa na upande Wa mtoa Huduma/mfanyabiashara au mzalishaji.
A. UMUHIMU WA CHAPA (BRAND) KWA UPANDE WA MTEJA.
1. Humwezesha mteja kuitambua bidhaa. Chapa humsaidia mteja kuweza kutofautisha bidhaa moja na nyingine, pia kutofautisha mzalishaji au kiwanda kimoja na kingine. Wateja ambao si wafuatiliaji sana wa bidhaa huwa ni rahisi kwao kuitambua bidhaa iliyopo dukani ambayo ina chapa fulani.
2. Kupunguza kubadilika badilika kwa bei na thamani ya bidhaa.
Bidhaa zenye chapa moja Mara nyingi huwa hazitofautiani sana bei, hivyo humfanya mteja kununua bidhaa sehemu yoyote kwa kujiamini.
3. Humwezesha mteja katika ununuzi wa spea za mashine, magari. Mara nyingi mtu anapiamua kununua spea ya mashine au gari lake ataangali ile ambayo ina jina au chapa sawa na mashine yake.
4. Hujenga imani kwa mteja.
Bidhaa ambayo ina chapa fulani inayojulikana huaminiwa na wateja kuliko ile ambayo haina chapa au yenye chapa isiyojulikana. Mteja hujenga saikolojia ya kuridhika na aina Fulani ya bidhaa yenye chapa au jina Fulani. Mfano: mfano unakuta mtu ameridhika na matumizi ya ngano chapa AZAM na ni vigumu sana kwake kubadili imani hiyo.
5. Humwezesha mteja kuagiza bidhaa mara kwa mara. Kama mteja anaifahamu na ameridhika na bidhaa ataweza kuagiza bidhaa na kuletewa hata bila yeye kufika sehemu ya kununulia au kuzalishia.
B. UMUHIMU WA CHAPA (BRAND) KWA MZALISHAJI.
1. Humsaidia mtengenezaji kutangaza biashara au bidhaa yake.
> Bidhaa yenye chapa ni rahisi kuitangaza na kuifanya watu wavutiwe nayo na kuihitaji.
2. Husaidia kulinda soko.
Bidhaa ambayo ina brand hudumu zaidi sokoni kuliko bidhaa ambayo haina chapa. Bidhaa yenye chapa hutengeneza kitu muhimu katika soko ; 'brand loyalty au brand patronage'
3.Kuongeza manunuzi kwenye bidhaa mpya. Kama mteja amejenga uaminifu na bidhaa Fulani itakuwa ni rahisi kwake kununua bidhaa nyingine mpya yenye chapa moja na ile aliyoizoea.
4. Hupunguza ulinganishwaji Wa bidhaa.
Mteja hataweza kulinganisha bidhaa zenye majina au chapa tofauti tofauti kwa sababu chapa zenyewe zinatofautiana. Hii pia husaidia kupunguza ushindani kwenye bidhaa .
5. Hutoa picha ya kampuni au mtengenezaji. Bidhaa bora hutangaza ubora na hadhi ya mtangazaji, kwa sababu hiyo inaongeza mauzo.
KUMBUKA:
> Kadri jina linavyozidi kusambaa ndivyo mauzo yatakavyoongezeka, usilikatae jina ambalo watu wanakuita kwa sababu ya bidhaa au huduma unayotoa. Mfano: Kama wewe ni muuza chapati Ukiitwa jina kama LUCAS MACHAPATI usikasirike kwa sababu wanakusaidia kutangaza bidhaa yako ya chapati.
> Naam, Chapa nzuri au jina zuri la bidhaa, au kampuni ndilo linaloonyesha mafanikio katika biashara yako, Hivyo ni Muhimu sana kutengeneza jina zuri. Jina bora lina thamani kuliko mtaji mkubwa. Kuna msemo usemao "Tafuta jina kwanza na pesa zitafuata"
Kama unahitaji kutengeza CHAPA (BRAND) itakyokufanya ung'ae sokoni karibu tusaidiane.
Kufikia hapo Sina LA ziada kuhusu BRAND & BRAND NAME.
LUCAS ROBERT
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com
