Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHITAJI MUHIMU YA MJASIRIAMALI: UTANGULIZI

       UTANGULIZI
Kabla hujawa mjasiriamali ni lazima ujue wewe ni nani, Ni muhimu kujua mjasiriamali ni nani, ana sifa gani na Anahitaji nini ili kuwa mjasiriamali. Katika masomo manane yaliyopita Yaliyokuwa na maada kuu "TAA ZA MJASIRIAMALI" Katika sehemu ya kwanza kabisa tuliongelea kuhusu mambo makuu mawili, Moja tuliangalia nini maana ya ujasiriamali na mjasiriamali?, Pili ni sifa za mjasiriamali. Ikiwa hukupitia nenda upitie kwa Sababu unaweza kuwa unajisemea kuwa wewe ni mjasiriamali kumbe siyo, Kumbe wewe ni mganga njaa tu.

 (KUSOMA "TAA ZA MJASIRIAMALI" BOFYA LINK)
https://ngwakwaufanisi.blogspot.com/2017/06/taa-saba-za-mjasiriamali-sehem-ya-kwanza.html?m=1

Pia kabla ya kuingia kuangalia mahitaji muhimu ya mjasiriamali naomba nikukumbushe pia kuwa kabla ya kuingia katika kiunga cha TAA ZA MJASIRIAMALI tuliangalia kuhusu umuhimu wa kujitambua kwa sababu hakuna mjasiriamali ambaye hajitambui.  Ndiyo maana kabla ya kumuelezea mjasiriamali nilitanguliza masomo yanayohusu kujitambua, kwamba wewe ni nani, unatoka wapi, Una sifa gani, kwa nini upo hivyo/hapo, na unatakiwa kufanya nini? Yote hayo yalijibiwa katika mfululizo wa makala zilizoruka hewani kwa kichwa kilichosema "UKWELI USIOPINGIKA". Katika makala hizo nililinganisha hatua za mafanikio ya mtu kama hatua za ukuaji wa mtoto, Mtoto anapozaliwa inabidi atengenezewe msingi imara, Atunzwe na kulelewa ipasavyo, Afundishwe kuanza kujitegemea, Ajitambue yeye ni nani na atambue mazingira aliyopo na mwisho ni lazima apange hatima yake au aweke malengo yake.

(KUSONA "UKWELI USIOPINGIKA" BOFYA LINK)
https://ngwakwaufanisi.blogspot.com/2017/04/ukweli-usiopingika-sehemu-ya-1-kuzaliwa.html?m=1

Naam, kama hukubahatika kuzisoma makala za ukweli usiopingika, Ni UKWELI USIOPINGIKA kuwa hautafaidi sana katika hiki tunachokiendea yaani "MAHITAJI YA MJASIRIAMALI"
>Usipange kukosa kutembelea blog hii inayojali kile unachokihitaji nawe hitajuta kwa kutoa muda wako kusoma kile kitakachokuwa kinaandikwa bali utagundua hazina zilizositirika ambazo inatakiwa kuzifichua na kuwa nazo kabla kuingia kuwa mjasiriamali wa kisasa na ambaye mafanikio yako ni dhahiri.

Karibu sana na Mungu akubariki.

LUCAS ROBERT
+255764075392 (WhatsApp tu)
lucastrngwakwa@gmail.com

*"LIVE AN INSPIRED LIFE"*