Ticker

6/recent/ticker-posts

BARA & MIJI YA KUKIMBILIA - AFRIKA

AFRIKA NI SEHEMU YA KUKIMBILIA (MIJI YA KUKIMBILIA)
Tangu mwanzo bara la Afrika lilikuwa ndilo bara ambalo lilitumika kuokoa mabara mengine, Watu wa mabara mengine walikuwa wanakimbilia katika bara la Afrika ili kupata msaada.
Katika historia inaonesha wazi kwamba baada ya Mapinduzi ya viwanda katika nchi za Ulaya malighafi zilikosekana katika bara la Ulaya na Asia, Lakini malighafi zilikuwa zinaweza kupatikana katika bara la America. Pamoja na uwezekano wa kuzipata hizo malighafi katika bara la Amerika bado bara la Afrika lilibaki kuwa bara la makimbilio kwa Dunia kwa sababu ni Afrika pekee ambapo malighafi nyingi zilipatikana na Nguvu kazi za kuzalisha malighafi huko Amerika zilichukuliwa Afrika. Hivyo Afrika ikawa ndiyo miji ya Makimbilio ili kutatua changamoto hizo.

Baada ya Mabara mengine kutambua kuwa Afrika ndiyo sehemu ya kukimbilia waliamua kuliangalia bara hili kwa jicho la pili, wote wakaanza kugombania kuja barani Afrika,  Kwa ajili ya kutanua utawala wao, mataifa mengi kutoka nchi za ulaya yalikimbilia Afrika na katika baadhi ya nchi za Asia, Baada ya ugomvi juu ya bara hili ambalo lilionekana kuwa ni sehemu ya kukimbilia kwa kila mtu kuwa mkubwa, Wakimbizi hawa wakaamua kuitisha mkutano huko kwao ujerumani ambao waliupa jina la mkutano wa Berlin (Berlin Conference) mwaka 1844 ili waweze kuzigawana Sehemu hizi za kukimbilia kwa Amani.  Baada ya mgawanyo kufanyika baadhi ya wagombaniaji wakaona mgawanyo uliofanya kuwa haukuwa sahihi, Na hii ikawa ni moja Ya sababu zilizopelekea vita ya kwanza ya dunia mwaka mnamo 1914, Japokuwa hii siyo sababu pekee, ila sababu zingine naomba tuziache maana zipo nje ya maada ninayotaka kuizungumzia.

Hebu tuangalie pia katika vitabuvitakatifu, sina Aya nyingi sana kutoka katika Quran tukufu zinazoongea namna Bara la Afrika lilivyotumika kama mkono wa msaada au wokovu kwa vizazi vilivyopita hata sasa ila naamini pia Bara la Afrika limetajwa vyema na kuthaminiwa pia. Hebu tuangalie kidogo katika Biblia, Historia inasema kulitokea njaa katika nchi aliyokuwa anaishi Abramu (Uru wa wakardayo) ambayo kwa sasa ni ipo Asia, Abramu alikimbilia Misri (ambayo ipo Afrika) ili kujiokoa na njaa iliyokuwa inakabili nchi yao. (Mwanzo 12: 10). Pia ilitokea njaa kali katika katika dunia yote watu wote wakakimbilia Afrika (Misri) kuchukua nafaka ambazo mtu mmoja mwenye hekima akiongozwa na Mungu alizikusanya kwa muda wa miaka 7. (Mwanzo 41: 53-57), Hayo tu hayatoshi kuonesha kuwa Afrika ni nchi ya kukimbilia? Ngoja tuendelee kidogo, Yesu aliopokuwa anatafutwa kuuawa na mfalme Herode alikimbizwa Afrika (Misri) na mama yake naye aliokoka na mkono wa Herode.

>Katika ulimwengu wa sasa pia uwekezaji mkubwa wa mataifa makubwa kama Marekani na China unafanyika Afrika, hii ni kuonyesha ni namna gani Bara la Afrika lilivyo tunu.

Utafiti wa hivi karibuni unaonesha hivi "Katika Miaka ya usoni Mabilionea wengi watatoka Afrika nao watafanikiwa sana kupitia KILIOMO - Uwekezaji katika kilimo cha kisasa". Utafiti huu unaonekana kuwa ni kweli kutokana na Sababu kuwa kilimo ndiyo shughuli inayotuwezesha kupata chakula chetu cha kila siku, na hivyo kwa vile idadi ya watu inazidi kuongezeka duniani mahitaji ya chakula pia yanaongezeka. Hivyo kwa mtu atakayewekeza katika uzalishaji wa bidhaa hii ambayo ni ya lazima kwa kila mtu atajipatia kipato cha kutosha na kumwezesha kuinuka sana kiuchumi.

> Naam, nimeandika hayo yote nikiwa nimelenga kuongea mambo makubwa mawili tu. Nayo ni kama ifuatavyo:-

1. Kilimo ni shughuli muhimu sana katika uchumi wa mtu binafsi na uchumi wa nchi kwa ujumla. Hivyo basi kutokana umuhimu wa shughuli hii, Vijana hasa vijana wa Tanzania na Afrika kwa ujumla ambapo sehemu kubwa ya Ardhi bado ipo wazi na ikiwa na rutuba hawapaswi kuzipuuza shughuli za kilimo hata kidogo ikiwa wanahitaji kufanikiwa. Ninawasihi vijana wenzangu tuangalie uwekezaji wa njia ya kilimo cha kisasa.
Ni wazi kuwa kilimo kina changamoto nyingi, Lakini penye changamoto nyingi ndipo penye fursa nyingi pia.

2. Mtazamo wa kujidharau kwa kuwa wewe ni mwafrika na kulidharau bara la Afrika sio sahihi hata kidogo. Bara Afrika limebarikiwa kwa kila kitu kuanzia Ardhi na hata watu wake pia wana nguvu nyingi sana lakini wengi wao walikuwa hawajajua kuitumia akili yao. Ikiwa kila kijana Mwafrika atajua kutumia Akili na Rasrimali zinazomzunguka kwa ufanisi Bila Shaka dharau kwa waafrika itakoma na watu wa Magharibi watajuta kwa nini walitupatia elimu.

Mwisho: Napenda kukusihi na kukuomba Usijidharau kwa jinsi ulivyo, usichague kazi na mazingira ya kazi na kila unachokifanya kifanye kwa juhudi, kwa nguvu zako zote, akili zako zote na kwa moyo wako wote ili uweze kufanikiwa.

Narudia tena "Afrika ni bara la kukimbilia na ndiyo sehemu ya msaada wako USILIPUUZE"

LUCAS ROBERT
+255764075392
+255713056903
lucastrngwakwa@gmail.com

"Live an inspired life"