MBINU ITAKAYOKUFANYA UBAKI SOKONI
Hapa tunaenda kujifunza namna ya Kuongeza idadi ya wateja kwenye biashara yako.
Kama wewe unuza bidhaa yoyote (Nguo, magari, vipodozi, vifaa vya ujenzi na kadharika.
Au kama unatoa huduma yoyote (Shule, mgahawa, hotel, stationery) andiko hili Ni kwa ajili yako.
NAMNA YA KUTANUA WIGO WAKO WA BIASHARA
Bila Shaka kila mtu anapokuwa anaanzisha Biashara Fulani lengo Ni kwamba ikue na Kufikia watu wengi kwa kadri inavyowezekana. Lakini Cha kushangaza Zaidi Biashara nyingi hufamiaka michache baada ya kuanzisha.
kuhusiana na watu ambao
Miaka kadhaa hapo nyuma shirika la utafiti huko Chini marekani lilifanya utafiti kuhusu watu wanaoanzisha biashara zao ili kujiajiri, Na iligundulika kuwa
>Biashara mpya ambazo zinaanzishwa takribani 20% huwa zinakufa katika miaka miwili ya kwanza tangu zilipoanzishwa.
>Huku 45% huwa zinakufa ndani ya miaka mitano baada ya kuanzishwa.
>Na 10% huwa zinakufa ndani ya miaka 10 ya kuanzishwa.
✓Ni 25% ya biashara mpya ndizo zinafanikiwa kufika zaidi ya miaka 15
Unapoamua kufanya Biashara yoyote ile tambua kabisa kwamba utakutana na ugumu pamoja na ushindani. Ili uendelee kubaki sokoni na kupanua wigo wako wa kupata wateja ni lazima uhakikishe unajiweka katika mazingira ambayo yatakufanya uendelee kubaki sokoni.
Hapa chini tunaenda kujifunza mbinu ambazo zitakufanya uendelee kuuza bidhaa yako au huduma yako kwa muda mrefu Zaidi huku ukiendelea kukua na kujipanua Zaidi.
1.Ongeza ujuzi.
Unapokuwa unafanya Biashara mambo mengi yanabadilika kila siku. Ili uendelee kubaki sokoni na Biashara yakokupanuka Zaidi inabidi uweze kujinoa kila siku ili uendelee kuzalisha kila bidhaa Bora au kutoa huduma Bora. Kuongeza ujuzi maana yake Ni Kuongeza uwezo wa kuwahudumia wateja wako, pamoja na kukabiliana na changamoto inazijitokeza.
- Katika changamoto nyingi Kuna fursa nyingi. Kwa hiyo kila changamoto itakayotokea katika Biashara yako itakulazimu Kuongeza ujuzi Fulani ili uweze kunyakua fursa inayopatikana ndani yake.
2.Fanya Tathimini sahihi ya soko (Market analysis)
✓Tathimini sahihi ya soko itakufanya ubaki sokoni. Fanya utafiti kuhusu wateja wako Ni kina Nani na wanaopatikana wapi, Ni vitu gani vinavyowafurahisha wateja wako, pamoja na vile inavyowakwaza wateja wako.
Katika kutathimini soko usiwe na upendeleo, pima kwa haki na Kama kitu kinakugusa rekebisha haraka uwezekanavyo.
3.Zalisha bidhaa kulingana na soko.
✓Bidhaa unayozalisha ni kwa ajili ya mteja siyo kwa ajili yako. Hivyo unapokuwa unataka kuzalisha bidhaa angalia hitaji la mteja na siyo hitaji lako, angalie Kile anachokipenda mteja wako siyo Kile unachokipenda wewe. Siyo Jambo baya kumuuliza mteja wako kuhusu Kile anachokipenda. Mteja yuko Tayari kulipia Kiasi chochote kulipia Kile ambacho Ni hitaji lake hasa na Kile anachokipenda.
4.Boresha Mahusiano yako na mteja
✓Hakikisha Mahusiano yako na mteja yanakuwa ya kudumu. Wasiliana mteja wako hata baada ya kupata huduma. Muulize namna alivyojisikia kupata huduma yako, na namna anavyoendelea baada ya kupata huduma. Mfanye ajisikie nyumbani, ajisikie kupata ndugu/ rafiki na anakubalika kwako
- Mthamini mteja wako Kiasi kwamba aone bidhaa yako ndiyo Bora
5.Kuwa mbunifu
✓Jifunze kuwa na mbinu bunifu kwenye bidhaa yako au katika utoaji wa huduma yako.
Bidhaa Ina Mahusiano mazuri Zaidi na mteja kuliko wewe. Hivyo hakikisha unaongeza Ubunifu utakaomfanya mteja wako avutiwe kutumia huduma au bidhaa yako Tena na Tena. Ifanye ionekane ya pekee na aone Hakuna ya kulinganishwa nayo.
Kama mzalishaji Ni muhimu kujua Bidhaa yako inahitajika wakati gani, katika Hali gani, na kwa namna gani.
Uwe makini katika mchakato wa uzalishaji wa bidhaa yako. Elewa vizuri malighafi unayoitumia.
Iwe na uwezo binafsi wa kuzalisha wateja zaidi
Bidhaa yako inafanya kazi ya kukutangaza (kwa ubora au ubaya)
6.Penda na thamini bidhaa yako.
Hakuna atakayethamini unachokifanya Bila wewe mwenyewe Kwanza kukithamini na kukipenda. Sema vyema bidhaa yako kwa wakati wote. Elewa vizuri Kile ambacho bidha/huduma yako inatatua na uwe Tayari muda wote kueleza Kile kinachotatuliwa na bidhaa au huduma yako. Onyesha ubora was bidhaa yako ukilinganisha na wengine.
7.Jali hisia za wateja wako.
Tafiti zinaonesha kwamba wateja hununua Zaidi kwa hisia Kisha kuthibitisha ubora wake baadaye. Kwa hiyo Ni muhimu ukajifunza kuelewa na namna ambavyo mteja wako anajisikia na uungane naye katika Hilo. Usipende kumpinga au kuonekana kutokujali utampoteza na hutampata Tena.
Kuwa tayari kukutana na changamoto za wateja. Wakati mwingine changamoto inaweza kutokea wakati wa utoaji huduma au wakati wa kutumia bidhaa yako. Kwa haraka inavyowezekana hakikisha unatatua changamoto hiyo na kuomba radhi kwa Kile kilichotokea.
Mhakikishie kwamba haitajirudia Tena na wewe kwa upande wako uhakikishe kweli haijirudii Tena.
Ifanye Biashara iwe Ni yake, Ni kwa ajili yake na inatatua tatizo lake na vinginevyo.
8.Tangaza bidhaa yako.
Matangazo ndiyo mapigo ya moyo ya Biashara yako, yakisimama tu ujue Tayari Biashara yako inajiandaa kwenda kaburini. Hata Kama uwe na bidhaa au huduma Bora kiasi gani Hakuna atakayejua bila kumwambia.
Tengeneza matangazo yenye uhalisia, yawe na mwendelezo lakini yasiyokera Wala kumkwaza mteja wako. Tangazo lako siku zote liwe linabeba utambulisho wa bidhaa, huduma, kampuni au taasisi yako. Hii itamfanya mteja wako kukumbuka kirahisi.
Matangazo yanatakiwa kubaki katika kumbukumbu za mteja wako ili itakapofika wakati wa kufanya uchaguzi wewe uwe wa Kwanza kuja katika machaguo yake na Hivyo itakuwa rahisi kukuchagua wewe miongoni mwa washindani wengine.
KUMBUKA mteja huwa hapendi kununua kitu ambacho hajakizoea au kununua kwa mtu ambaye hajamzoea.
9.Weka Mikakati ya kusonga mbele
Ili uendelee ubaki sokoni kwa muda mrefu unatakiwa kuwa na mipango endelevu na ya muda mrefu kuhusu Biashara yako. Tengeneza mazingira yatakayoipa uhai Biashara yako kwa muda mrefu, ifanye Biashara yako iweze kujisimamia na kujiendesha hata pasipo uwepo wako binafsi.
Miongoni mwa sababu zitakazofanya Biashara yako iwe na uwezo wa kujiendesha kwa muda mrefu hata pasipo wewe binafsi kuwepo Ni pamoja na:
✓Kuwa na Mahusiano chanya na jamii inayotuzunguka.
Hii itakuwezesha kuwa na wateja wa kudumu wanaokuamini na kukuheshimu daima. Pia inakuongezea ulinzi wa bidhaa zako, huduma na Mali zako kwa ujumla.
✓Jenga uwezo wa kuongeza wateja wapya kila Siku. Tengeneza mfumo utakaomfanya mteja kuleta mteja mwingine. Mpe motisha mteja atakayekuletea mteja mwingine.
✓Bei ya bidhaa
Bei ya bidhaa mteja anaweza kuihusianisha na ubora wa bidhaa yako. Fanya utafiti kabla hujapanga bidhaa yako, Bei ya bidhaa yako huwa inaashiria mambo mengi Sana kwa mteja. Bei haitakiwi kuwa chini Sana kiasi kwamba mteja akawa na wasiwasi na ubora wa bidhaa yako au ikawa ya juu Sana kiasi kisichoendana na matokeo halisi. Chunguza pia Bei za washindani wako ili ujue namna ya kucheza na upya sokoni.
✓uza bidhaa au huduma.
Kuna tofauti ya kufanya matangazo na kuuza. Unaweza kufuatwa na wateja wengi lakini ukashindwa kuwauzia bidhaa au huduma yako. Kuuza Ni kuleza Kile ambacho mteja atakipata ukilinganisha na pesa anayoitoa. Uza matokeo ya bidhaa yako. Mfanye mteja wako aone thamani ya pesa anayoitoa Ni ndogo ukilinganisha na faida atakayoipata kwa kutumia huduma au bidhaa yako. Hii itamlazimisha mteja wako kukupa kiasi chochote, wakati wowote pasipo kuwa na visingizio.Tengeneza umahili katika uuzaji wa bidhaa yako.
✓Ridhisha kila mteja.
Tumia uwezo wako na ujuzi ulio nao kuhakikisha unamridhisha mteja. Jitahidi kusikiliza kwa makini wateja wako kabla hujajibu, usiogope kuuliza Kama umeelewa vizuri hitaji lake au changamoto yake. Weka umakini mkubwa kwa mteja mmoja na weka matatizo binafsi nje ya Biashara yako.
- Heshimu uwepo wa kila mteja
- Epuka kubeza mtejela kwa sababu ya yeyote ile, iwe mwonekano wake.
- Shughulika na mteja uliyeanza naye.
- Shika jambo moja kwa wakati mmoja.
✓Boresha mahusiano miongoni mwa watoa huduma wako
Watumishi wawe na Mahusiano mazuri wao kwa wao, wathaminiwe na wathaminiane wao kwa wao. Hii itawafanya wawe na ari kubwa ya utendaji kazi na Hivyo Kuongeza uzalishaji katika Biashara yako. Wapatie uhuru wafanyakazi wako, uhuru wa kusikilizwa, uhuru wa kutoa maamuzi na uhuru wa kufanya maamuzi yaliyo ndani ya mipaka yao. Weka mpango mathubuti wa kuwaendeleza kielimu, waongeze maarifa.
Biashara yoyote itakayozingatia mambo hayo tisa itabaki sokoni kwa muda mrefu Sana na Wala haitatokea hata siku moja ikakosa wateja.
Kwa maoni na ushauri usisite kuniandikia maoni yako
Au piga simu/WhatsApp number +255786216172
"Live an inspired Life"

