Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHITAJI MUHIMU YA MJASIRIAMALI: WATU

HITAJI LA PILI: WATU.
Hitaji la taifa lolote ni hitaji la watu, Sio watu tu, Bali watu wenye ujuzi, Elimu na maarifa Na wenye utayari kufanya kazi kwa moyo na nguvu zote kwa ajili ya Taifa lao.
Mwandishi mashuhuri Ellen G. White katika kitabu chake cha kiingereza kiitwacho Elimu (Education), uk, 57 Anasema "Hitaji kuu la ulimwengu, Ni hitaji la watu, watu ambao hawatanunuliwa wala kuuzwa, watu ambao ndani ya Nafsi zao hasa ni waaminifu na wakweli. Watu ambao hawaogopi kuitaja dhambi kwa jina lake. Watu ambao dhamiri zao zina uaminifu kwa wajibu kama dira ionyeshayo ncha ya kaskazini. Watu watakaosimamia ukweli hata kama mbingu zinaanguka" Hao ndio watu wanaotafutwa. Je wewe ni miongoni mwa watu wanaotafutwa?
Binadamu anaweza kubadili dunia, nchi au kitu kingine kuwa namna anavyotaka kiwe.
>Jamhuri ya watu wa china ni nchi inayoongoza kwa idadi ya watu duniani, Sambamba na hilo asilimia kubwa ya watu wa china wana ujuzi au Elimu na uzalendo pamoja na kujituma kwa ajili ya Taifa lao, ndiyo maana Nchi ya china imefanikiwa kukua kwa kasi kubwa hii ni kutokana na sababu kwamba watu ndio mtaji namba moja wa taifa lolote.

Huo ni mfano tu wa Nchi zinazotumia rasrimali watu vizuri, Lakini kiuhalisia kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2013 ya shirika la OECD, wanapozungumzia wasomi, ni ile idadi ya watu waliomaliza elimu ya vyuo vikuu na walau mtu kua ana digrii moja.
>Kwa mjibu wa takwimu hizo nchi iliyokuwa inaongoza kwa kuwa na wasomi wengi URUSI, inayoongozwa na Rais Vladimir Putin ina jumla ya watu Milioni 144.1 (2015) kwa mujibu wa Banki ya dunia na ina jumla ya wasomi wapatao 53.5%.

>Ikifuatiwa na Canada yenye jumla ya watu milioni 35.85  kwa sensa ya mwaka (2015 ) Kutoka Benki ya dunia , Canada ina kiwango cha elimu ya chuo kikuu kwa 51.3%.

>Namba tatu ilishikiliwa na Japan iliyokuwa na watu wapatao milioni 127 (Kwa mujibu wa sensa ya benk ya dunia, 2015, na ni nchi inayoongoza kwa Teknolojia na Sayansi duniani. Japan ina kiwango cha elimu ya chuo kwa 46.4%.

>Namba 4 ilichukuliwa na Nchi ya Israel yenye kiwango cha elimu ya chuo kwa 46.4%.
Marekani ilikuwa katika nafasi ya tano ikiwa na kiwango cha elimu ya chuo kwa 42.5%.

>Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2015 chini ya Benki ya dunia ilibainisha uwepo wa watu wapatao milioni 50.62 nchini Korea, ikiwa ina kiwango cha elimu ya chuo 40.4% inayoipa nafasi ya sita kwa kiwango cha wasomi duniani.
>Namba saba ni Uingereza (UK) chini ya utawala wa Malkia Elizabeth wa pili na Waziri Mkuu Theresa May, Nchi hii yenye wakazi wapatao milioni 65.14 ina kiwango cha elimu ya chuo 39.4%.

>New Zealand ilishika nafasi ya nane ikiwa na wakazi wapatao milioni 4.596, na kiwango cha elimu ya chuo kwa 39.3%.

>Namba tisa Ilishikwa na Finland yenye kiwango cha elimu ya chuo kwa 39.3%.

>Na kumi ikiwa ni Australia yenye wakazi wapatao miloni 23.75 kwa mujibu wa Benki ya Dunia mwaka 2015, Na Kiwango cha elimu ya chuo ni 38.3%.

Ukiangalia katika nchi zilizomo kwenye namba kumi bora kwa wasomi duniani itagundua kuwa ni nchi ambazo zimeendelea na uchumi wake upo vizuri. Miongoni mwake utakuta ni nchi zinazoongoza kwa technologia na hata zipo nchi zinazoongoza kwa uchumi duniani. Hii ni kuashiria kwamba "Katika maendeleo ya taifa hitaji kuu ni watu wenye Elimu, Ujuzi na maarifa -wasomi".

> Viwanda vinahitaji nguvu kazi ili kuweza kuzalisha bidhaa, Wingi wa Malighafi pekee hauweze kufanya kiwanda kuwa na uzalishaji. Nguvu kazi au wafanyakazi wanaohitajika kwa ajili ya uzalishaji kiwandani ninakuwa katika makundi mawili:-
* Wafanyakazi wenye ujuzi au wataalamu (skilled labour) Na,
** Wafanyakazi wasio na ujuzi (Unskilled labour).
Pamoja na kwamba sehemu zote mbili za wafanyakazi zinahitajika lakini mojawapo ni ya muhimu zaidi na ikikosekana tu uzalishaji unaweza kupungua sana au kutokuwepo kabisa nayo ni Wafanyakazi wenye maarifa au wataalamu.

> Kama ambavyo Nchi yoyote inavyohitaji watu wenye ujuzi, Elimu na utayari wa kufanya kazi kwa nguvu na moyo wote, Kadhalika mjasiriamali kama taasisi au mtu binafsi anahitaji watu walio na Elimu, ujuzi na utayari wa kufanya kazi kwa nguvu na moyo wote. Kabla hajahitaji watu wenye ujuzi kutoka nje, mjasiriamali hana budi kuwa na ujuzi, Elimu na utayari wa kufanya kazi kwa moyo na nguvu zake zote kwa ajili ya mafanikio yake binafsi.
Sharti kutafuta maarifa, Elimu na ujuzi kwa namna yoyote ile kuhusiana na shughuli ambayo unakusudia kuifanya.
Kuna mtu mmoja alisema "Nikihitaji kufanikiwa nahitaji marafiki na ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui"
Lakini mimi ninasema hauna haja ya kutengeneza uadui na watu wengine, bali unatakiwa kutengeneza uadui na nafisi yako mwenyewe. Nafsi yako ndiye adui namba moja wa maendeleo yako na unatakiwa upambane naye na umfundishe kutenda kwa kadri ya matakwa yako.
"Asili ya mwanadamu ni kuwa mvivu katika kila kitu" Alisema Harriet Beecher Stowe, Ndiyo maana ametengeneza vitu kama vile baiskeli na matairi kwa sababu hapendi kutembea au kubeba vitu - Lech Walesa.
Kwa hiyo binadamu anafanya kazi kwa sababu anahitaji kuishi na bila kufanya kazi kuishi kwake kutakuwa ni kwa shida na maumivu tupu, Na wakati mwingine bila kufanta kazi anaweza kushindwa kuishi kabisa.
Adui ambaye unatakiwa kupambana naye kila siku ni moyo wa kutopenda kufanya kazi ambao upo kwa kila mtu.

Mwalimu alisema "Ili nchi iendelee na ipate maendeleo inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora". Mwalimu alikuwa na maana kwamba vitu hivyo vinne vinategemeana sana na kimoja kikikosekana huenda vingine vikashindwa kufanya kazi.
Na ifahamike kwamba mambo manne aliyoyataja Mwalimu hakuyataja kwa kubahatisha wala hakuyataja kirahisi, Kiuhalisia Mwalimu aliyataja kwa uzito wa kipekee, Na ukichunguza kwa makini kauli hiyo utakuta ameongelea vitu viwili Muhimu, Ardhi na watu, Na akasisitiza zaidi kuhusu watu wanaohitajika kuwa ni watu werevu watakaoleta siasa safi na uongozi bora.
Hivyo kwa maana nyingine "Hitaji kubwa ni hitaji la watu".
Hoja yangu haipo kwenye kujadili hotuba Ya Mwalimu bali nilitaka kuonesha ambavyo hata mwalimu pia alitambua umuhimu wa watu.

>Watu ndiyo kila kitu katika dunia na unapowataja unazungumzia watu ambao wapo kudhibiti dunia na kuifanya dunia iwe vile wanavyotaka. Kukiwa na watu ambao watataka kuiharibu dunia basi itaharibika, kukiwa na watu watakaotaka kuitengeneza dunia basi itatengenezeka.
> Sifa za watu salama ambazo zinaweza kuwa kipimo cha watu ni utu, uadilifu, uzalendo, umoja, uchapakazi, kujituma, kujitolea na mambo kama hayo.

Leo tunaweza kujipima juu ya aina ya watu tulionao, wakoje? Maana, kimsingi lazima tukubaliane kuwa  ili tuendelee tunahitaji watu kama kitu cha kwanza kama ambavyo nimetangulia kusema.

>Swali la kujiuliza? Mbona watu tunao, wako zaidi ya Milioni 55, kwa nini taifa letu halina maendeleo ya kuridhisha wakati limekamilisha hitaji la kwanza la maendeleo ambalo ni “watu?” Jibu la swali hili ni rahisi, watu tunao lakini hawana Elimu, ujuzi, maarifa, uchapakazi na moyo wa kujituma kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Sehemu kubwa ya hawa watu milioni 55 wanakosa sifa muhimu za kujiendeleza na kundeleza taifa; huyu hana elimu nzuri, huyu anauelewa finyu kuhusu kile anachofanya, yule hana maadili na nidhamu ya kazi, huyu si mchapakazi - mvivu, huyo si mzalendo, mimi siwezi kujitolea n.k.

Kama “watu” ni hitaji mojawapo la maendeleo, basi Tanzania inao watu wasiotumika kuleta maendeleo na wasioandaliwa mazingira ya kujiletea maendeleo – kwa hiyo tunaendelea kuwa taifa lenye “watu” jina na si “watu” kwa maana ya hitaji kwa ajili ya maendeleo.
Albert Einstein Alisema "Dunia ni sehemu hatari sana kwa kuishi, sio kwa sababu ya watu wanaofanya maovu duniani, bali ni kwa sababu ya watu ambao hawafanyi chochote". Alimanisha kuwa ukitaka dunia iwe mahali hatari sana kwako usijishughulishe na chochote, wewe kaa tu bila kufanya kazi utaona dunia itakavyokuwa hatari kwako.

Nchi yangu Tanzania inao watu wanaolalamika kwa kila kitu, Wakidai kuwa, Maisha ni magumu-(Vyuma vimekaza) "Wasomi tumekuwa wengi hivyo ajira hizitoshi", huku wakisahau kuwa zipo nchi zenye wasomi wengi maradufu kuliko wao na wala hawalalalamika kuhusu ajira.

Uwepo wa wasomi wengi wasio na ajira ni fursa kwa kila msomi mjasiriamali kwa sababu ukihitaji wafanyakazi wenye ujuzi (wataalamu) wapo kila mahali na wengi ni wale ambao umesoma nao. Ikiwa tungeamua kuikomoa serikali tungeweza, Tungeingia katika ujasiriamali ambapo tungezalisha mazao na bidhaa ambazo watumiaji ni sisi wenyewe na tungeendelea kuishi kwa uhuru bila kutegemea ajira huku serikali ikilalamika kuhaha kutafuta wafanyakazi ambao ingewaajiri katika miradi yake na ambao ingewapata kwa gharama kubwa kwa sababu watu wako bize na kazi zao binafsi.
> Usije ukanielewa vibaya, Juzi waziri Suleiman Jafo alisikika akisema, "Mkurugenzi wa kila wilaya lazima ahakikishe anafungua viwanda 100 ndani ya wilaya yake kabla ya mwaka wa bajeti 2017/2018 kuisha". Kiukweli mimi mwenyewe sikumuelewa lakini baada ya kutafakari nimegundua kile alichokisema kinawezekana. Viwanda alivyoongelea vinahitaji wataalamu ambao wapo mtaani na ndio wanaolalamika hawana ajira. Pamoja na kwamba mtaji ni changamoto kwa kila mmoja wetu lakini uwepo wa vitu muhimu kama Ardhi, Afya (nguvu) na Elimu tunayodai kuajiriwa kwayo tunavyo, hivi ndivyo vinaweza kutumika kama sehemu yetu ya kuanzia.
> Usisubiri mpaka uwe na mtaji wa mamilioni ndipo uanze biashara, ili uwe mjasiriamali au mwekezaji. Anza na kila ulicho nacho, tumia kile ulichonacho kufanya kile unachokipenda na utashangaa namna itakavyogeuka kuwa fursa kwako na kwa wengine pia. Kama wewe ni mtaalamu wa kilimo, tumia elimu hiyo kujiajiri, na usaidie wengine kuwaelimisha kuhusu njia bora za kilimo, Kama a wewe ni mwalimu, jitolee kufundisha wototo wa kijijini au mtaani kwako, baada ya muda utashangaa namna itakavyobadilika kuwa fursa. Kama una kipaji cha kuandika hadithi andika wape watu wasome hata kama ni bure, ipo siku utashangaa kilo ulichoanzisha kama sehemu ya kitu ukipendacho kitakavyobadilika na kuwa kiwanda cha kutengeneza pesa. "Anza sasa, anza hivyo hivyo ulivyo, anza na kile ulicho nacho, na badili hoby yako kuwa fursa"

>Wengi wanasema kwenye ajira ndipo ambapo kuna ulinzi kimaisha (Job security).
Lakini Bill Gate alisema "Sehemu yenye ulinzi muda wote ni gerezani, Na ukitaka uwe na ulinzi muda wote lazima uwe gereza yaani ukubali kuajiriwa na mwingine akulipe anavyotaka"

KWANINI WATU NI MUHIMU KWA MJASIRIAMALI?.
1.Ndio wateja wa huduma unayotoa.
Kipaumbele cha biashara yako lazima kiwe ni kutatua matatizo ya watu katika jamii na kisiwe kupata faida kupitia kuuza bidhaa. "Mthamini kila mtu bila kujali hali aliyo nayo maana huyo ndiyo anaeeza kuwa mteja wako au anaweza kukuletea mteja baadaye".

2. Ndio watakaokushauri kuhusu kile unachotakiawa kufanya.
Mjasiriamali sio mtu aliyeshiba maarifa na kuridhika kwa namna alivyo. Mjasiriamali au mfanyabiashara wa kweli siku zote huwa na kiu ya kupata maarifa na ushauri mpya kutoka kwa watu wengine, Ushauri huo haupatikani kwa miti au wanyama bali hupatikana kwa watu. Ni muhimu sana kupata ushauri kutoka kwa watu waliobobea, watu wenye uzoefu au watu waliofanikiwa kupitia kitu kinachafanana na kile unachokifanya.

3. Ndio wa kuwaiga - Watu wa mfano. (Role model).
> Ni vizuri sana kuwa na Mtu wa mfano Kocha- (Role model) wa maisha yako ili uweze kufanikiwa. Mtu huyu atakusaidia kugundua makosa, kujua vitu muhimu unavyotakiwa kuvifanya na kujupatia ushauli na mwelekeo kuhusu safari ya mafanikio yako. Mtu wa mfano siyo lazima awe mtu ambaye alifanikiwa mara moja pasina kuanguka bali anaweza kuwa mtu yoyote ambaye inafurahishwa na mfumo wake wa maisha na unayefikiria kuwa ungependa kumuiga. "Watu wazuri sana tunaowafahamu ni wale tuaofahamu kushindwa kwao, Tunaofahamu masumbufu yao, tunaofahamu juhudi zao, tunaofahamu walivyopoteza, Na wale ambao wamefanikiwa kuipata njia yao kutoka katika kina kirefu. Mtu huyu huwa anautambuzi, hisia, uelewa wa maisha uliojaa uaminifu, ubinadamu na upendo wa kweli. Watu wema sio kwamba wanatokea tu" Alisema -Elisabeth Kübler-Ross

4. Ndio watakaokutia moyo mambo yanapokuwa magumu.
> Kitu ambacho unatakiwa kukiogoma sio kujaribu, unatakiwa ajaribu mara nyingi mpaka ufanikiwe, Bali unachotakiwa kukiogopa kuliko vyote na kukata tamaa. Wapo watu ambao watukukumbusha hasara ya kukata tamaa na mara nyingi watakutia moyo kusonga mbele na kukuonesha jinsi ambavyo umeyakaribia mafanikia yako na watakukumbusha gharama ulizotumia mpaka kufika hapo ulipo. Watu hawa wanaweza kuwa marafiki, ndugu, jamaa, wazazi mke au mme. Wanasema "Nyuma ya mtu aliyefanikiwa lipo kundi kubwa la watu". Pamoja na hilo Wakati mwingine anaweza asiwe mtu mwingine tofauti na wewe mwenyewe.
5. Ndio utakaofanya kazi nao (utakaoshirikiana nao) - Co-workers
> Ni bora kutembea wawili kuliko kutembea mmoja kwa maana akianguka mmoja mwingine atamuinua, Anaendelea kusema, Lakini ole wake atembeae peke yake pindi atakapoanguka ni nani atamuinua?. "United we stand divided we fall". 

6. Ndio watakaokusaidia kukufanyia kazi.
> Hakuna mtu ambaye yuko vizuri katika kila eneo kuna eneo ambalo upo vizuri kuliko mtu mwingine yeyote lakini pia lipo eneo ambalo upo vibaya kuliko woye, Hivyo katika eneo ambalo hauwezi inahitaji mtu ambaye atakusaidia kulifanya kwa namna ambayo litafaa zaidi. Kitu ambacho tuanshindwa kuelewa ni kujilazimisha kufanya mambo ambayo tunajua kabisa hatuwezi na badara ya kuboresha tunaharibu kabisa, wakati kama tungemualika yule ambaye ni taaluma yake angetusaidia na mwisho wa siku mambo yangeenda vizuri zaidi.
8. Ndio watakaokutia wivu wa maendeleo.
> Ukiwa umezungukwa na watu walofanikiwa, watu wanaoendesha magari mazuri, wenye nyumba nzuri na maisha yao hayawapigi chenga, bila shaka utatamani sana siku moja uje uishi maisha kama wao. Usijute kuzungukwa na watu wanaokuzidi kipato bali watumia kama hamasa itakayochoma moyo ili uwezo kufanikiwa. Kuzungukwa na watu waliokuzidi kimaisha si jambo baya, na watu hawa ni wa muhimu sana unaweza hata kuwaomba ushauri namna ya kufika huko waliko.
9. Ndio unaofanya kazi kwa ajili yao.
> Mara nyingi tunafanya kazi kwa ajiri ya watu, Tunafanya kazi kwa ajili ya watoto wetu, Familia zetu na wakati mwingine tunafanya kazi kwa ajili ya watu wengine wasiojiweza ambao bila shaka  wanauhitaji sana msaada wetu. Ni lazima pia kukumbuka mafanikio yako ni mafanikio ya watu wanaokuzunguka pia. Watu wenye mafanikio hufurahia kuona wengine wakiinuka kimaisha.
10. Wewe ni zawadi kwao.
"Kila mtu aliyekuzunguka ni zawadi ambayo Mungu amekupatia"
Bila kujali ni ndogo kiasi gani, Dhaifu kiasi gani, Chafu kiasi gani lakini ni ya Muhumu sana kwako, Na kama hutaithamini ipo siku itakuwa haipo tena na ndipo utakapokumbuka Umuhimu wake.

*"KILA MTU ALIYEKUZUNGUKA NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU, ITHAMINI*

>Lakini napenda kukuambia tu kuwa wewe hapo una kitu ambacho mimi sina na ikumbukwe kuwa wewe kama zawadi kwa ulimwengu unatakiwa ukitoe kile ambacho Mungu alikuleta uweze kukitimiza.

>"Kila mtu atatoweka duniani baada ya kukamilisha kusudi uliloletwa kwalo"
Tumia uwezo wako wote kabla hujanyang'anywa wote.

*You should go away exhausted because you will be remembered by what you gave but not what you got*


C. Joybell C. alisema, "Ni lazima tukubali kupendwa na watu ambao kweli wanatupenda, na ambao kweli ni wa muhimu. Mara nyingi tumepofushwa macho na  na matakwa ya watu kutupenda, na watu ambao hata sio wa muhimu, huku tukipoteza muda kutembea na watu wasiotupenda huku wakituangalia namna tunavyoteseka kuomba omba mitaani" akahitimisha kwa kusema " Huu ni wakati wa kujiachia kupendwa na watu"

> Ni kweli kwamba watu ni wa muhimu sana katika maisha ya mjasiriamali, lakini uchaguzi wa watu utakaoshirikiana nao hauna budi kufanywa kwa makini sana.
Kama nilivyo tangulia kusema kuwa hitaji la mjasiriamali ni hitaji la watu, watu wenye utayari, walio na ujuzi na maarifa katika jambo wanalofanya, hao ndio wanaofaa kuingia katika tathinia ya ujasitiamali. Na mtu wa kwanza ni wewe mwenyewe.


_Yours_
Lucas robert
+255764075392 (whatsApp only)
lucastrngwakwa@gmail.com

"LIVE AN INSPIRED LIFE"