KUFIKIA KILELE CHA MAFANIKIO.
Bila Shaka kila mtu aliyezaliwa na mwanadamu ambaye ana akili timamu anatamani Sana siku moja afikie mafanikio ya juu sana katika maisha yake. Ukweli ni kwamba mafanikio hayo hayafikiki bila kufanya chochote. Ikiwa una ndoto za kufanikiwa katika kitu chochote unachofanya lakini hufanyi chochote wewe ndiye ambaye unaifanya dunia iwe mahali pabaya kabisa pa kuishi.
Mwana Fizikia wa kijerumani Albert Einstein (1879 - 1955) alisema, "Ulimwengu ni sehemu hatari kwa kuishi, Sio kwa sababu ya watu waovu ,bali ni kwa sababu ya watu ambao hawaifanyii chochote" Hivyo ili angalau ufae kuishi katika ulimwengu huu na ufanikiwe ni lazima ufanye kitu.
Ili kufikia kilele cha mafanikio ni lazima ufanye vitu muhimu sana vitano;;
1. Kuwa na Lengo katika maisha.
Usiishi Kama kipofu, kuwa na Lengo la kufika sehemu fulani. Vunja vunja malengo yako katika sehemu ndogo ndogo na ujipe muda maalumu wa kuyatimiza. Hatua kwa hatua panda ngazi moja baada ya nyingine mpaka ufike ulipokusudia kufika. Weka malengo makubwa ambayo Yatakupa hamasa ya kufanya kazi kwa nguvu ili uweze kuyafikia.
2. Tafuta maarifa muda wote.
Bila kuwa na maarifa huwezi kufanikiwa maishani, Lakini maarifa pekee bila hekima hauwezi kufanikiwa zaidi. Ili uweze Kukuza taaluma yako, hauna budi kutafuta maarifa mengi kwa kadri iwezekanavyo. Maarifa pia ni ya muhimu katika Kutengeneza utu wetu, Kurekebisha tabia zetu pamoja na kujua named ya Kushughulika na watu. Katika Niall ya kuelekea mafanikio yako utakutana na watu wa aina tofauti tofauti hi to no muhimu pia kuwa na Hekima na maarifa kuhusu namna ya Kushughulika na watu.
Usichoke kujifunza ili kujipatia maarifa kila kunapokucha, maarifa ni kama matofali ambayo utayatumia ili kupanda kwenda juu. Elimu Hainan mwisho. Pale unapojisikia kuridhika na maarifa uliyonayo na kukosa hamu ya kupata maarifa mapya hapo ndipo anguko litakapokujia.
3. Fanya kazi kwa bidii.
Kazi ndiyo heshima ya MTU. Wengi tunataka heshima na mafanikio bila Kufanya kazi kwa bidii. Mtu mmoja alisema "asilimia kubwa ya watu wenye mafanikio SAA kumi na moja asubuhi huwakuta wako macho, wakiwa Wameshaamuka tayari ama wakiwa wanakwenda Kuala". Huo ni mfano tu lakini lengo ni kuonesha jinsi gani ilivyomuhimu Kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufanikiwa. Mchawi mkubwa wa mafanikio ya kila mmoja wetu ni uvivu. Maandiko matakatifu biblia katika kitabu cha Muhubiri 9: 10 imeandikwa "Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe". Kabla hatujatoka duniani ni lazima tuhakikishe tunatumia nguvu zetu za mwili na akili Kufanya kazi kwa bidii. "Juhudi inalipa".
4. Kuwa Mvumilivu.
Gharama ya mafanikio ni kubwa Sana, hasa pale unapokuwa na ndoto kubwa. Gharama ya mafanikio ni kitu ambacho unatakiwa kulipa kutoka kwenye maisha yetu. Mafanikio ni kitu ambacho kina madai mkubwa Sana kiasi kwamba kinaweza kutunyang'anya hata vitu muhimu sana Kama gharama au malipo ya mafanikio.
Akili au kipaji pkekee hakitoshi kukufanya ufanikiwe ikiwa Hautavumilia changamoto na maumivu mbalimbali. Uvumilivu ni tabia Inayokuruhusu Kuendelea Kusonga mbele. Hii ni nguvu ya ndani ambayo inakusaidia kupuuza changamoto, maumivu au vikwazo unavyokutana navyo na kujikaza Kusonga mbele kuelekea malengo yako au njia uliyoichagua. Kwa vile njia ya mafanikio ni ngumu bila kuwa na uvumilivu itakuwa ni rahisi sana kukata tamaa pale unapokutana na changamoto au vikwazo.
5. Fanya urafiki (Na Mungu na watu chanya).
Maarifa tuliyonayo, vipaji tulivyonavyo, Kufanya kazi kwa bidii pamoja na uvumilivu wetu havitaweza kutuletea mafanikio ikiwa hatatakuwa na uhusiano mzuri na Mungu wetu pamoja na binadamu wenzetu. Mungu ametuahidi mafanikio ikiwa Tutazishika sheria zake ambazo maana yake halisi ni Upendo: Upendo kwa Mungu na Upendo kwa Wanadamu wenzetu. Kumbukumbu la torati 4:40 inasema "Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo Bwana, Mungu wako, milele"
A. P. J Abdul Kalam, mwanasayansi na mwasiasa wa kihindi ambaye pia ni Raisi wa 11 wa India alisema "Usiache kupambana mpaka utakapofika katika sehemu Unayotakiwa kufika, kuwa na Lengo maishani, Endelea Kujiongezea maarifa, fanya kazi kwa bidii na uwe na uvumilivu ili uweze kufikia maisha ya hali ya juu".
Ili ufikie ndoto yako ni lazima ulipe gharama, Ikiwa ni pamoja Kuchelewa kwenda Kulala na kuwahi kuamka, kuwa na marafiki wachache na Kutokueleweka kwa wengi, Kijisikia kulemewa na kujihoji kuhusu utimamu wa akili zako pamoja na kujipa moyo hata kama hakuna Anayekutia moyo au anayekubali kile unachokifanya.
Lipa gharama ili uweze kufikia kilele cha mafanikio yako.
Karibu katika safari ya mafanikio na huu ndio mwanzo tu.
Lucas Robert
+255764075392
lucastrngwakwa@gmail.com
"Live an inspired Life"
