Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUNZISHA BIASHARA MPYA NA KUISIMAMIA MPAKA IFANIKIWE

 Jinsi ya kuanzisha na kukuza Biashara mpya kwa Haraka...


Kila mwaka Biashara nyingi Sana zinaanzishwa, lakini pia kila mwaka Biashara nyingi Sana zinashindwa kuendelea na kufa. 


Bila Shaka utakubaliana na Mimi katika hili kwa kutazama Biashara nyingi zilizokuwepo miaka kadhaa iliyopita katika eneo lako hivi Sasa hazipo, na Kuna Biashara nyingine nyingi mpya ambazo zipo hivi Sasa.


Pamoja na hayo zipo Biashara chache amazo zimejipambanua na zinazidi kukua na kujipanua licha ya kwamba zingine yawezekana hazina muda mrefu.


Je unafahamu Hii Ni kwa sababu gani?


Yapo mambo kadhaa ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuanzisha Biashara yako mpya na wakati unaendesha Biashara yako mpya.



Kabla hujaanza Biashara unatakiwa kuzingatia au kujiuliza mambo yafuatayo:

1. Lengo la kufanya biashara

Kwa Nini unataka kufanya Biashara hiyo?

Wengi tunataka kufanya Biashara ili kujiingizia kipato kitakachoboresha maisha yetu. Lakini kiuhalisia hili halitakiwi kuwa kipaumbele chako. 

Kipaumbele Cha kuanzisha Biashara yako kinatakiwa kuwa Ni kutatua changamoto zilizopo katika jamii yako. Fanya utafiti katika jamii ili kujua Kuna tatizo gani lililopo katika jamii yako ambalo ukilitatua watu watakuwa tayari kukupa pesa zao.

Biashara itakayoanzishwa katika mfumo Huu itakuwa vigumu Sana kufa. Weka furaha ya mteja wako kuwa ndiyo kipaumbele chako.


2. Mlengwa wa Biashara yako.

Mteja wa Biashara au huduma yako Ni Nani?

Kama ukifanikiwa katika hatua ya kwanza ya kujua Ni tatizo gani utakalotatua katika jamii, manake Ni kwamba utakuwa unamjua mwenye tatizo na ndiye atakayekuwa mteja wako.

Katika Biashara usimlenge kila mtu, Biashara inayomlenga kila mtu maanake Ni kwamba haijamleonga yeyote. Lazima utengeneze chujio litakalochambua kati ya wateja wako sahihi na wale ambao siyo sahihi.

3.Bidhaa au Huduma

Hapa Kama umeshajua tatizo unaloenda kulitatua kwa mteja uliyemkusudia hatua inayofuata Ni kubuni na kutengeneza bidhaa au huduma Bora itakayotatua tatizo Hilo. Tengeneza suluhisho sahihi kwa ajili ya tatizo la mteja uliyemkusudia. 


Baada ya kuanza Biashara ili Biashara yako iweze kuendelea na kukua yapo mambo ya kuzingatia:-

1. Matangazo

Matangazo ndiyo uti wa mgongo wa biasgara au huduma yoyote.

Ili Biashara yako iweze kukua Ni lazima iwe na wateja. Hukuna mtu atakayejua kwamba unatoa huduma Fulani au bidhaa Fulani. Hata uwe na  bidhaa Bora kiasi gani hakuna atakayetambua ubora wa bidhaa yako Kama hujamwambia. Mtu mmoja alisema "Kuwa na Biashara pasipo kuitangaza Ni sawa na kumkonyeza msichana kwenye Giza"

Kwa hiyo kwenye kila faida utakayoipata katika Biashara yako hakikisha unatenga kiasi Fulani kwa ajili ya matangazo, kwa sababu matangazo Zaidi ndiyo yatakayokuletea faida zaidi.

Kitu kingine cha muhimu sana cha kuzingatia ni aina ya matangazo na njia utakayotumia kutangaza biashara yako. Chagua njia ya matangazo inayoendana na biashara yako.




2.Nidhamu  ya fedha

Ili Biashara yako iweze kusimama na kudumu lazima uwe na nidhamu ya fedha. Iheshimu fedha inayotokana na Biashara yako. Ni muhimu Sana kuweka Malengo na utaratibu wa namna pesa inayopatikana kutokana na Biashara yako na uhakikishe unazifuata. Siyo kwamba kwa sababu umefanya mauzo makubwa leo Basi ukalewe au umnunulie zawadi kubwa mpenzi wako, Na Wala siyo kwamba kwa vile pesa Ni ya Biashara Basi uishi kwa kujitesa, fuata mpango wako uliojiwekea, usifanye manunuzi ya bidhaa kwa hisia au kwa maahindano ukatoka kwenye utaratibu.


3.Malengo

Kama hujui unakoenda Basi maanake huendi popote. Kuweka Malengo maanake Ni kuona au kuwa unakoenda kabla hujafika. "If you fail to plan you are planning to fail" kwa maana isiyo rasmi Ni kwamba ukishindwa kupanga (Malengo) maanake unapanga kushindwa (Kufikia Malengo). Weka Malengo makubwa ila yanayofikika, Kisha pambana kuhakikisha kwamba unayafikia. 


4.Kuwa na mwendelezo (consistency).

Wakati unafanya Biashara au unapotoa huduma unatakiwa kuwa na mwendelezo wa kufanya kile unachofanya. Hii Ni mojawapo ya kitu muhimu Sana kuwa nacho katika utoaji huduma au bidhaa, kwa sababu inakufanya ufahamike na uzoeleke sokoni na kukufanya upate wateja zaidi.

Kwa kawaida siyo rahisi mtu kununua kwa asiyemfahamu vizuri, Ni muhimu Sana kujitambulisha kwa wateja wako mara kwa mara na hasa kwa kuwapatia bidhaa au huduma katika viwango vya juu Zaidi.

Ni muhimu ukatambua kuwa unapoanza Biashara Fulani wazo lako litakuwa na ugumu katika kukubalika lakini pia panaweza kuwepo na washindani ambao wanakuwa na bidhaa au huduma Kama zako, Hivyo mwanzoni inaweza pita muda wa kukatishwa tamaa lakini mwendelezo utakufanya ukubalike na kuingia katika akili za wateja. Hii itakufanya kuwa wa Kwanza kuja katika fikra ya mteja pindi anapohitaji kupata huduma Fulani.

Kitu kingine Cha kuzingatia hapa Ni kutokubadilisha badilisha bidhaa au huduma unayotoa mara kwa mara, na ikitokea unataka kuibadilisha fanya kwa utaratibu maalumu na kuwajulisha wateja wako kabla ya kufanya Hivyo.


Mpendwa msomaji nipende kukwambia tu ukifuata taratibu hizo kabla ya kuanzisha Biashara na wakati unaendesha Biashara yako nikuhakikishie tu kwamba Biashara yako itadumu na itapanuka kwa haraka Zaidi.


Ni Mimi mwalimu wa mafanikio LUCAS ROBERT

Kwa maoni na ushauri Unaweza kuniandikia katika kibox Cha maoni hapo chini.

Au Nipigie/sms +255764075392

Email: lucastrngwakwa@gmail.com


"Live an inspired life"