Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHITAJI MUHIMU YA MJASIRIAMALI: AFYA

HITAJI LA KWANZA: AFYA.
Afya ndiyo kitu cha kwanza ambacho mjasiriamali yoyote yule anatakiwa kukitafuta kwa nguvu zote. Waswahili walisema "mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe". Huwezi kuwa na nguvu bila kuwa na Afya bora. Unatakiwa ujari Afya yako katika nyanja zote, Kiakili, kimwili, Kiroho na kijamii.
Moja, Afya aya kiakili (mental health). Ni lazima kujali afya ya kiakili ili uweze kufikiri vizuri, Akili ndicho kiwanda chako namba moja, Lisha akili yako vitu ambavyo vitaifanya iwe na Afya bora, Tumia muda wako kusikiliza, kutazama au kusoma vitu vitakavyoamsha akili yako na kukutia hamasa kusonga mbele, Jenga mtazamo chanya hata pale unapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo, Kukata tamaa ndiyo hatua ya kwanza ya kushindwa, Ukiona unakata tamaa mapema ujue akili yako haina nguvu ya kutosha kuvumilia changamoto, na kuna uwezekano mkubwa ukawa na utapia mlo wa akili hivyo unahitaji kuirisha akili yako kwa chakula bora. Robert kiyosaki anasema "The size of your success is measured by the strength of your desire; the size of your dream; and how you handle disappointment along the way." - Robert Kiyosaki,  Kwa tafsiri isiyo rasmi anamanisha "Ukubwa wa mafanikio yako unapimwa na uimara wa matamanio yako; ukubwa wa ndoto zako; na namna unavyovumilia bila kukata tamaa unapokuwa njiani"
Huwezi kuota kile ambacho hufikirii maana ndoto ni matokeo ya kile unachofikiria na utaendelea kukifikiria mpaka utakapo fikia au kuikamilisha ndoto yako, Pia huwezi kuwa mtu ambaye hukuwahi kufikiria kuwa kwa sababu "Unavyofikiria ndivyo ulivyo". Lisha akili yako vitu vikubwa vyenye afya, Ili ufikilie vitu vikubwa na uwe mtu mkubw yule unayetaka kuwa. Na mwisho ili kuimalisha Afya ya akili yako, Epuka matumizi ya vitu vitakavyoichosha au kuidhoofisha akili  yako. Hivyo basi ikiwa hutajari afya ya kiakili kwa namna Yoyote ile utamtumikia mtu anayetumia akili yake vizuri, kwa kupenda au kutokupenda.

Pili, Afya ya kimwili (Physical health), Ili uweze kutekeleza majukumu yako kwa ufanisi ni lazima uwe na mwili wenye Afya. Dunia ipo katika mwendo wa kukimbia ikiwa afya yako ni mgogoro hutaweza kwenda kwa kasi kama dunia inavyokwenda, maana huwezi kufanikiwa kama wewe haujafika pale ambapo dunia imefika. Siri kubwa ya watu waliofanikiwa ni uwezo wa kufika kule dunia inapokwenda kabla haijafika. "Jana ni bora kuliko leo". Ili uweze kuishi vizuri leo ni lazima uwe ulifanya kazi vizuri jana lakini pia "Leo ni bora kuliko kesho" Tengeneza afya ya mwili wako leo maana unategemea afya ya leo ili ufike kesho. Watu waliofanikiwa hutumia muda mwingi katika kuboresha afya zao na wamewekeza vingi katika Afya zao. Ukihisi afya ya mwili wako haiko vizuri ni bora ukasitisha kile unachokifanya kwa muda uishughulikie kwanza na baada ya hapo ndipo uendelee vizuri. Hapo utakuwa umeepuka mambo makuu mawili, Kupoteza muda au kuharibu kazi (kazi isiyo na ufanisi) lakini pia utakuwa Umesalimisha Afya yako ambao ndio chanzo cha kile ulichonacho na mwili huo ndio unaouhangaikia.

Tatu, Afya ya kijamii. Katika mafanikio ya mtu yoyote kuna watu ambao wako nyuma ya mafanikio hayo. Watu hao wqnaweza kuwa ni ndugu (Wazazi, kaka, dada, mke au mme), marafiki wenye mawazo chanya, viongozi n.k. Mafanikio ambayo mtu anatakiwa kujivunia ni yale ambayo kipindi inafanikiwa wale waliokusaidia kufanikiwa pia wanafanikiwa. Unatakiwa ujisikie fahari kuona wale ambao wako chini yako wanafanikiwa kama ambavyo kuna uwezekano wewe wakati unafanikiwa wale ambao walikuwa juu yako walijivunia mafanikio yako na kukuona kama mmoja wao. Ni muhimu sana kujenga uhusiano mzuri na watu au jamii inayokuzunguka kwa sababu wao ndio ambao watakutengenezea ngazi itakayokuwezesha kupanda juu. Kuna msemo mmoja unaitwa - An inspirational quote by African Proverb about the value of Team Work: “If you want to go fast, go alone. If you want to go far, go together.”
Huu ni msemo wa kiafrika unaosisitiza katika kufanya kazi kama timu, ambao kwa tafsiri isiyo rasmi unamanisha kwamba "Ukitaka kutembea haraka tembea peke yako, lakini ukitaka kutembea umbali mrefu tembea na wenzako". Ni wazi kuwa kila aliyekaribu yako ana kitu kinachokufaa katika mafanikio yako, mthamini wala isimbeze. "Every one arround you is a gift which God has granted to you, Value him/her"

Nne na mwisho, Afya ya kiroho. Afya ya kiroho hukuwezesha kupata msaada pale ambapo nguvu za kiakili na kimwili haina msaada tena. Yapo mambo ambayo ukipigana kwa akili zako hautashinda kamwe. Unahitaji msaada wa Mungu, Au nguvu isiyokuwa ya kawaida (super natura power) ili uweze kufanikiwa zaidi. Afya ya kiroho inakuwa pale tunapoongeza imani yetu kwa Mungu, Kwa kuamini kuwa yeye ndiye mpaji wa vyote na ndiye ambaye anaweza kutulinda na kutuelekeza njia ambayo tunatakiwa kupita ili kufikia mafanikio yetu. "Mungu siku zote huingilia kati pale ambapo nguvu ya kibinadamu haina msaada tena" -"Man's extremity is God's Opportunity"  Ni lazima ufanye sehemu iliyondani ya uwezo wako kwa nguvu zote kabla ya kuomba msaada wa Mungu. "Do the best and God will Do the rest"

***Kwanini Afya Ndiyo kiwe kipaumbele Chako?
1. Ili kuongeza uzalishaji.
Miili yetu imetengenezwa kwa uwezo wa ajabu kwamba inao uwezo wa kuhisi mabadiliko. Tunaifanya miili yetu kama mashine yenye uwezo wa kuwekewa mafuta na kuendelea kuifanyisha kazi bila kuwa na muda wa matengenezo. Imekuwa ni kawaida kwamba mtu anapokuwa amechoka anajaribu kuondoa uchovu huo kwa kutumia vinywaji vya kuongeza nguvu na vyenye sukari nyingi. Mazoea haya ni mabaya sana. Habari njema ni kwamba ikiwa utajizoeza kufanya mazoezi na kula vizuri utajisikia kuwa na nguvu muda wote na kuwa na uwezo wa kufanya kazi kea nguvu na kuzalisha zaidi.

2. Kuepuka visababishi vya magonjwa.
Chochote ambacho itaweka kwenye mwili wako kinaweza kufanya kazi ya kuujenga mwili wako na kuufanya ufanye kazi vizuri(mtunda, mbogamboga na nafaka nzima), au vinaweza kufanya kazi kinyume chake na kusababisha mwili kufutuka na kulundikana kwa mafuta (vyakula vya kusindika, vikaangwa, na vyakula vyenye sukari nyingi).
Kama utaendelea kuingiza vitu vinavyoudhuru mwili utakuwa unakaribisha magonjwa kama vile magonjwa ya moyo na kisukari.
Pia bila kusahau mazoezi, Maisha ya kukaa muda mwingi husababisha magonjwa mwngi mbalimbali. Miili yetu haikuumbwa kukaa tu muda wote. Kama kazi yakl ni ya kukaa muda Mwingi hakikisha unapata muda wa kufanya mazoezi angalau kutembea mita 10,000 kwa siku.

3. Familia yako.
Watu wengi hiwa hawajali afya zao eti kisa wanajali familia zao, kiukweli kama unafanya hivyo utasabaishia familia yako matatizo zaidi ya unavyofikiria. Kama utaipa afya yako kipaumbele utakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi na kuitunza familia yako vizuri zaidi. Kama una watoto utakuw aunaweka mfano mzuri mbele yao kuhusu njia bora ya mafanikio. "Weka kipaumbele kwenye afya yako, kwa ajili ya familia yako"

"Kwa namna yoyote ile, Na kitu chochote kile hapa duniani utaweza kukitimiza ikiwa tu utakuwa na Afya bora. Afya bora inaanza na kile unachochagua kukifanya kila siku. Usipoteze muda, anza kufanya matengenezo ya afya sasa maana ndio njia kuu ya kukufikisha uendako".


Ndugu msomaji, Afya ndilo hitaji la kwanza kabisa katika ujasiriamali. Pamoja na kwamba ujasiriamali unahitaji utayari na wakati mwingine hata kujihatarisha, Unaweza kuhatarisha vyote, Mali, taaluma na hata marafiki unaoona hawakufai, lakini usije ukahatarisha Afya yako, Kwa sababu badala ya kupata vyote unaweza kupoteza vyote.
*"JALI AFYA YAKO"*

LUCAS ROBERT
+255764075392 (whatsApp only)
lucastrngwakwa@gmail.com

*"Live an inspired Life