FAHAMU JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA MPYA HATARI WA HOMA YA MARBURG
Homa Ya MARBURG Ni ugonjwa hatari Sana ambao unasababishwa na virusi Aina ya Marburg. Virusi hawa wapo katika kundi la virusi wanaosababisha kutokwa na damu katika sehemu mbalimbali za mwili (viral hemorrhagic fever)
Virusi wa MARBURG hupatikana katika Aina Fulani ya popo wanaopatikana mapangoni.
Virusi hawa hupatikana katika majimaji ya mwili wa mwathirika Kama vile kinyesi, matapishi, damu, jasho, mkojo, mate na makohozi.
Ugonjwa Huu unaathiri binadamu na wanyama wengine walio katika familia moja na binadamu (primates) Kama vile Nyani, sokwe na ngedele.
DALILI ZA UGONJWA WA MARBURG.
Dalili za ugonjwa wa homa ya marbug zimegawanyika katika sehemu mbili,
(a) Dalili za awali/mwanzo
(b)Dalili za baadaye
Mgonjwa wa homa Ya MARBURG huweza kuonesha dalili za awali Kama ifuatavyo:-
1.Homa Kali
2.mwili kuishiwa Nguvu
3.maumivu makali ya kichwa
4.Maumivu ya Misuli
5. Macho kuwa mekundu
6. Vidonda kooni
7.vipele kwenye ngozi
8.maumivu ya Tumbo.
Dalili za baadaye za ugonjwa wa homa Ya MARBURG Ni Kama ifuatavyo:-
1. Kutapika damu
2. Kuharisha damu
3. Kutokwa na damu puani
4.vidonda mdomoni na kutokwa na damu
5. Kutokwa jasho jingi
NAMNA YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA MARBURG
1.Epuka kugusa majimaji ya mwili wa mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Marburg Mfano, kinyesi, Jasho, mikojo, mate, matapishi na damu
2. Nawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara
3. Epuka kugusana na mtu mwingine Kama vile kusalimiana kwa kushikana mikono, kukumbatiana au kubusiana.
4 Epuka kula au kugusa mizoga ya wanyama Kama vile, popo, Nyani, tumbili na swala wa mwituni.
5. kuchangia Nguo, matandiko, kitanda, miswaki au vyombo vya chakula na mtu mwenye dalili za ugonjwa wa marbug.
6.Epuka kuosha maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa MARBURG pasipo kuwa na vifaa vya kujikinga.
7. Wahi au muwahishe mtu mwenye dalili za ugonjwa Kama zilivyoainishwa hapo juu katika kituo Cha kutolea huduma za afya kilicho karibu.
Toa Taarifa haraka pindi uonapo mtu mwenye gonjwa dalili za ugonjwa wa marbug.
Tuma ujumbe mfupi kwa kuandika Nene TETESI (herufi kubwa) ikifuatiwa na jina la wilaya uliyopo Kisha dalili za mgonjwa kwenda namba 199.
KUMBUKA: ugonjwa wa MARBURG unazuilika, Jikinge, waking wengine.
Fanikiwa na Afya yako tunajali afya yako na ya wale uwapendao.
Tafadhali share ujumbe Huu na wengine uweze kuokoa maisha yao.
Ahsante kwa kujali

