NAMNA YA KUPATA WAZO ZURI LA BIASHA.
Mtu mmoja alisema "Kila unachokiona katika ulimwengu wa mwili kilianza katika ulimwengu wa roho". Vile Vile Kila biashara unayoiona ilianza Kama WAZO. Mafanikio ya biashara yoyote hutegemea wazo la biashara, mazingira na mikakati wezeshi katika kufanikisha biashara hiyo.
*NAMNA YA KUPATA WAZO ZURI LA BIASHARA KIRAHISI.....*
Wazo zuri la biashara imekuwa Ni changamoto Ambayo inawatesa watu wengi wanaotamani kuanzisha biashara.
________________________________________________________________________________
Kuna uwezekano umehitimu chuo, Lakini Unajiuliza Ni Aina gani ya biashara itakayokuingizia kipato kinachotesheleza mahitaji yako...
Pengine wewe Ni mjasiriamali ambaye umekuwa ukianzisha biashara Baada ya muda inasambaratika na kufa, na kupoteza mtaji wako wote...
Wewe kijana upo hapa unao mtaji wa kutosho Lakini hujui hujui uanzie wapi ili uweze ujiajiri...
Wakati mwingine uliwahi kuingia katika biashara Ambayo marafiki zako wa karibu walikuwa wakiingiza faida kubwa Lakini wewe ulivyojaribu ukashindwa vibaya sana, Ukaangukia pua na kuishia kupoteza mtaji!.....
Kama unapitia au umewahi kupitia Mojawapo ya changamoto nilizozitaja hapo juu👆, Ujumbe Huu Ni kwa ajili yako...
Hapa Kuna Taarifa Muhimu Sana itakayokuwezesha kujua Ni wapi ulikuwa unakosea, kabla ya kuanzisha biashara yako!!
P.S: Lengo la Biashara inatakiwa kuwa Ni Kutatua Tatizo Fulani katika jamii. Wakati kupata Pesa inatakiwa kuwa Ni matokeo ya kutatua Matatizo ya wateja wako.
Wengi tumekuwa tukianzisha biashara bila hata kujua Biashara hiyo inataka kutatua tatizo gani!
Usianze kuanza biashara kwa kutazama faida utakayoipata tu, Bali Anza biashara kwa kuangalia Ni tatizo gani utakaloenda kulitatua kupitia huduma yako au bidhaa yako.
Watu wapo tayari kulipia kiasi chochote kununua utatuzi wa tatizo lako.
Mara nyingi unapokutana na wateja Lakini Kila unapomtajia tu Bei ya bidhaa au huduma yako anaishi kukwambia "Bei yako Ni kubwa", Au "Ngoja nijipange Kwanza", "Nitakutafuta" na kauli nyinginezo zinazoashiria kabisa kwamba anataka kukwepa huduma yako,
......... Hapa Tambua kabisa kwamba mteja wako hajajua Kama huduma au bidhaa yako inatatua tatizo lake.
*NAMNA YA KUPATA WAZO ZURI LA BIASHARA*
Njia nzuri ya kupata wazo Zuri la biashara Ni kuangalia tatizo fulani linalokabili kundi fulani la watu Kisha tafuta suluhisho lake.
Tembelea katika maofisi katika mji unaokaa, Ongea na Wafanyakazi wake, waulize Ni changamoto inayowakera Zaidi katika shughuli zao, waulize kiasi ambacho wako tayari kukulipa ikiwa utawasaidia kuondokana na Tatizo Hilo, Waambie kuwa unalo suruhisho la tatizo Lao, Angalia namna wanavyofurahi kupata uruhisho Hilo, Baada ya hapo kaa Chini tafuta suruhisho la tatizo Lao. Baada ya hapo Rudi kwao Kama (mtaalamu) professional wa Jambo Hilo.
*Mpaka hapo Tayari Umeshapata wazo zuri la Biashara*
Mfano: Wafanyakazi wengi wa maofisini wanakabiliwa na kuwa na vitambi na uzito mkubwa Kutokana na kukosa muda mwingi wa kufanya mazoezi, Hivyo unachotakiwa wewe Ni Kutafuta namna ya kuwasaidia kutatua tatizo lao pasipo kuathiri shughuli zao.
Ukifanikiwa kupata suluhisho la tatizo Hilo kweli kweli Nakuhakikishia pesa zitakuja Kama mvua.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Tembelea kwa wakulima ongea nao kuhusu changamoto mbayo inawakera katika shughuli zao, waulize kwamba Kama ukiwasaidia kutatua changamoto iyo wako tayari kukulipa kiasi gani? Waambie kuwa unalo suruhisho la tatizo Lao, Angalia namna wanavyofurahi kupata suruhisho Hilo, Baada ya hapo kaa Chini tafuta (buni) suruhisho la tatizo Lao. Baada ya hapo Rudi kwao Kama (mtaalamu) professional wa Jambo Hilo.
Bila shaka utaanza kugundua kuwa hapa Kuna wazo la kukuingizia kipato.
Kwa mfano: Wakulima wengi wanasumbuliwa na kukosekana kwa soko na Bei nzuri ya mazao Yao, Kutokana na kukosekana wa mfumo unaowaunganisha na wateja wao. Kazi yako wewe Ni kutengeneza mfumo unaowaunganisha wakulima na wanunuzi wa mazao Yao au wewe mwenyewe uwe kiunganishi au daraja Kati ya Wakulima na wanunuzi wa mazao. Nakuhakikishia ukifanikisha Hilo Wakulima watakulipa vizuri Sana mpaka utashangaa...
NB: (i)Kujenga professional Ni Somo lingine zito Sana (Ninahitaji muda kulielezea) ila La muhimu Sana kabla ya kuingia sokoni.
(ii) kuwa professional Siyo lazima uwe na Elimu ya Darasani juu ya kile unachotaka kukifanya, Bali unahitaji skills tu muhimu...
Jamii tunamoishi imejaa Matatizo ya Kila Aina na inahitaji watu wa kuyatatua ili iweze kuwalipa. Kundi moja Lina Matatizo tofauti na kundi jingine.
P.S: Unatakiwa kulenga kundi fulani mahususi kwa ajili ya kulisaidia kutatua changamoto zinazowakabili. Usijaribu kutatua tatizo la Kila mtu. Biashara inayomlenga Kila mtu maana yake haimlengi mtu yoyote.
KUMBUKA: Binadamu siku zote Ni mbinafsi, Anaangalia faida yake Kwanza kabla ya kuangalia faida ya mwingine. Mtu hayuko Tayari kutoa Pesa yake kwa ajili ya kukunufaisha wewe, Ila Yupo Tayari kutoa kiasi chochote ili kujinufaisha yeye tu.
Hakikisha kile unachotoa kinamsaidia mteja wako kwelikweli la sivyo wazo lako la Biashara halitafika mbali litakufa...
Kipaumbele chako kisiwe Pesa, kipaumbele chako kiwe tatizizo la mteja wako.
Mfanye mteja wako aone anakupunja kwa kutoa Pesa yake kununua huduma au Bidhaa yako. Na Hii Mojawapo ya mbinu zinazotumika kuuza bidhaa zenye Bei kubwa kirahisi. (Namna ya kuuza Bidhaa za Bei kubwa kirahisi Ni somo pana na linahitaji muda pia).
Natumaini umeeleewa Namna ilivyorahisi kubuni wazo zuri la Biashara itakayokuingizia faida kubwa Katika mazingira yoyote kwa mtaji kidogo.
Kama bado unahangaika kupata wazo zuri la Biashara litakalokupatia kipato Cha kutosha na Endelevu Usisite kuwasiliana nami.
Nitakupatia wazo la Biashara lililofanyiwa utafiti Tayari Katika hatua zote, na utaweza kulifanyia kazi Katika mazingira uliyopo kwa mtaji mdogo Sanaa.
_______________________________________________________________
Piga simu/ WhatsApp sasa +255786216172
Au gusa Link hapa Chini ili uweze kuwasiliana nami moja kwa moja.
https://wa.me/message/VQBA7BVUJWUKA1
P.S: Wazo zuri la Biashara Ni msingi wa mafanikio ya Biashara yoyote kwa hukupatia Taswira halisi ya kile utakachokipata Katika biashara yako. Hivyo wekeza muda wako hapa ili usije ukapoteza mtaji wako kwa kuwekeza Katika wazo la Ovyo.
