Ticker

6/recent/ticker-posts

VITU SABA (7) VINAVYOPIMA MAFANIKIO YAKO MIAKA MITANO IJAYO

 VITU SABA (7) VINAVYOPIMA MAFANIKIO YAKO MIAKA MITANO IJAYO

Watu wengi hujilaumu kwa Nini hawapigi hatua za mafanikio tofauti na wenzangu ambao wameanza nao kazi au wenye umri Kama wao?

Mafanikio hayaji Kama ajali, mafanikio Ni matokeo ya dhamira ya kweli ya kuyatafuta mafanikio kwa kufanya mambo sahihi kwa wakati sahihi.



Yafuatayo Ni mambo Saba ya muhimu Sana ambayo yanaweza kutathimini mafanikio yako miaka mitano ijayo:

1.Vitabu unavyosoma

Miongoni mwa vitu ambavyo vinakuwa na matokeo (impacts) kubwa katika maisha yako Ni usomaji wa vitabu. Hii Ni kutokana na sababu kwamba kusoma kunahusisha sehemu nyingi za mwili Kama vile mikono, macho na ubongo. Chagua vyema na kwa makini Aina ya vitabu unavyosoma maana matokeo yako Ni makubwa pengine kuliko ulivuokuwa unafahamu.


2. Akaunti za mitandao ya kijamii unayofuatilia.

Mitandao ya kijamii hivi Sasa inachukua Zaidi ya 30% ya muda wa watu walio wengi. Kama tujuavyo katika mitandao ya kijamii asilimia kubwa ya Taarifa unazoziona zinatoka kwa marafiki na watu au akaunti ulizozifollow. Hivyo chagua akaunti unazozi-follow  ziwe Ni zile ambazo zinaendana na kile unachotaka kuwa.


3. Chakula unachokula.

Chakula ndicho kinatengeneza wewe.

Kuna msemo usemao 

"you are what you eat"              

 >wewe Ni kile unachokuala.

Kile unachokula na vile unavyokula kina mchango mkubwa Sana katika mafanikio yako, Ulaji mbovu unaweza kupelekea afya yako kuzorota na kupunguza Nguvu yako ya kufikia mafanikio unayoyatamani.


4. Watu ambao unatumia muda wako mwingi nao.

Utafiti unaonesha kwamba "mafanikio yako Ni wastani wa watu wako watano wa karibu ambao unatumia muda mwingi pamoja nao". Chagua vyema wale ambao unatumia muda mwingi pamoja nao. Epuka watu hasi, watu ambao wanaweza kukuvunja moyo muda wote, watu ambao hawana imani hawawezi kukutia moyo kwamba inawezekana. Kama binadamu wakati mwingine tunachoka, tunakata tamaa au tunachoka Hivyo watu tunaotumia muda mwingi nao ndio wanaweza kututia moyo na kutupatia nguvu za kuendelea.

5. Taarifa unazofuatilia.

Kuna msemo wa kizungu usemao "information is power". Taarifa unazofuatilia au unazopokea zina nguvu kubwa Sana ya kukufanya kuwa mtu Fulani. Fundisha akili yako kufuatilia Taarifa ambazo zina manufaa kwako. Taarifa unazofuatilia zinatakiwa kuwa Ni zile ambazo zitakuwa matofali ya mafanikio yako.


6. Mazungumzo unayofanya.

Mazungumzo nayofanya yanaweza kukujenga au kukubomoa, mazungumzo nayofanya yanaweza kukuletea watu au vitu vitakavyokuwa na msaada katika maisha yako au hasara. Chagua kwa makini mazungumzo unayofanya, Aina ya watu unaofanya mazungumzo nao, mnazungumza kuhusu Nini? na wakati gani unafanya mazungumzo.

 7.Watu unao wasikiliza

 Siyo kila mtu unapaswa kumsikiliza, ukimsikiliza kila mtu Bila Shaka hautakuwa na msimamo na mwiho wa Siku utapoteza mwelekeo. Ni vizuri kuwa na watu wachache ambao unawasikiliza. Ni Bora wakawa watu waliokuzidi na wenye maadili mema, wawe watu ambao wanakuongoza katika njia sahihi kwenye mafanikio yako.



PS: Kwa ufupi tu niseme "Kile unacholisha mwili na ubongo wako, ndicho kinachokutengeneza wewe, na ndicho kinachopima kwamba utakuwa mtu wa namna gani".

Mambo haya Saba ndiyo yanayotengeneza Aina ya mtu anayetaka kuwa miaka mitano ijayo. Kama ukichagua vyema katika mambo hayo Saba na kuweka msisitizo katika mambo chanya si muda mrefu utakuwa Aina ya mtu anayetaka kuwa.


Weka sehemu hizo katika vitendo na ninakuhakikishia kuwa utakuwa Aina ya mtu unayetaka kuwa, na utatimiza ndoto zako.


Ni Mimi Lucas Robert

Mdau wa mafanikio yako.

+255764075392


"Live an inspired Life"