Matajiri huwa wanakuwa mtazamo chanya. Na hiki ndicho kinawatofautisha na watu maskini. Huwa wanakabiliana na changamoto ya kushindwa kwa kauli Mona tu "NINAWEZA". Matajiri hutumia kufeli kama njia ya kujifunza ili kufanikiwa kwa kutorudia makosa yaleyale. Mara zote hupenda changamoto na huwa hawaogopi kuchukua hatua hatarishi.
Kama unataka kuwa bilionea, angalia tabia yako. Tabia yako ina mchango mkubwa sana katika mafanikio yako, watu wenye mtazamo chanya, msukumo chanya na wenye uwezo ndio ambao hufanikiwa.
Unaweza kufanikiwa ikiwa utakuwa na kukuza Tabia zifuatazo ambazo mabilionea huwa nazo:
1.Tabia ya ubunifu Ubunifu.
Ubunifu ni kitendo cha kuleta wazo kitu kipya chenye thamani, chenye kuleta faida au kutatua tatizo katika jamii. Mafanikio yetu hutegemea sana namna tuna to both amino na kuwathamini wengine, pia hutegemea namna tunavyotatua matatizo yetu na matatizo ya wengine. Hivyo ubunifu wa kuleta vitu vipya vyenye thamani na vyenye uwezo wa kutatu matatizo ni kitu cha muhimu sana ili tuweze kufikia mafanikio tunayoyatamani.

2.Tabia ya Kujiamini
Kujianini ni namna tunavyojichukulia au kujithamini. Watu ambao wamefanikiwa ni wale wanaojithamini na kujichukulia kuwa wanaweza. Habari jemba ni kwamba unaweza kujifunza kujiamini kupitia mazoea ya kufanya vitu na kujitathimini mwenyewe na kujichukulia kuwa unaweza. Kujiamini huanza ndani ya moyo. Kujiamini kunakusaidia kufikia shabaha pasipo kuyumba.

3.Tabia ya kuweka Malengo makubwa
Huwezi kuwa kile ambacho hujawahi kufikiria kuwa. Watu waliofanikiwa walifikiria kuwa vile walivyo kabla hawajawa. Waliweka malengo na wakawa na nidhamu kuyafikia. Kwa hiyo ni muhimu kuweka malengo ya kuwa MTU yule unayetaka kuwa hata kama unaona ni ngumu au itachukua muda mrefu kufanikiwa.
4.Tabia ya Ujasiri
Ujasiri tunaoongelea hapa ni uwezo wa kurejea haraka katika hali ya kawaida baada ya kukutana na ugumu, changamoto, tatizo au janga. Si kweli kwamba watu wenye mafanikio hawakumbani na vitu vinavyoweza kuwatoa kwenye njia au hali yao ya kawaida, La wanapata. Lakini kinachowasaidia kuendelea mbele ni ule uwezo wa kurudi katika mapambano haraka baada ya changamoto.
5.Tabia ya Kupenda kufanikiwa
Mtu mwenye mafanikio huwa na kiu kubwa ya mafanikio, Shauku yake ya kufanikiwa ni kubwa kuliko changamoto anazokutana nazo. Mwelimishaji katika maswala ya ujasiriamali kutoka marekani, Robert Kiyosaki anasema "The size of your
success is measured by the strength of your desire; the size of your dream; and how you handle disappointment along the way". Kwa tafsiri isiyo Rasmi anamanisha "Ukubwa wa mafanikio yako hupimwa kwa uimara wa hamasa yako, Ukubwa wa ndoto yako, na namna unavyoshughulikia kukatishwa tamaa njiani"
6.Tabja Kuinuka baada ya kushindwa au kuanguka (wanajua Namna ya kushughulika na kushindwa).
Watu waliofanikiwa wana mtazamo tofauti kuhusu kushindwa. Hawaogopi kushindwa maana wanatambua kushindwa ni njia ya kujifunza.
Kushindwa msongo wa mawazo.
Mtu mwenye mafanikio ni lazima awe na uwezo wa kushughulika na kuushinda msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo hupunguza uwezo wa kufikiri vitu chanya vitakavyokuletea mafanikio. Msongo wa mawazo huweza kumfanya MTU akae katika njia panda muda mrefu bila kufahamu ni njia IPI iliyo sahihi kuifuata.
7.wana Kipaji cha uongozi.
Kiongozi hushirikiana na wengine ili kuweza kufanikisha lengo lililokusudiwa. Mtu mwenye mafanikio hujisikia amani kabisa kutembea kwa ushirikiano na wengine, Uwaonesha njozi kubwa aliyonayo ambayo ikifikiwa itamnufaisha yeye na wale alioshirikiana nao.
8.Wana nguvu (energetic)
Unaweza ukawa unatamani kufanikiwa na kuwa tajiri kwa sababu hauna nguvu ya kukufikisha huko. Nguvu tunayoongelea hapa ni uwezo wa kuchangana, kuchambua na kutumia mawazo chanya kwa Ufanisi. Ili MTU awe na afya ya kimwili anahitaji kula chakula Bora. Kadharika katika sehemu hii akili yako inatakiwa kuwa na nguvu kwa kupata chakula chake, Kujihusisha na watu chanya, kusoma vitabu vyenye hamasa na kula vyakula vinavyoboresha afya ya mwili na akili.
9.Wanapenda kuwasiliana (Sociable).
Kujitenga na watu ni kuukimbia utajiri kwa sababu utajiri hutoka kwa watu. Ili ufanikiwe hauna budi kuwa MTU wa watu, MTU anayechangamana na watu. Kupitia kuchangamana na watu utaweza kuziona / kuziona fursa ambazo zinaweza kukuingizia pesa.
10.Hupenda Kukabilika (adaptable).
Mtu mwenye mafanikio siyo MTU wa kuogopwa, ni MTU ambaye unaweza kumkabili na kumweleza jambo. Kuna baadhi ambao hufikiri kuwa kuruhusu mianya ya kuzoeana na watu wengi kutakupotezea pesa, Pasipo kujua wamejifungia milango ya mafanikio maana hawajui kuwa watu wa karibu yako ndiyo ngazi kuekekea mafanikio.
Tabia hizi siyo kwamba kila MTU amezaliwa nazo, Bali huweza kujifunza.

Tengeneza na kukuza tabia za MTU mwenye mafanikio ndani yako.
Utajiri ni tabia, jenga tabia za kitajiri. "Ishi kama unamiliki benki siyo kama unataka kuomba mkopo benki"
Lucas Robert
+255764075392
lucastrngwakwa @gmail.com
*"Live an inspired Life "*
Utajiri ni tabia, jenga tabia za kitajiri. "Ishi kama unamiliki benki siyo kama unataka kuomba mkopo benki"
Lucas Robert
+255764075392
lucastrngwakwa @gmail.com
*"Live an inspired Life "*